bcsolution
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 394
- 177
Kiongozi mimi nimemsaidia tu huyo mama.Kwa taarifa za majirani inaonekana mteja hayupo eneo hilo mwezi sasa hivyo tunaba utusaidie taarifa kamili au wewe utusaidie namba yako ya simu
Tupo kukuhudumia
Nimemuonea huruma mtu mzima na hajui mambo ya mitandao.
Na nimemkuta analalamika kwamba hajui cha kufanya.
Nimetoa msaada tu kwake.
Nyie kama TANESCO mtafuteni namba nimewapa.
Namba zangu za simu hata nikikupa hazitosaidia sababu sipo tena huko Bagamoyo nishaondoka.
Fanyeni njia mjuayo mumpate mteja wenu.
Namba ya simu nimewapa PM.
Jaribuni kumpigia tena au hata kutuma ujumbe wa sms labda atauona .
Kama nilivyokuambia mwanzoni ni MAMA mtu mzima si mtoto mdogo wala kijana.
Anaweza hata kuwa umri sawa na mamako mzazi au mama yangu au kapita zaidi.
Wao simu zao unajua wanaziweka sio kama sisi kutwa ziko mikononi.
Kwa iyo mtafuteni au bandikeni namba zenu pale mlangoni kwake kama mkimkosa akija atawapigia yeye akiona huo ujumbe kwenye mlango wake.
Tumieni njia mnazozijua nyie na kumpata huyo mteja wenu.
Kila la heri. Kazi njema.