Je umewahi kifika ofisini kuulizia?
 
Je ulipatiwa gharama za kulipia? Ushauri wetu ni kwamba kwa mteja aliyembali na miundimbinu anashauriwa kusubiri imfikie tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Simu
 
Gharama sijapatiwa naitwa Oscar Mkandya John nipo Wilaya ya Buchosa Mwanza simu 0768145634
Swala la kufikiwa miundo mbinu huwa linachukua muda gani jamani ikiwa tu hadi sasa ni miezi nane sijahudumiwa ?
 
Gharama za kufunga umeme kwa mji wa NJOMBE ni shilingi 27000 au bei ni tofauti na hiyo?
 
KAMA KAWAIDA YENU TANESCO KILA JTATU NA JUMANNE UBUNGO BUSSINESS PARK HAMNA UMEME,MMESHAKATA HILI TATIZO LITAKWISHA LINI?MBONA NYIE NI SIKIO LA KUFA,NAMNA HII KWA ENEO LENYE MATUMIZI MAKUBWA KAMA HILI MNAPOTEZA MAPATO NA MNATUTIA SISI HASARA. SIJUI MTABADILIKA LINI NYIE
 
*SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)*

*KATIZO LA UMEME MKOA WA KINONDONI KUSINI*

Shirika la Umeme Tanzania *TANESCO* Mkoa wa Kinondoni Kusini linaomba kuwataarifu wateja wake kuwa kutakuwa na katizo la umeme kama ifuatavyo.

*Siku* Jumanne 01-09-2020

*Muda* Saa 03:00 asubui hadi SAA 09:00 Alasiri

*SABABU*
Kuhamisha line ili kupisha ujenzi wa barabara ya Shekilango.

*MAENEO YATAKAYOATHIRIKA*
Tandale Yote, Sinza yote, Mburahati, baadhi ya maeneo ya Manzese, NBC Ubungo Shekilango, Ubungo Terminal, TBS, Magomeni, Kigogo na maeneo ya Urafiki.

*Tunaomba radhi sana kwa usumbufu utakao jitokeza*

*Tahadhari*
Usikanyage wala kugusa waya uliokatika au kulala chini.

Wasiliana nasi kwa simu na.zifuatazo: Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kusini: 0715271461/0784271461

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz,

Mitandao ya kijamii

Twitter, www.twitter.com/tanescoyetu,

Facebook https://www.facebook.com/tanescoyetultd/

Imetolewa na:
*OFISI YA UHUSIANO NA HUDUMA KWA WATEJA- KINONDONI KUSINI*
31-08-2020
 
Mimi nipo Arusha.... mradi wa umeme wa REA umepita ktk mtaa wetu na baadhi ya watu wameshafungiwa ila wengine bado! leo tunapata ujumbe wa sms kujulishwa kulipia gharama za umeme lakini ajabu gharama ni sh 177,000! je; za nini wakati umeme wa rea tunaambiwa ni sh 27,000????
 
Tafadhali fika ofisi ya eneo lako kwa maelezo ya kina dhidi ya eneo husika
 
Hakuna shaka yoyote zipo juhudi zinachukuliwa na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), katika kusambaza Umeme maeneo mbalimbali nchini. Umeme umesambazwa katika vijiji mbalimbali, kwa mujibu wa Takwimu zinazotamkwa na Viongozi walioko Serikalini ni kuwa zaidi ya Vijiji 10,000 vimefikiwa na umeme na vimesalia Vijiji 2000+ kufikiwa na Umeme, ambapo vijiji vyote vitakua vimefikiwa na nishati ya umeme.

Huduma ya upatikanaji wa Nishati ya Umeme inazidi kwenda vijiji mbalilimbali ili hali Ofisi za Tanesco zinaendelea kubaki zile zile, Uongezaji wa Vijiji Unapaswa kwenda Sambamba na Ujenzi wa Ofisi Kila Tarafa ama Kata, Kutokufanya hivyo kutasababisha usumbufu kwa baadhi ya vijiji pindi itokeapo changamoto

TANESCO mnaposambaza Umeme Vijijini iende sambamba na Ujenzi wa Ofisi za Kanda na Ofisi ndogo

Cc
TANESCO
 
Maeneno ya Makumbusho, Kijitonyama, Kinondoni, Mikocheni hatuna umeme toka jana usiku. Shida ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…