Tanesco mlininyima umeme yaani sina LA kuwafanya lakini moyo wangu umejaa simanzi kubwa sana, mnaubaguzi, baadhi ya maeneo mnawapa umeme wengine mnatunyima. Hii nchi yetu sote ila sawa tu ngoja twendelee kutumia vibatari tu na solar
 
kaka hadi huku temeke pia hakuna umeme kazi ni hyo tu
 
TANESCO, Dodoma kuna maeneo ya Mpamaa sio mbali na mjini, vpi mna mpango wa kupeleka umeme lini huko?maana ni maeneo yaliyopo within 13km kutoka ofisi zenu kuu. Inashangaza Dodoma mjini baazi ya maeneo hayana umeme..na eti ni capital city..
 
Maeneo yote yatapata huduma ya umeme kwenye awamu mbalimbali za usambazaji wa umeme mijini, vijijini na maeneo ya pembezoni mwa miji.Tumepokea taarifa yako pia kwa ufatiliaji na hatua zaidi
 
Kulikoni umeme umekuwa unakatika kila saa kwa maeneo mengi ya Dar?

Mfano huku Mbezi, Kimara na baadhi ya maeneo kule Ubungo umeme unakatika hovyo hovyo tu.
 
Huduma imeimarika hivi sasa
Kwa akili zenu za ajabu mnadhani mnadanganya umma mpaka lini Bonyokwa hii line ya stopova na Vertasi shule ni kero sana muda huu saa Nne mmekata umeme tena. Lazima kuna hujuma ama ni mpango wenu ovu wa kujipatia per diem.
 
Taafadhali onyesha namba yako ya simu kwa hatua zaidi
 
Maeneo yote yatapata huduma ya umeme kwenye awamu mbalimbali za usambazaji wa umeme mijini, vijijini na maeneo ya pembezoni mwa miji.Tumepokea taarifa yako pia kwa ufatiliaji na hatua zaidi
TANESCO, asante kwa kujibu haraka..ila jibu lipo too general..anyway.ningependa kujua maybe lin umeme utakua umefka eneo nililolitaja hapo juu..given the fact kwamba still lipo mjini..
 
Na namba zao za huduma kwa wateja ukipiga iko busy muda wote, uking'ang'ania kupiga mara nyingi ukapata line, inaiiita mpaka inakata, ukijaribu tena hapo hapo, iko busy. Na mbaya zaidi wanaweka customer care wasiojua chochote kuhusu umeme, nu telephone operators, wanajua kusema MAFUNDI WAKO/WATAFIKA ENEO LA TUKIO KUSHUGHULIKIA, tumeshawataarifu, utapigiwa simu. Ukiwauliza nini shida na tutegemee baada ya muda gani, utapigiwa simu.

Ni hivi waTZ wenzangu,jambo linalowashinda Tanesco na serikali yao, sisi mmoja mmoja tunaweza kufanya kwa kujibana. Tujiwekee plan za miaka hata 2, nunua solar system kidogo kidogo, Panel 2 X 300W, hii inaweza kuchukua hata miezi 6 kwa mwenye uchumi wa kati ya kati, inverter ya Watts 500 inatosha kwa miezi 6 iliyobaki kwenye mwaka wa kwanza. 6 ya wa pili unatafuta 200Ah betri moja na 6 ya mwisho vikolokolo vilivyobaki.

Taa zote za nje na sehemu muhimu ndani, sebule, jiko, choo na socket 2 unaziunga kwenye solar, Tanesco tunawaachia Friji na pasi na kwa wale wa uchumi wa juu ya kati, AC na heater mnawaachia wao. Jua tunalo la kutosha, tuachane na hawa wanyanyasaji. Tujifunze kuvuna huu umeme jua kwa fujo haswaaa, ulaya huko wameingiza umeme wa jua, upepo, jotoardhi kwenye grid kwa kiwango kikubwa, sasa sisi tuingize majumbani mwetu,uzuri tunaruhusiwa, mpaka huyu mkoloni akiona anazidiwa sio leo, atakuja na katazo au kutulipisha pesa za kutosha ukitaka kuzalisha umeme kwa matumizi yako binafsi.

Baada ya miezi 6 ya matumizi madogo, tuunza kuomba tariff ya kununua unit 75 kwa tzs 10,000 kwa mwezi.

Ndo suluhu la umeme kutokatika katika nyumbani kwako.
 
Hapa tu nipo gizani wamekata saa 1 lishapita. Wilaya ya Ubungo hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…