Kwa taarifa za majirani inaonekana mteja hayupo eneo hilo mwezi sasa hivyo tunaba utusaidie taarifa kamili au wewe utusaidie namba yako ya simu

Tupo kukuhudumia
Kiongozi mimi nimemsaidia tu huyo mama.

Nimemuonea huruma mtu mzima na hajui mambo ya mitandao.

Na nimemkuta analalamika kwamba hajui cha kufanya.

Nimetoa msaada tu kwake.

Nyie kama TANESCO mtafuteni namba nimewapa.

Namba zangu za simu hata nikikupa hazitosaidia sababu sipo tena huko Bagamoyo nishaondoka.

Fanyeni njia mjuayo mumpate mteja wenu.
Namba ya simu nimewapa PM.

Jaribuni kumpigia tena au hata kutuma ujumbe wa sms labda atauona .

Kama nilivyokuambia mwanzoni ni MAMA mtu mzima si mtoto mdogo wala kijana.
Anaweza hata kuwa umri sawa na mamako mzazi au mama yangu au kapita zaidi.

Wao simu zao unajua wanaziweka sio kama sisi kutwa ziko mikononi.

Kwa iyo mtafuteni au bandikeni namba zenu pale mlangoni kwake kama mkimkosa akija atawapigia yeye akiona huo ujumbe kwenye mlango wake.

Tumieni njia mnazozijua nyie na kumpata huyo mteja wenu.

Kila la heri. Kazi njema.
 
Tumerudi kwako kwakuwa wewe umekuwa ukitulaumu kuwa hatujamfikia lakini hapokei simu za wataalamu wa Bagamoyo wala Makao Makuu hivyo tukisihi kutoa msaada wa jinsi ya kumuhudumia kwa kuwa hapokei simu na eneo tulilofika hakuna mtu majirani wanada anamwezi hayupo
 
Nimewalaumu sababu niliongea na jana na kumuuliza kama mlifika, akaniambia hamjafika wala kumpigia.

Sasa yule mama ni mzee inawezekana hajaona miss call .

Na pengine hata hajui kucheki misscall.

Sikuwalaumu bila sababu.

Nilichukua maelezo ya mama ndio nikawalaumu.

Shirika kuaumiwa ni kawaida na sio ajabu.

Muhimu unamuelekeza mteja na mwisho wa siku mteja anawaelewa.

Usiogope kulaumiwa.

Mpigieni mida ya asubuhi kama mida hii inawezekana jua likiwa kali anaingia ndani kuwasubiria.
 
Tunapenda kusikiliza sana wateja wetu na malalamiko ni sehemu ya mrejesho kwetu lakini ukileta JF na kutunyoeshea kidole bila kutoa ushirikiano inakuwa sio sawa kwa kuwa unatujengea taswira mbaya.

Toa taarifa

Fatilia

Pata mrejesho kamili

Tupo kukuhudumia
 
Taarifa imeanza kutolewa Tanesco bagamoyo na ikapewa namba 890

Wewe ukasema hiyo namba 890 inasema iko mlandizi ( hapo makosa ya nani ? )

Haya nikafatilia kumuuliza yule mama kama mlienda na yule mama akaniambia hamjafika, ( hapo kosa liko wapi ? )

Ndo mwisho nikalaumu.

Lakini ulipotuma picha za mafundi wako hapo nikaamini na nikajua tatizo liko kwa yule MAMA MTU MZIMA.

ndo nikasema mtafuteni mumpate kwa njia mnayoijua hata kubandika namba zao hao mafundi waliofika hapo mlangoni kwake..au kama hawawezi kuweka namba basi waweke hata UJUMBE HUU

FIKA TANESCO BAGAMOYO MUONE ......

akiona huo ujumbe atakuja au atatafuta kijana amsaidie kuja kama yeye hawezi au hapajui.

Asante mkuu kazi njema.
 
Tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Simu

Tatizo

Toka lini

Kwa hatua zaidi
Je Remote ya Kuingizia Token Number inapogoma kupanch baadhi ya Namba wakati wa Kuingizia Umeme tatizo linakuwa ni nini na nini kifanyike?
 
Je Remote ya Kuingizia Token Number inapogoma kupanch baadhi ya Namba wakati wa Kuingizia Umeme tatizo linakuwa ni nini na nini kifanyike?
Ndugu mpendwa mteja wetu

Tunashukuru kwa taarifa yako, Tafadhali onyesha taarifa kamili ili kuturahisishia kufatilia na kufanyia kazi taarifa zako kama ifuatavyo[emoji116]

Jina...

