lufungulo k
JF-Expert Member
- Apr 19, 2012
- 2,601
- 2,058
Naishi Mbagala charambe - kwa Mwarabu maeneo ya jirani na Msikiti eneo letu toka asubuhi ya leo HATUNA UMEME nyumba kadhaa huku wengine wakiwa na umeme tatizo ni nn?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kama upo ndani ya mita 30 utafungiwa umeme ndani ya siku 30 za kaziNimefuatilia control number kwa miezi minne, mwezi wa nane mwishoni nikafanikiwa kulipia lakini yapata wiki mbili sasa naona kimya ,sijapata huduma . Naomba kujua inaweza kuchukua muda gani adi kuhudumiwa mteja yuko umbali wa zaidi ya mita 30.
Duuuh, 90 days ni bora nisingelipiaKama upo ndani ya mita 30 utafungiwa umeme ndani ya siku 30 za kazi
Mita zaidi ya 30 hadi 100 ndani ya siku 90 za kazi
Zaidi ya mita 100 au upanuzi wa mradi unahitajika ndani ya siku 90 za kazi
Nashukuru tatizo lilitatuliwa , isipokuwa Jana 8/09/2020 kulikuwa na ukosefu wa umeme bila taarifa toka saa 1900- 0000Tunashukuru kwa taarifa tafadhali onyesha namba ya simu
Kwahyo nikienda offisini kufuatilia naweza kupata huduma mapema??Haina maana kuwa lazima usubiri siku hizo bali inategemea na sababu nyingine ndio maana tunasema ndani ya muda huo
ndugu TANESCO nimekuelewa ila sisi wengine ukituona humu ujue tunazungumzia matatizo ya eneo kubwa baada ya kujiridhisha kuwa ni eneo lote ntalozungumzia limeathirika.Tunapenda kupata mawasiliano ya mteja ili kumpigia na kumsikiliza zaidi kwani tatizo la Ubungo sio lazima liwe la Kimara tunakuletea elimu ya kwanini tunaomba taarifa kamilo hivi punde
Tatizo la Kimara na maeneo ya jirani linafanyiwa kazi kwa kujenga kituo kikubwa cha kupooza umeme ili kuikarisha hali ya upatikanaji wa umeme.Tumekuwa tukitoa taarifa za maeneo hayo mara zote tunapopata hitilafu tafadhali onyesha namba yako yenye WhatsApp tukuunge kwenye eneo la taarifa zaidindugu TANESCO nimekuelewa ila sisi wengine ukituona humu ujue tunazungumzia matatizo ya eneo kubwa baada ya kujiridhisha kuwa ni eneo lote ntalozungumzia limeathirika.
Hivi hapa nnavyokuambia Kimara mwisho yote ina matatizo ya kukatika umeme mara kwa mara.Kimara mwisho nnayozungumzia mimi ni hii ya upande wa Dawasco,Matangini,hospitali ya Kimara,kanisa katoliki,TRA,Sokoni hadi Machinjioni.Lakini nnapofuatilia nagundua umeme huu unakuwa umekatika njia yote ya line yetu hadi Ubungo,so umeme unakatiwa kwenye chanzo huko kwenu kwa sababu wanazojua wakataji.Ila hatuna taarifa na tunaona siku zinavyozidi kwenda huu ukataji unashika kasi.Unakuta umeme unakatwa nusu saa unarudi,baada ya masaa kadhaa unakatwa tena nusu saa au saa unarudi.Kwa sisi wenye matumizi makubwa ya umeme ni kadhia kubwa.Jana mlitaka kuniharibia mota ya mashine yangu,sababu ya huu ukatikaji umeme wa aina hii.Lakini why?kwanini watu wa Kimara wasipate umeme vizuri kama kwingine Dar?ni miundombinu au nini?
Hivi nnavyoandika hakuna umeme kule.hii saa nne na dk 7 asubuhi,laini hiyo yote inayolisha eneo nililosema hakuna umeme now.
nipo Kimara tangu 2006 na sijawahi kuona umeme ukiwa stable na majibu ya aina hii ndio tunapewa kila tukipiga simu kwenye namba zenu.Tatizo la Kimara na maeneo ya jirani linafanyiwa kazi kwa kujenga kituo kikubwa cha kupooza umeme ili kuikarisha hali ya upatikanaji wa umeme.Tumekuwa tukitoa taarifa za maeneo hayo mara zote tunapopata hitilafu tafadhali onyesha namba yako yenye WhatsApp tukuunge kwenye eneo la taarifa zaidi
Tunakuelewa mpendwa mteja wetu ndio maana zipo hatua kadhaa zilizochukuliwa kuendelea kuboresha upatinaji w umeme eneo husika.Sisi hatukati umeme wala kupenda umeme ukatikanipo Kimara tangu 2006 na sijawahi kuona umeme ukiwa stable na majibu ya aina hii ndio tunapewa kila tukipiga simu kwenye namba zenu.
TANESCO unataka kutufanya wateja wenu malaika nadhani.Tangu asubuhi mpaka sasa hakuna umeme,na ndio utaratibu uliopo kukatiwa umeme si chini ya siku nne kwa wiki,halafu kila ukiuliza unaambiwa ni hitilafu,mafundi wanahangaikia,huduma zitarudi..since 2006!now you are telling me sijui nisubiri kituo kipya..we mpaka ujenge hicho kituo mimi biashara zangu zinasubiri tu?so what you are saying ntaendelea kupata huduma ya umeme isiyo na uhakika mpaka kituo kipya hicho kikamilike?hiyo project inakamilika lini?leo jioni?kesho?...hivi we ungekuwa mimi ungeliona hili ni jibu rahisi kwa mteja anayekulipa stahiki zako everyday lakini hapati huduma yako?you take it simple isnt it?...ngoja nijiondokee naona unanitia hasira zaidi.!
Nafasi zote za kazi zinatangazwa na Utumishi kupitia Ajira Portal hivyo tafadhali wasilisha swala lako sehemu husikaTanesco nashindwa kuwaelewa nafasi za kazi zinatangzwa tegeta,kinyerezi na somanga halafu usahili mmapeleka mwanza [emoji849]
Mantiki yenu ni nini,mnatuumiza kiuchumi hatupo poa wenzenu benchi lishatumaliza
Nafasi zinazokusudiwa kujazwa ni za Kanda ya Ziwa (Ofisi ya Kanda, Mikoa, Wilaya na Ofisi Ndogo). Walengwa wakubwa ni wananchi wenye sifa wa maeneo hayo kwa sababu kazi hizo ni za muda mfupi (miezi 12).Tanesco nashindwa kuwaelewa nafasi za kazi zinatangzwa tegeta,kinyerezi na somanga halafu usahili mmapeleka mwanza [emoji849]
Mantiki yenu ni nini,mnatuumiza kiuchumi hatupo poa wenzenu benchi lishatumaliza
Je umelipia kwa jina ganiNimelipia kuunganishwa kupata huduma ya umeme kwenye nyumba yangu tokea 10.07.2020 katika tawi la gongo la mboto lakini mpaka leo hii sijaunganishiwa na nipo ndani ya Mita 30 tokea nguzo ilipo kwenye form ya kulipia imeandikwa ndani ya siku 30 za kazi nini tatizo?