*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*

*TAARIFA YA KATIZO LA UMEME MTWARA*

*07/08/2020*

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake wa Mkoa wa Mtwara kuwa, kutakuwa na katizo la umeme siku ya Jumapili Agosti 09, 2020 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri.

*Sababu:-* Kuruhusu TPDC kuunga mtambo wa gesi kwa watumiaji wa majumbani.

*Maeneo yatakayoathirika:-* Mkoa wa Mtwara, Wilaya ya Tandahimba, na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Lindi yanayopata huduma ya umeme kutokea Mtwara.

Tunaomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza

Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au ulioanguka chini, toa taarifa Ofisi za TANESCO zilizo karibu.

Wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: - Kitengo cha Miito ya Simu 0222194400 na 0768 985100

*Tovuti:*
www.tanesco.co.tz

*Mitandao ya kijamii:*

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd

Imetolewa na:-
Otisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
 
Nililipia umeme Kigamboni mwezi wa sita tarehe 18 mwaka huu, nililipia nguzo moja. Lini mipango ya kuweka umeme? Kuna maneno kuwa nguzo zimeisha sasa inakuwaje?
 
Nililipia umeme Kigamboni mwezi wa sita tarehe 18 mwaka huu, nililipia nguzo moja. Lini mipango ya kuweka umeme? Kuna maneno kuwa nguzo zimeisha sasa inakuwaje?
Tutakufikia usambazaji wa nguzo unaendelea
 
Sasa nyie tanesco hivi kweli huku VIWEGE hawa mafundi hawafungi nyaya mpaka tuwalishe.. kwamba tuchange pesa eneo zima tujitolee kina mama tupike wao wale?
Kwamba tusipofanya hivyo kwetu hawatapitisha nyaya na wanasema eti hatuna ushirikiano.. hivi huo ni ushirikiano au rushwa.?? Nimeshangaa narudi mizungukoni naambiwa nitoe elfu mbili ya chakula kwa ajili ya mafundi wanaofunga nyaya..

Na ndicho walichokifanya kule mbele kabisa umeme umepita kwenda nyuma wa mbele na wakati hakuna waya wala umeme yani mwenye hela ndio anafungiwa watu wameuliza mbona hapa mumeweka nguzo na hamfungi nyaya wanajibu kwamba zimwagilieni maji ile ziote! Hivi huu ni uungwana.. mnagawa umeme kwa mafungu kwa kigezo cha pesa .. yani mwenye hela ndiye anayehudumia[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848] ..

Bado tupo nyuma sana .. najua hlutajibu maana nyie ndio walewale
 
Tunasisitiza kuwa hakuna malipo yeyote yanayoruhusiwa kufanywa na mteja kwemda kwa mfanyakazi au kampuni iliyopewa kazi na TANESCO, tafadhali tusaidie namba yako ya simu na jina la aliyekutaka kuchangia hilo
 
We Wekeni na namba ya mkurugenzi mkuu wa tanesco hapa, ili apigiwe.mfano mikoa ya Kanda ya ziwa Kuna miradi mipya ya umeme inahitajika aipitishe ili miradi ufanyike kabla ya uchaguzi mkuu Hadi Sasa hajapitishwa wekeni namba tumpigie.Huku tunashindwa kufanya kampeni kisa ahadi ya Mh Rais kuhusu wananchi kupata nishati ya umeme haijatimizwa.
 
Miradi gani tafadhali iorodheshe
 
Mmepeleka utaratibu wa ajira kupitia utumishi mmetuletea shida kubwa cjui kama mnajua hili
 
Miradi gani tafadhali iorodheshe
Ina maana Tanesco haina miradi mipya ya kusambaa umeme mikoa ya Kanda ya ziwa? Unataka iorodheshe ? Kama haipo semeni haipo ili tuwatangazie wananchi kuwa hakuna miradi mipya ya umeme bakini gizani.Kama ipo wekeni orodha hapa ili wananchi waweze kuiona na kufahamu ili wajiandae kuipokea. Tanesco punguzeni maswali chapeni kazi.
 
Onyesha namba yako ya simu tukupigie maana lalamiko lako lipo kwa ujumla kanda nzima
 
Samahani TANESCO, inachukua mda gani kutumiwa namba ya malipo(control number)?! Manake Tangu June nimejaza form na mkandarasi alishachora mchoro. Nipo Mabalanga wilaya ya Kilindi mkoani Tanga. simu 0621149433
 
Samahani TANESCO, inachukua mda gani kutumiwa namba ya malipo(control number)?! Manake Tangu June nimejaza form na mkandarasi alishachora mchoro. Nipo Mabalanga wilaya ya Kilindi mkoani Tanga. simu 0621149433
Tunashukuru kwa taarifa tunaifanyia kazi
 
Habari TANESCO .
Naomba kuuliza endapo mita ya Luku haifanyi kazi inachukua muda gani kubadilishiwa baada ya maombi kuwasilishwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…