Eneo...

Wilaya...

Simu...

Tatizo...

Umetoa taarifa lini (Tar..Mwezi.. Mwaka)...

Kama una namba ya taarifa...


Simu zetu za Huduma kwa Wateja[emoji116]

0768 985 100/022 219 4400

TANESCO Huduma kwa Wateja

Makao Makuu
 
Tunashukuru kwa uungwana wako akipatikan tutamfikia mkuu
 
Tafadhali tambua mteja halipi nguzo wala mita kwa kuwa vyote hivi ni mali ya TANESCO bali mteja analipia gharama halisi ya kuunganishiwa umeme ambapo vijijini ni 27000 mijini 321000 ndani ya mita 30 kutoka kwenye miundombinu iliyopo
Mbona Mimi nililipishwa Sh 515,000/= kuingiza Umeme na Kuambiwa ni pamoja na Nguzo na TANESCO KIGAMBONI?
 

Kuna Tatizo Tanesco Geita.

Hasa watu wa chini.

Kinachoendelea Mwabasabi ,Sio kwamba taarifa hazijulikani?
 
Tatizo:Control Number

Eneo : Mwatulole Geita Mjini

Jina 😀atius Theophil Kyobya

Toka lini: Survey ilifanyika November 2020 Hadi Leo Control number haijatoka

Simu: +255 758 515 989

Mkoa: Geita

Wilaya :Geita Mjini
 
Tatizo:Control Number

Eneo : Mwatulole Geita Mjini

Jina 😀atius Theophil Kyobya

Toka lini: Survey ilifanyika November 2020 Hadi Leo Control number haijatoka

Simu: +255 758 515 989

Mkoa: Geita

Wilaya :Geita Mjini
Je ulipatiwa maelekezo yeyote ya kwanini haukupatiwa? Je ulipo umeme umefika?
 
Tatizo:nimelipa gharama za kuunganishwa umeme sijafanikiwa kuunganishiwa umeme

Eneo : Busenga Ilemela Mwanza

Jina: Christopher Laurent Esomba

Toka lini: nilfanya malipo tarehe 23/10/2020

Kiambatanisho cha malipo:
Malipo yamepokelewa kwenda TANESCO
Ankara Na: 991032135543
Kiasi: 515617.52 TZS
Risiti Na: 920297014749416
Tarehe: 2020-10-23T12:48:32
Kupitia:FH890871603446510


Simu: +255 764112724

Mkoa: Mwanza

Wilaya :Ilemela
 
Ahsante kwa taarifa tunafanyia kazi
 
Meneja wa Tanesco Monduli awajibike kwa athari zozote zitakazotokea. Watu wameripoti kuhusu miti iliyoko karibu Na Nyumba zao inagusa waya Na kutoa moto Mara kwa mara wakiomba ushirikiano wa kuikata hakuna kinachofanyika wengine report ni mwaka sasa
 
Tatizo lilianza nilipofungiwa mita ,alikuja mfanyakazi wenu kuunganisha umeme sasa baada ya kufanya kazi akamwambia wife ampe chochote ili mita isiwe inakula unit,qkadai apewe 70000 ,wife akamgome yule bwana akaomba ngazi akapanda juu ya mita sasa sijui aliichezea vipi akashuka nakuondoka zake akqmwambia wife nnajua utanitafuta tu akadai kuwa si ameona 70000 ni nyingi ataona,ndugu zangu tokea siku hiyo utafikiri ninakiwanda humu ndani ,wakati ni tv,taa zipo 9 na frigde lakini umeme wa elfu 50 haumalizi siku kumi yaani,baada ya kufuatilia saana ikaonekana yule jamaa alitapeli sehem nyingine na kashafukuzwa kazi ila sasa nikaelekezwa kuandika barua mpaka wa leo ni maumivu kabisa,ninakaa madale tunahudumiwa na wilaya ya ubungo,mtaa wetu unaitwa kwa mzungu.
 
Nikipona hili janga ntapumua asee maana nataka kukimbia nyumba kabisa maana bila laki na nusu kwa mwezi sitoboi mwezi yaani,nateseka sana,nimefikiria nijichange niweke sola tu liumeme niwaite mje mlitoe limita lenu kwangu.
 
Tanesco kisesa isangijo mnampango Gani na Sisi Mnatuzunguka tuuu leo mnaweka huku malaga huku wengine mnatuluka tatizo nini kama ni form mtaa mzima tusha leta iLA ndo hivyo since 2020 mnazunguka tuuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…