Mimi ni Mkazi wa eneo la mwembe mtengu mkokozi maeneo ya kanisa la kkkt,
Napenda kutoa dukuduku langu leo maana tumeshakaa na kuvumilia muda mrefu sasa bila jawabu kutoka kwa wahusika,
Eneo tuliopo ni muda sasa hakuna nishati ya umeme, licha ya wenzetu waliotuzunguka pande zote nne wanawekewa umeme na hadi hivi sasa naandika hapa wameshawashia hapo juzi, lakini sisi hakuna hata procedure zinazoendelea,
Miezi mitatu iliyopita tulipeleka maombi ya kuhudumiwa Tanesco ya mkuranga, walituahidi mwezi unaoanza (September) wangekuja kufanya survey wajue nguzo ngapi zinatosha kutokea umeme ulipokomea, licha ya kuwajibu kuwa kuna nguzo mbili tu kutoka umeme ulipo na Nyumba ya kwanza kwenye eneo letu, na hadi umeme ufikie Nyumba zote zilizoeneo letu (jumla nyumba 20 tu) ni nguzo saba 7 pekee kuanzia na Zile mbili za njiani.
Hadi hivi leo ninavyoongea hakuna kilichofanyika tumeshafanya juhudi za kurudi kufatilia atleast wangekuja tu kutupa tu nguzo chini kungekuwa na ahueni Kuna jambo limetendeka,
Hili eneo jeografia yake sio nzuri, ni mwisho wa eneo hili la mkokozi tumezungukwa na bonde hivyo inapelekea hakuna eneo la makazi tena ukitoka kwetu , wezi na vibaka wanachukua advantage hiyo kutoka kwenye mabonde huko kuja huku kwetu kufanya uhalifu kwa sababu hakuna umeme ni giza totoro ikifika saa moja tu,
Hata ukichukua boda boda usiku hakufikishi hadi kwako kwakuhofia usalama wake anakuachia hapo kkkt kanisani palipo na umeme,
Tunaomba mtusaidie tuna jitahidi kujenga kupendezesha mji na kuleta maendeleo lakini serikali yetu inatukwamisha.
Namba zangu ni
0768900531
Johnson Mgaya.
Mkazi wa mwembe mtengu, mkokozi , kkkt kwa diwani.