Hapa Kimara mwisho line hii ya mavurunza inaanzia Ubungo inaishia machijioni Kimara.Hii line kila panaponyesha mvua lazima umeme ukatike.
Ni line ndogo lakini imebeba Dawasco,Hospitali,kambi ya jeshi,Tra,makanisa,misikiti,vyuo,shule na taasisi nyingi,na mji wenyewe wa Kimara sokoni na madukani vyote viko upande huu.Ni jambo la kuhuzunisha umeme unapokosekana eneo kama hili kwa sababu zile zile kila mara.Kuna transfoma zinasumbua katika line hii kila mara mvua ikinyesha lazima zilete shida.Mojawapo naijua mimi ni ile iliyopo maeneo ya shule ya Ebonite.
Kama mimi mwananchi wa kawaida naweza kujua tatizo la Tanesco,nyinyi wenye kazi yenu mnashindwaje kujua miundombinu dhaifu muiondoe na kuweka ile ambayo haisumbui watu nyakati zote,za mvua na jua,peak hours etc?!mnatuharibia sana shughuli kwa mambo yale yale.
Mimi nakusaidia tanesco,nenda kimara fanya uchunguzi,badilisha haya madude yenu mojawapo lile la pale Ebonite,ni mabovu,yanatusumbua wakati wa mvua.Acheni uzembe.Hatutaki umeme ukatike,hata mvua inyeshe vipi.Na huu ni msimu wa masika.Mnataka kusemaje?kwamba tukae home sasa hakuna kazi?!