Mimi nimelipia kila kitu tangu mwezi wa 6 tar 15 hamjaleta nguzo wala chochote kwa nini TANESCO?
 
Tanesco fanyeni mpango tuwe na uwezo wa kuhama na metre tulizolipia kwa maana tunalipia kwenye majengo ya watu mnalijua hilo ila tukitaka kuondoka na hizo metre tukaendelee kutumia mnakataa ni gharama kubwa kwenda tena kuanza process za kuomba umeme wakati ulikuwa na metre uliyokuwa chini yako kwa jengo la mtu mwingine
 
Ndugu mkuu wetu

*ELIMIKA NA TANESCO*

Je mteja anaweza kuhama na mita kutoka eneo moja kwenda lingine?

*Jibu la TANESCO*

[emoji3578]Mita ni kifaa kinachotumika kupima matumizi ya mteja

[emoji3578] Mteja halipii wala kununua mita bali analipia gharama halisi ya kufungiwa umeme (Service line connection fee)

[emoji3578]Mita inaendelea kuwa mali ya TANESCO wakati wote mteja anaotumia umeme

[emoji3578]Mita ya umeme ikiharibika au kupata hitilafu yeyote ambazo haitokani na uzembe au matumizi mabaya ya mteja TANESCO inabadilisha mita hiyo kwa gharama zake kwa kuwa ni kifaa chake

[emoji3578] Wajibu wa mteja wa TANESCO unaanzia baada ya mita kurudi ndani ndio maana mteja au fundi ( mkandarasi) haruhusiwi kufanya ukarabati wowote wa mita ya TANESCO

[emoji3578] Mita ya umeme ikishafungwa haiwezi kuhamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine isipokuwa ndani ya ploti husika na inafanywa na TANESCO kupitia maombi kwa maandishi ya mteja

[emoji3578] Unapoona hitilafu yeyote kwenye mita au kifaa chochote cha umeme kuanzia kwenye mita kwenda nje toa taarifa TANESCO mara moja na sisi tutaifanyia kazi bila gharama yeyote.

*Toa taarifa kupitia* [emoji116]

[emoji3578] TANESCO APP

[emoji3578]Facebook/twitter/tanesco yetu

[emoji3578]Instagram:tanesco_official page

[emoji3578]Tovuti: www.tanesco.co.tz

[emoji3578] Barua pepe: Customer.service@tanesco.co.tz

[emoji3578] Huduma kwa wateja
0768 985 100/ 022 219 4400

*TANESCO* Tunayaangaza Maisha yako
 
Maombi yangu yako hivi mm nafanya biashara inapotokea niliunganishwa umeme kwenye jengo A na mkataba ukaisha ninaenda kufanya biashara zangu jengo B niweze kuondoka na hiyo metre maana mimi ndie niliyelipia garama za kuwepo kwa huduma ya umeme mahali pale na kwa kuwa nighara sana kuanza upya kutuma maombi mapya pawepo na ghara nafuu za nyinyi tanesco kuihamisha hiyo metre
 
Tafadhali pitia tena maelezo yetu
 
Tayari washakata umeme sahizi ni giza tupu

Sijui tatizo ninini

Vipi tujuzane maeneo uliyopo hapa Dar kuna umeme? Au ni huku ubungo tu?
 
Mita yangu unasoma hivyo lakini umeme hakuna hapo nimewasha Genereta ndiyo imesoma hivyo ,nikizima Genereta hakuna umeme
 
Mkuu hadi kibamba hakuna Umeme,na Leo umekatika three times,,,na hatupewi sababu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…