Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndugu mkuu wetuTanesco fanyeni mpango tuwe na uwezo wa kuhama na metre tulizolipia kwa maana tunalipia kwenye majengo ya watu mnalijua hilo ila tukitaka kuondoka na hizo metre tukaendelee kutumia mnakataa ni gharama kubwa kwenda tena kuanza process za kuomba umeme wakati ulikuwa na metre uliyokuwa chini yako kwa jengo la mtu mwingine
Maombi yangu yako hivi mm nafanya biashara inapotokea niliunganishwa umeme kwenye jengo A na mkataba ukaisha ninaenda kufanya biashara zangu jengo B niweze kuondoka na hiyo metre maana mimi ndie niliyelipia garama za kuwepo kwa huduma ya umeme mahali pale na kwa kuwa nighara sana kuanza upya kutuma maombi mapya pawepo na ghara nafuu za nyinyi tanesco kuihamisha hiyo metreNdugu mkuu wetu
*ELIMIKA NA TANESCO*
Je mteja anaweza kuhama na mita kutoka eneo moja kwenda lingine?
*Jibu la TANESCO*
[emoji3578]Mita ni kifaa kinachotumika kupima matumizi ya mteja
[emoji3578] Mteja halipii wala kununua mita bali analipia gharama halisi ya kufungiwa umeme (Service line connection fee)
[emoji3578]Mita inaendelea kuwa mali ya TANESCO wakati wote mteja anaotumia umeme
[emoji3578]Mita ya umeme ikiharibika au kupata hitilafu yeyote ambazo haitokani na uzembe au matumizi mabaya ya mteja TANESCO inabadilisha mita hiyo kwa gharama zake kwa kuwa ni kifaa chake
[emoji3578] Wajibu wa mteja wa TANESCO unaanzia baada ya mita kurudi ndani ndio maana mteja au fundi ( mkandarasi) haruhusiwi kufanya ukarabati wowote wa mita ya TANESCO
[emoji3578] Mita ya umeme ikishafungwa haiwezi kuhamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine isipokuwa ndani ya ploti husika na inafanywa na TANESCO kupitia maombi kwa maandishi ya mteja
[emoji3578] Unapoona hitilafu yeyote kwenye mita au kifaa chochote cha umeme kuanzia kwenye mita kwenda nje toa taarifa TANESCO mara moja na sisi tutaifanyia kazi bila gharama yeyote.
*Toa taarifa kupitia* [emoji116]
[emoji3578] TANESCO APP
[emoji3578]Facebook/twitter/tanesco yetu
[emoji3578]Instagram:tanesco_official page
[emoji3578]Tovuti: www.tanesco.co.tz
[emoji3578] Barua pepe: Customer.service@tanesco.co.tz
[emoji3578] Huduma kwa wateja
0768 985 100/ 022 219 4400
*TANESCO* Tunayaangaza Maisha yako
Tafadhali pitia tena maelezo yetuMaombi yangu yako hivi mm nafanya biashara inapotokea niliunganishwa umeme kwenye jengo A na mkataba ukaisha ninaenda kufanya biashara zangu jengo B niweze kuondoka na hiyo metre maana mimi ndie niliyelipia garama za kuwepo kwa huduma ya umeme mahali pale na kwa kuwa nighara sana kuanza upya kutuma maombi mapya pawepo na ghara nafuu za nyinyi tanesco kuihamisha hiyo metre
Huku kwetu pia. Jana wamekata kuanzia saa nane mchana mpaka saa nne usiku.
Hata mbezi hakuna umeme
Sent
Mkuu hadi kibamba hakuna Umeme,na Leo umekatika three times,,,na hatupewi sababu
ttcl bana.inamaana kaka yake tanesko asipokuwepo na yeye anasusa[emoji23]Umeme ukikatika na internet ya ttcl inapotea
Poleni huku kwetu upo 24/7