Asante kwa taarifa tunafatilia kwa hatua zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tanesco kuweni wazalendo na nchi yetu nasikitika kusema yanayofanywa na mameneja wa mikoa ni hujuma dhidi ya serkali,nikupoteza/kuharibu mitaji ya wafanya biashara na kufifisha mitaji.

Nakumbuka ilikuwa tarehe 13 June 2020 umeme ulikatika ghafla jengo zima tukatoa taarifa Tanesco kitengo cha dharula wakatuahidi kufika kwa muda mfupi lakini hawakuja siku nzima tukalazimika kutafuta fundi akague jengo zima,fundi akabaini umeme ulikata kwenye mita tukaendelea kuwasumbua Tanesco lakini majibu yalikuwa yakukatisha tamaa baada ya siku nne ndio wakaja wakabaini mita ni mbavu kweli wakasema wanapeleka taarifa kitengo husika lakini mpaka leo ni wiki tatu hatuna umeme wanadai mita hazipo.

Shughli nyingi zimesimama hatuzaliahi chochote tunakula mitaji.

Mimi nimewasiliana na afisa mahusiano mkoa lakini majibu yake niyaleyale nimeomba msaada kwa DC naye kapigwa danadana mpaka kajitoa.

Swali kwenu Tanesco mnakaaje maofisini mnashindwa kutatua kero za wateja wenu? Kila Mwezi tunatumia umeme wa sh,400,000 na sasa hamkuziingiza hamuoni siku kampuni nyingine zikiruhusiwa ninyi mtafunga vilago?

Ni utaratibu upi mliojiwekea mita ya mteja inapopata hitrafu?

Nategemea kapata majibu sahihi na maelekezo ili nichukue hatua.
 
TANESCO nje ya nyumba nnayojenga umeme wa two phase uko mita chache sana. Hata nguzo ya ziada haihitajiki.
Je nikitaka three phase kwa nyumba yangu hii two phase ndio mtakayo i covert mniwekee three phase au mtanivutia nguzo zingine kuuleta wa three phase maana huu nauona uko mbali sana yaani huo wa three phase.
 
Hiv kwann mtu akihama na luku yake anahamia sehem nyingne mnachaj tena as if ndo anavuta tena umeme...y msiskip hzo gharama za line na luku mcharge ya ufundi tuu kufunga pale juu...hvi nyie mna matatZo gan..ngoja tuwachongee kwa mkuu maana ndo boss wenu
 
Hairuhusiwi kuhama na mita ya LUKU kwa kuwa mita ni kifaa cha kumia matumizi ya mteja amnacho ni malo ya TANESCO, mteja analipia gharama ya kuunganishiwa umeme na sio kununua mita hivyo basi wajibu wa mteja unaanzia baada ya mita kurudi ndani ya nyumba yake na ndio maana hata moya ikiharibika tunatengeneza au kibadilisha wenyewe bila gharama zozote kwa mteja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nipo Goba mpakani, ningependa kujua gharama ya kuweka umeme bila kutumia nguzo hata moja kwa sababu nguzo ipo chini ya mita kumi kutoka kwenye nyumba yangu je na inachukua cku ngapi
 
tunashukuru kusogea karibu na wateja wetu
Mimi nipo Goba mpakani, ningependa kujua gharama ya kuweka umeme bila kutumia nguzo hata moja kwa sababu nguzo ipo chini ya mita kumi kutoka kwenye nyumba yangu je na inachukua cku ngapi
 
Mimi nipo Goba mpakani, ningependa kujua gharama ya kuweka umeme bila kutumia nguzo hata moja kwa sababu nguzo ipo chini ya mita kumi kutoka kwenye nyumba yangu je na inachukua cku ngapi
Tafadhali kamilisha wiring njoo chukua fomu tukumipimie na kukupatia gharama halisi huo ndio utaratibu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msaada : Nimewekea mita wiki mbili zilizopita hizi za remote, Baada ya umeme kuisha nimenunua umeme wa sh 5000 lkn kila nikiweka hauingii na wakati mwingine mita inazima kabla ya kumalizia kuingiza token zenyewe. Nini tatizo
Nipo wilaya ya mtwara
 
Msaada : Nimewekea mita wiki mbili zilizopita hizi za remote, Baada ya umeme kuisha nimenunua umeme wa sh 5000 lkn kila nikiweka hauingii na wakati mwingine mita inazima kabla ya kumalizia kuingiza token zenyewe. Nini tatizo
Nipo wilaya ya mtwara
Tafadhali onyesha

Eneo

Simu

Namba ta mita

Tatizo

Kinachokea ukiingiza umeme

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani Tanesco nashukuru sana sana na Mungu awabariki tayari Tanesco Wilaya ya Hanang wamekuja kukagua na tumeshalipia tayari tangu tarehe 3/7/2020 na kupewa stakabadhi na kuingizwa kwenye system za Tanesco.Yaani nimewapenda bure natoa shukrani zangu za dhati kwa Tanesco.Sasa ningeshukuru kama wangeenda kuunganisha umeme kwani haitaji hata nguzo.Natanguliza shukrani zangu tena .
Jina ni Monica Lazaro
Wilaya ya Hanang Meascrow .Asanteni kwa huduma nzuri
 
Asante sana utafungiwaaa umeemme mkuu wetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…