Eneo: Mzenga Sekondari na maeneo jirani.

Wilaya: Kisarawe, Pwani.
(Tunahudumiwa na ofisi ya Mlandizi)

Kero: Hatuna umeme tangu Ijumaa 12/02/2021 usiku.

Tunaomba mtatue hii kero tafadhali!
 

Nguzo moja ni shilingi ngapi?
 
Ahsante kwa taarifa tafadhali onyesha namba ya simu kwa hatua zaidi
Ndugu mpendwa mteja wetu

Wataalamu wetj wamefatilia mpaka serikali ya mtaa hakuna taarifa hii tafadhali onyesha namba yako ya simu kwa hatua zaidi
 

Ahsante kwa taarifa tafadhali onyesha namba ya simu kwa hatua zaidi

Ndugu mpendwa mteja wetu

Wataalamu wetj wamefatilia mpaka serikali ya mtaa hakuna taarifa hii tafadhali onyesha namba yako ya simu kwa hatua zaidi
 
NAKATAA kwa herufi kubwa hamjafika kitongoji cha lyalamu,kijiji cha Ilunda,Kata ya mtwango,mkoa wa Njombe kufanya marekebisho mbaka muda huu kupo Giza kwa siku 4 hamjafika kutengeneza halafu mnanambia mmefika hamjaona tatizo kwa kudai niweke namba ya simu
Hebu acheni urongo kuuhadaa umma kwamba mmekuja na hakuna tatizo hivi mnapata faida gani kudanganya ?

Mtanifanya niandike shit mods wanipe ban hapa kwa ajili yenu
Hebu fikeni hilo eneo mtatue tatizo
Naishia hivi!
 
Tunaomba kutatatuliwa Tatizo la umeme kukosa nguvu maeneo ya mtwara DC katika kata ya Libobe
Wananchi tumewasiliana na Tanesco mtwara huduma ya dharula lkn wameendelea kutupa matumaini Kila siku. Tatizo hili leo ni siku ya nne tuna umeme wa Taa tu hata TV hauwashi na Baadhi ya nyumba hauwaki kabisa

Tunaomba Sana,biashara zinazohitaji umeme zimesimama
 
Asante, tunaweza kupata namba yako ya simu ndugu mteja
 
Rumepokea kwa hatua za haraka zaidi
 
asante tumelipokea na tutalifanyia kazi
Habari za kazi na poleni kwa majukumu. Nipo turiani morogoro nyumba yangu ilipo umepita umeme wa REA na nyumba za jirani wameasha washiwa mimi sikuwa na nguzo baada ya kufwatilia nilipewa nguzo na kuvutiwa waya lakini nguzo haina waya wa stay unaoshika nguzo nimefwatilia mpka kwa meneja naambiwa subiri watu wa REA wakitoka kilosa watafunga umepita mwaka sasa na bado sijapata huduma hadi nimekata tamaa naomba ushauri labda kuna namna nyingine naweza kufanya niwashiwe umeme maana hata kulipia tu nimekatazwa mpka niwekewe stay. Asante
Namba yangu ya simu ni 0621066798
 
Ahsante kwa taarifa tumepokea kwa hatua zaidi
 
Tafadhali onyesha namba ya simu kwa hatua zaidi
 
Tunashukuru kwa taarifa

Tafadhali weka namba ya simu hata inbox tuweze kukuhudumia kwa kuwa lengo la kutoa taarifa ni kuhudumiwa na imekuwa vigumu kukupata bila mawasiliano
 
Maimuna Ahmadi
Kivule kwa ticha
Ilala
Dar es salaam
0715 737 203/0768 333 953
Tatizo letu ni nguzo kuwa ndani ya eneo letu (kiwanja chetu)

Huu ni mwaka was nne sasa, tunaenda Tanesco Gongolamboto, tunaandika barua, tunakutana na viongozi. Wanatuambia eti magari yote mabovu hawana magari. Kila tunaenda kuwaomba waje tuisogeza tu hawataki.

Nguzo zimekaa vibaya, siwezi endeleza eneo langu. Maana nyaya zinapita kati kati. Hata ukuta nashimdwa kujenga.

Tunaomba huko Tanesco makao makuu mtusaidie. Sidhani kama hili ni jambo gumu sana.
 
Ila TANESCO mnajitahidi mno kujibu humu ndani na pia mno moyo, taasisi nyingi zimekimbia ila nyie mmebakia, hongereni......

Hivi kwanini nyinyi mnasubiria wateja wawafate ili kuunganishiwa huduma, kwanini msitafute wateja nyinyi afu gharama mtakatana mbele kwa mbele?
 
Tunawatafute wateja wetu

Tumepunguza bei vijijini sasa ni 27000 tu sawa na jogoo wawili tu hivyo maombi ya wateja ya umeme ni mengi tunaendelea kuwafungia kwa ari kubwa zaidi
 
Ahsante kwa taarifa

Je unaweza kutuma naka hata kwa picha ya barua hizo kwenye namba 0714219508
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…