Na namba zao za huduma kwa wateja ukipiga iko busy muda wote, uking'ang'ania kupiga mara nyingi ukapata line, inaiiita mpaka inakata, ukijaribu tena hapo hapo, iko busy. Na mbaya zaidi wanaweka customer care wasiojua chochote kuhusu umeme, nu telephone operators, wanajua kusema MAFUNDI WAKO/WATAFIKA ENEO LA TUKIO KUSHUGHULIKIA, tumeshawataarifu, utapigiwa simu. Ukiwauliza nini shida na tutegemee baada ya muda gani, utapigiwa simu.
Ni hivi waTZ wenzangu,jambo linalowashinda Tanesco na serikali yao, sisi mmoja mmoja tunaweza kufanya kwa kujibana. Tujiwekee plan za miaka hata 2, nunua solar system kidogo kidogo, Panel 2 X 300W, hii inaweza kuchukua hata miezi 6 kwa mwenye uchumi wa kati ya kati, inverter ya Watts 500 inatosha kwa miezi 6 iliyobaki kwenye mwaka wa kwanza. 6 ya wa pili unatafuta 200Ah betri moja na 6 ya mwisho vikolokolo vilivyobaki.
Taa zote za nje na sehemu muhimu ndani, sebule, jiko, choo na socket 2 unaziunga kwenye solar, Tanesco tunawaachia Friji na pasi na kwa wale wa uchumi wa juu ya kati, AC na heater mnawaachia wao. Jua tunalo la kutosha, tuachane na hawa wanyanyasaji. Tujifunze kuvuna huu umeme jua kwa fujo haswaaa, ulaya huko wameingiza umeme wa jua, upepo, jotoardhi kwenye grid kwa kiwango kikubwa, sasa sisi tuingize majumbani mwetu,uzuri tunaruhusiwa, mpaka huyu mkoloni akiona anazidiwa sio leo, atakuja na katazo au kutulipisha pesa za kutosha ukitaka kuzalisha umeme kwa matumizi yako binafsi.
Baada ya miezi 6 ya matumizi madogo, tuunza kuomba tariff ya kununua unit 75 kwa tzs 10,000 kwa mwezi.
Ndo suluhu la umeme kutokatika katika nyumbani kwako.