TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Kuna matapeli wawili wanapita huku mitaa ya Chanika nyeburu wakiwachangisha watu fedha ili wawafanyie mpango Wa Umeme haraka wana uniform na Vitambulisho vya tanesco

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunakuomba toa taarifa polisi au serikali ya mtaa pia ofisi zetu za maeneo hayo wakati wanafanya tukio hilo ili watiwe mbaroni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwann sh 5000 napata units 14 wakati mwingine kwa pesa hiyo anapata 41units?

from kibiti
 
Kuna mgao nini au just coincidence, j3 iliyopita umeme ulikatika toka saa tatu ukarudi saa 11, leo tena j3 saa tatu umekatika tena, kama mgao tujulishwe tujiandae!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumetokea hitilafu kwenye Grid ya Taifa ya umeme, Mikoa mengi wanakosa umeme.

Shirika linahakikisha huduma inarejea ndani ya muda mchache.

TANESCO tunaomba radhi sana kwa usumbufu unajitokeza kwa sasa

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Kumetokea hitilafu kwenye Grid ya Taifa ya umeme, Mikoa mengi wanakosa umeme.
Shirika linahakikisha huduma inarejea ndani ya muda mchache.
TANESCO tunaomba radhi sana kwa usumbufu unajitokeza kwa sasa

TANESCO "Tunayaangaza maisha"
Mikoa ipi hasa itaathirika mkuu!?
 
Nikilipia luku mpya 515600 wiki ya 3 Leo sijafungiwa umeme mnachukuaga muda gan kuweka umeme (ni nguzo moja yaitajika)
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUOMBA RADHI

Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi Wateja wake waliounganishwa katika Gridi ya Taifa kwa katizo la umeme lililotokea majira ya Saa 7:32 Mchana.

Jitihada za kutatua tatizo hili zinaendelea, hadi kufikia saa 8:00 mchana baadhi ya Mikoa imeanza kupata umeme.

Taarifa rasmi kuhusu hitilafu hiyo itatolewa pale uchunguzi utakapokamilika.

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu


IMETOLEWA NA:- OFISI YA UHUSIANO
TANESCO MAKAO MAKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzinduzi wa Miradi ya REA 3 mkoa wa Rukwa
TANESCO
6a9d1460effabd65ed600832e1c2407e.jpg
d00c7f0d569daf3b6cf26bda37437eb7.jpg
62f33a476c708bc8e780d54217e6d339.jpg
aede2c4c280bab6ad3698072cdc9fb19.jpg


TANESCO "Tunayaangaza maisha"
 
Tanesco Arusha tulipeni fidia zetu au tumepanga tuende mahakamani ikifika mwisho Wa mwezi huu August 2017 .hamna ataa aibu mnazungusha watu miaka 2 naa sasa .mnatoa sababu za kijinga eti mkurugenzi ajasaini cheque .miaka miwili mkurugenzi aja saini tuu .mnatia hasira sana .

Yaani sioni ataa tofauti ya Uwepo Wa Raisi Magufuli na kauli yake ya hapa kazi tuu. Yaani Sijui ni raisi Wa Dar es salaam tuu.Huku Arusha ni kama tumetelekezwa mambo ni Yale Yale ya enzi ya Kikwete na tena mbaya zaidi sasa .ofisi za umma zimegeuka kama magenge ya ualifu Wa kupangwa .

sio bure kila Raisi Magufuli akifika mikoani anapokelewa na mabango .shame on you Tanesco Arusha and the likes ,
 
Tanesco Arusha tulipeni fidia zetu au tumepanga tuende mahakamani ikifika mwisho Wa mwezi huu August 2017 .hamna ataa aibu mnazungusha watu miaka 2 naa sasa .mnatoa sababu za kijinga eti mkurugenzi ajasaini cheque .miaka miwili mkurugenzi aja saini tuu .mnatia hasira sana .Yaani sioni ataa tofauti ya Uwepo Wa Raisi Magufuli na kauli yake ya hapa kazi tuu. Yaani Sijui ni raisi Wa Dar es salaam tuu.Huku Arusha ni kama tumetelekezwa mambo ni Yale Yale ya enzi ya Kikwete na tena mbaya zaidi sasa .ofisi za umma zimegeuka kama magenge ya ualifu Wa kupangwa .sio bure kila Raisi Magufuli akifika mikoani anapokelewa na mabango .shame on you Tanesco Arusha and the likes ,
Mpendw mteja wetu
Tunaomba taarifa zifuatazo
Jina
Namba ya simu
Na fidia ya eneo au kitu gani

TANESCO MAKAO MAKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom