TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Haha
Wanaboa mno, tatizo hata Njiro lipo ila sie tuliwaita wakatubadilishia line. Sisi ile line ilikuwa kila asubuhi lazima ukatike, na jumamosi haupo siku karibu nzima

Ni hatari pia kwa usalama wetu na mali zetu
 
Nipo Kimara kwetu huku.Nilivyoona mvua tu nikajua nanuna sasa hivi,na kweli TANESCO mvua ni maji lakini yamekushinda.Ushakata umeme.Na malalamiko nnayosoma humu inaonekana nchi nzima kuna tatizo la umeme kimya kimya.
 
Hapa Kimara mwisho line hii ya mavurunza inaanzia Ubungo inaishia machijioni Kimara.Hii line kila panaponyesha mvua lazima umeme ukatike.

Ni line ndogo lakini imebeba Dawasco,Hospitali,kambi ya jeshi,Tra,makanisa,misikiti,vyuo,shule na taasisi nyingi,na mji wenyewe wa Kimara sokoni na madukani vyote viko upande huu.Ni jambo la kuhuzunisha umeme unapokosekana eneo kama hili kwa sababu zile zile kila mara.Kuna transfoma zinasumbua katika line hii kila mara mvua ikinyesha lazima zilete shida.Mojawapo naijua mimi ni ile iliyopo maeneo ya shule ya Ebonite.

Kama mimi mwananchi wa kawaida naweza kujua tatizo la Tanesco,nyinyi wenye kazi yenu mnashindwaje kujua miundombinu dhaifu muiondoe na kuweka ile ambayo haisumbui watu nyakati zote,za mvua na jua,peak hours etc?!mnatuharibia sana shughuli kwa mambo yale yale.

Mimi nakusaidia tanesco,nenda kimara fanya uchunguzi,badilisha haya madude yenu mojawapo lile la pale Ebonite,ni mabovu,yanatusumbua wakati wa mvua.Acheni uzembe.Hatutaki umeme ukatike,hata mvua inyeshe vipi.Na huu ni msimu wa masika.Mnataka kusemaje?kwamba tukae home sasa hakuna kazi?!
 
Tumeambiwa tusizurure hovyo bila ya kuana safari ya muhimu ili kuepukana na maambukizi ya CORONA, sasa kukaa home nako joto kali, umeme hamna wamekata yaani ni tabu.

Yaani naona bora nikazurure tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nimetuma maombi ya kubadirishwa kwenda kwenye Zero tariff kupitia App yenu lakini imekuwa kimya sijapata majibu yoyote kutoka kwenu. Mwanzo nilikuwa kwenye matumizi ya Zero tariff lakini mita ikaaribika sasa toka nimepewa mpya hii huduma sijaipata kabisa. Namba ya mita ya zamani ni 01319958011,. Namba ya mita mpya Ni 43021919931 , Eneo Mwanza Ilemela.
 
TANESCO,

Nasikitika sana kumekuwa na ukataji wa umeme karibu kila siku kwa masaa kadhaa, kupelekea jana kuunguliwa na Tv yangu kwa sababu ya kuja na kuondoka kwa umeme, baada ya kufuatilia naambiwa ni karibu mji mzima wa mbeya umeme unakatika. Mbona hatupewi taarifa yoyote kama kuna mgao wa umeme, na kwa mimi niliyeunguliwa na Tv mtanilifund???

Wadau hebu tujuzane, huu ni mgao ama ni hitilafu za kwaida???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa watu inabidi watumie nguzo za zege, hii miti imezidiwa umri kila siku inaanguka na ndio reason yao ya ukatikaji wa umeme kuwa miundo mbinu mibovu kutokana na mvua,

Ili wawe na plan B inabidi watimuliwe kazi kidogo ndio watapata akili maana wanasubiri hadi shida itokee ndio warekebishe.
 
Salaam wakuu wa humu jukwaani.

Kwa siku nne mfululizo sasa kumekuwa na tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara hasa nyakati za jioni.
Hali hii inasababisha adha kubwa kwa wananchi watumiaji wa umeme katika mji wa Shinyanga na viunga vyake.
Kwa upande wa Shirika la umeme nchini Tanesco ofisi ya Shinyanga wamekuwa na kigugumizi kuhusu sababu hasa ya tatizo hili.

Wito wangu kwa Tanesco, ninawaomba wajitahidi kutoa taarifa za uhakika kwa wateja wao hasa wamiliki wa viwanda pindi wanapotaka kukata umeme ili kuepusha hasara zinazojitokeza mara kwa mara.

Sent using honor
 
Tanesco wa Kisarawe wana dharau sana,

Watu wanaenda kuwaambia tatizo wanaandika kwenye kompyuta kisha wanakuambia tutakuja hapo sasa ndo wanakaa miaka hawatokei, yani wewe uwe unaenda na kurud tu kwao kueleza shida moja.

Watu hawafanyi biashara kwa ajil yao, wakazi wa kisarawe tunawaulizb mtabadilika lini? Na kazi yenu ipi hapo ofisin kwenu? Tanzania ya viwanda itawezekana mtu hapati umeme miezi sita! Mnakera
 
Back
Top Bottom