MSAADA KUPATA CONTROL NAMBA TAFADHALI

Niliandika barua ya kupata clntrol namba ili nifanye malipo ya huduma nyumba yangu ipo umbali wa mita 89 kutoka kwenye nguzo ya huduma .

yapata miezi miwili sasa kila nikifuatilia naambiwa nitapewa taarifa kwa meseji, sidhani kama utoaji wa control namba tu unaweza kuchukua muda wote huu nsona kabisa hapa kuna mazingira ya rushwa yanatengenezwa.
 

Mkuu mita 89 ni nyingi sana, je hapo katikati kuna nguzo?, je vipi survery amekuja?
 
Tafadhali tusaidie

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Pia je ulipimiwa? Maana control number mpaka upimiwe ndio upewe makadirio halisi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mita 89 ni nyingi sana, je hapo katikati kuna nguzo?, je vipi survery amekuja?
Wameshafanya survey mkuuu... utaratibu wa sasa kama upo umbali zaidi ya mita 30 kutoka kwenye nguzo utatakiwa kusubiri hadi huduma ikusogelee au

Utaandika barua ta kuomba kulipia mwenyewe kwa gharama zako ikiwa unahitaji huduma kwa haraka na upo tayari kugharamia , sasa hiyo barua ndo sijajibiwa mpaka leo napigwa kalenda tu mwezi wapili sasa.. wananizungusha kutoa control namba nikalipe

Gharama zake ni kama 690k ivi.
 
Mimi niko Dar es salaam hapa. Survey walishakuja na hela ilishalipwa. Ni extension ya meter tu na ni hapa hapa mjini. Ni wiki 2 sasa sijaona watu wanakuja kufunga meter. Watanzania tutaendelea siku tukibadilika. Maana TANESCO wafanyakazi hamjatambua kama hii ni biashara mnafanya.
 

Yani unataka kujilipia mwenyewe harafu hawataki kukupa majibu, ukisikia utendaji wa kazi mbovu ndo huu sasa, naomba wakupe majibu fasta iwezekanavyo
 
Yani unataka kujilipia mwenyewe harafu hawataki kukupa majibu, ukisikia utendaji wa kazi mbovu ndo huu sasa, naomba wakupe majibu fasta iwezekanavyo
Ndo ivo mkuu... chaajabu nashuhudia majirani wakishushiwa nguzo tu ambao naamini siku pishana nao sana kwenye maombi
 
naombaa msaada nilituma maombi ya kuvuta umeme tangu mwaka jana mwezi wa 11 na survey akaja akapima vzr ni mahali panaitaji nguzo moja lakini mpaka mwezi wa 5 mwaka huu nikarudishiwa form na survey akasema kwa sasa hakuna nguzo mpaka pale serikali itakapo tangaza tena nimebaki gizani mpaka sasa



location kilimanjaro/ Himo
 
Tafadhali onyesha taarita tulizoomba kwa hatua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeomba kwa jina gani

Namba ya simu

Eneo

Na je ulijibiwa kwa maandishi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo wilaya ya rungwe halmashauri ya busokelo,ni kawaida kukatika umeme kuanzia saa kumi jioni kukiwa na ratiba ya mpira.umem ulikuwepo tangu asubuh mpira umeanza umekatika.nini tatizo?
 
Hizo nguzo za umeme zipo au hazipo maana nimeenda Tanesco ( ) naambiwa nguzo za bure hakuna zipo za kuuza Waziri was nishati tupe jibu Kuna nguzo kwa wateja za bure na za kuuza cash? Happy ndipo napoanza kuichukia serikali mbona nyie watu rushwa itawaua ? ETI nisiende kuwashtaki!!! Sasa nahitaji majibu vinginevyo Dom siyo mbal
 
Ufafanuzi

Mteja hanunui nguzo wala halipii nguzo bali analipia gharama ya kuunganishiwa umeme ambapo ndani yake kuna vifaa kadhaa ikiwemo mita nguzo myara nk na hakuna mteja anayeambiwa au kupewa makadirio kuwa nguzo ni tsh fulani na makadirio yote yanatoka kwa maandishi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuingiziwa umeme umbali wa mita sita toka kwenye nguzo huwa inachukua muda gani
 
@TANESCO naomba mnitatulie tatzo hili sugu..LUKU yangu inakata umeme kila siku usiku kuanzia saa 2 Hadi saa 3 na nusu Kisha unarudi..nimedumu na tatizo hili kwa zaidi ya maika miwili..
Naomba mnisaidie naitwa LEONARD ROBERT..namba ya LUKU 54182960069 nipo buswelu-mwanza namba 0767101328
 

Umewahi kwenda kwenye ofisi zao hapo mwanza?
 
Tanesco ubungo kibangu umeme umekatika tangia asubuhi sijui nini shida. Afu kila mara mnakata sana hili eneo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…