Tafadhali onyesha namba ya taarifa na namba ya simu kwa hatua zaidi
mrejesho wa taarifa hii niliyoitoa usiku wa jana.
leo asubuhi mafundi walikuja, ila wamedai kua ni hitilafu kidogo iliyojitokeza katika matumizi yangu binafsi ya umeme wa hapa nyumbani, hivyo kesho asubuhi nitatumiwa namba ambazo nitaziingiza katika hiki ki remote.
ni hayo tu hivyo bado napambana na giza langu.
 
Wateja wote wa REA wanapewa unit 10 za mkopo wakinunua zitakatwa,upo kundi la matumizi ya nyumbani
 

Habari za wakati huu ndugu zangu.
Heri ya mwaka mpya.

Napenda kuipongeza shirika la umeme Tanzania kwa kunifikia kwa awamu ya kwanza.

Baada ya kuandika ujumbe huu juzi jumamosi nilitembelewa na wahusika nyumbani kwangu nashukuru wamejionea Changamoto tunayoipata na uhitaji tulio nao.

Mafundi (surveyors) walifika eneo husika tukajadili kuhusu shida yetu na wakachukua majina ya wahusika eneo hilo Bahati nzuri tulishajaza forms za maombi ya umeme na kuloji Tanesco mkuranga hivyo nikawafahamisha tayari hiyo stage tulishaivuka.

Baada ya majadiliano wahusika wakaniambia leo juma Tatu (siku ya kazi ) nitapigiwa simu kujua kinachoendelea na kitakachojiri,
Hadi muda huu sijapigiwa bado simu na siku tumeshaigawa,
tafadhalini tunaomba mrejesho.

narudi tena hapa kuomba speed mliyoianza imalizieni najua mmetingwa wahitaji ni wengi ila tunaomba mtusaidie, eneo husika tukipata nguzo kadhaa tu zitatosha tutapitishiana waya hata juu ya nyuma zetu ili tupate sote umeme.

Asanteni.

Johnson Mgaya
0768900531
 
Ahsante kwa ukumbusho
 
Nadhani kama shirika mnapaswa kuyafanyia kazi malalamiko mengi yanayotolewa na wateja juu ya Tawi lenu la Kibaha. Nikiwa kama mmoja wa waombaji wa kuunganisha huduma, katika eneo la Kongowe Kati, wilaya ya Kibaha, tokea mwezi 10, 2020 mpaka leo hii tarehe 5 Jan, 2021 sina matarajio ya kupata huduma hiyo kwa weredi wa kawaida. Matatizo ya msingi yapo kwenye Survior na kupata Control namba ili uweze kulipia. Hembu tuwekeni wazi kuwa hizi ndizo policy za shirika kwamba mteja lazima asumbuke kupata huduma, au mnakiri kuwa mnao watendaji ambao hawana weredi na mnashindwa kuwawajibisha?
 
BADO Sana mkuu [emoji28] nimepata Huduma ya umeme baada ya miezi 9 Kama Mimba[emoji28] tena kwa mbinde. Nilisaidiwa na makao makuu kupata control number bila hivyo ningekuwa nahangaishwa na Wilayani Hadi leo
 
Tanesco mnasemaje hili suala la Kunguru kusababisha mkatiko wa umeme Dar? Halafu mbona umeme unakatika sana usiku wakati kunguru wakiwa wamejichimbia kwenye malalo yao? Naomba mtufafanulie zaidi ni kwanamna gani kunguru wanakula nyaya za umeme na kusababisha mgao/ kukatika umeme Kinondoni.
 
Tafadhali onyesha namba ya simu
 
Kuna wakati tu naambiwa unapoomba umeme nguzo hazilipiwi, lakini huku Gongolamboto Daressalaam hakuna kitu kama hicho! Tunalipishwa tu!

Naomba ufafanuzi, hii habari ni kweli kwamba nguzo hazilipiwi au ikoje!?

Nyumbani kwangu ili niunganishwe umeme nimeambiwa panahitajika nguzo tatu!!
 
Mteja analipia gharama ya kuunganishiwa umeme na sio vifaa
 
Mteja analipia gharama ya kuunganishiwa umeme na sio vifaa
Kuna muda nimeona malalamiko kwamba unajibu kihuni au kama robot! Hakuna 'kastama kea' hapa! Ikiwa unachoka maswali kausha usijibu!!

Inajulikana kwamba mteja analipia gharama ya kuunganishiwa umeme na sio vifaa, sawa! Lakini vifaa hivyo vinapojumuisha nguzo iwe moja au zaidi hupelekea gharama kuwa kubwa sana kuliko mteja asiyehitaji nguzo kufungiwa umeme!

Je tunagharamia nguzo ama la!
Nikihitaji kuunganishiwa umeme bila nguzo kutumika Huku Gongo la mboto nalipia 321,000Tsh ikihitajika nguzo moja nalipia 500k+ ikihitajika nguzo zaidi ya moja bei huogezeka maradufu!!

Huwezi kulitolea hili ufafanuzi kausha na usijibu kama wewe ni Polisi!!
 
Tunaendelea kukuelimisha kuwa mteja analipia gharama ya kuunganishiwa umeme na sio vifaa.Gharama hizi zinatofautiana kati ya mijini na vijijini ambapo vijijini wateja wanalipa 27000 tu mijini gharama inategemea na sababu nyingi ambazo zibaonyeshwa kwenye barua ya makadirio
 
Baada ya msoto wa muda mrefu hatimae wamenifungia umeme ila sasa msoto umehamia kwenye kusajili meter number.. ni wiki sasa inakatika kila nikienda wananiambia nunua kesho ila holaaa..

Naweza pata msaada upi hapo.. na inasemekana umeme ukiisha meter itajiblock sina uhakika kama ni Kweli.. hem naombeni muongozo hapo
 
Tafadhali onyesha namba ya simu,namba ya mit na wilaya husika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…