TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Eneo: Mzenga Sekondari na maeneo jirani.

Wilaya: Kisarawe, Pwani.
(Tunahudumiwa na ofisi ya Mlandizi)

Kero: Hatuna umeme tangu Ijumaa 12/02/2021 usiku.

Tunaomba mtatue hii kero tafadhali!
 
ZIJUE TARATIBU ZA KUFATA ILI KUFUNGIWA UMEME NA TANESCO

HATUA YA KWANZA
(MAOMBI YA MWANZO

[emoji843]Mteja anaweza kuchukua fomu ya maombi ya umeme katika ofisi yeyote ya shirika ndani ya kanda yake bila kujali kuwa eneo hilo linahudumiwa na ofisi husika. Ila atapaswa kurudisha ofisi ya maeneo ambayo makazi yake yapo ili kurahisisha kufanyiwa vipimo (service line survey)

[emoji843]Fomu za maombi ya umeme zinatolewa bure kabisa kwa wateja wote

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA WAKATI WA KUCHUKUA FOMU

[emoji843]Hakikisha umeme umefika maeneo yako na kama ni mradi uwe umekamilika.

[emoji843]Hakikisha mtandao wa nyaya ndani ya nyumba yako (wiring) umefanyika kupitia mkandarasi aliyesajiliwa na umekamilika (orodha zao zipo TANESCO)

[emoji843]Kitambulisho kinachomtambulisha muombaji wa umeme mfano leseni ya udereva, hati ya kusafiria, Kitambulisho cha taifa nk (hii inasaidia shirika kumtambua mteja husika)

[emoji843]Kwa mwombaji wa mita ya ziada (meter separation) jina litakalotumika ni la mwenye nyumba kama linavyosomeka katika mita ya awali. Vinginevyo mteja atapaswa kutumia uthibitisho wa maandishi wa ruhusa ya mwenyenyumba. mteja anashauriwa kuja na namba ya mita (kama zipo zaidi ya moja aje nazo zote) ili kuhakiki kama kuna yenye deni. (kama mita ya awali ina deni hatoruhusiwa kuomba mita ya pili)

[emoji843]Kwa waombaji wanaomba kwa ajili ya ofisi, makapuni au taasisi za serikali au binafsi anapaswa kuja na leseni ya biashara, tin namba, udhibitisho wa usajili wa kampuni. Au udhibitisho wa ofisi ya husika.

[emoji843]Kwa wapangaji wa nyumba za taasisi au makampuni waje na barua za waliopangisha zinazoonyesha kuwe wenye nyumba hizo wameridhia mita husika iwe na jina la mpangaji husika au la taasisi husika

[emoji843]Shirika linapenda kuwaomba wamiliki wa nyumba kupenda kufika ofisi zetu wenyewe ili kuzuia udanganyifu ambao umekuwa ukifanywa na baadhi ya watu wasiokuwa waaminifu

HATUA YA PILI KUWEKA MCHORO, PICHA NA KUINGIA MAKUBALIANO YA KUFUNGIWA UMEME NAKUREJESHA FOMU

[emoji843]Endapo mteja atakidhi vigezo na masharti ya hatua ya mwanzo na kupatiwa fomu ya maombi ya mwanzo anatakiwa afanye yafuatayo:-

[emoji843]Kuisoma fomu ( Mkataba wa kufungiwa umeme baina ya mteja na TANESCO) kwa umakini mkubwa na kukubailiana na vigezo namba moja hadi kumi na mbili. Mteja akijiridhisha kuwa amekubaliana na masharti yote ataweka sahihi sehemu husika (ukurasa wa pili wa fomu ya maombi ya umeme)

[emoji843]Kumpatia mkandarasi aliyesajiliwa ili achore mchoro wa mtandao wa nyaya (wiring diagram) wa nyumba husika pamoja na kugonga muhuri. (gharama ni makubaliano baina ya mteja na mkandarasi husika), wakandarasi wanapatikana kwenye ofisi zao maeneo mbalimbali, orodha ya waliosajiliwa pia inapatikana kwenye ofisi za TANESCO. Mteja anapaswa kupewa orodha na kuchagua mkandarasi anayemtaka yeye.

[emoji843]Mteja atapaswa kuweka picha moja ya mwombaji wa umeme

[emoji843]Kisha mteja atarudisha fomu hiyo iliyokamilika ofisi ya eneo ambalo makazi yake yako (inayomudumia)

HATUA YA TATU- KUFANYIWA VIPIMO (SURVEY)

Mara baada ya mteja kurejesha fomu iliyojazwa kikamilifu, mteja atapangiwa tarehe ya kufanyiwa vipimo (survey). Mafundi watafika kwenye nyumba au sehemu inayoombewa umeme ili kutathimini gharama atakazolipia mteja kwa kuzingatia umbali wa eneo ilipo miundombinu ya umeme kama nguzo na transfoma na uwezo wa umeme huo kuunganisha kwa wateja wapya.

HATUA YA NNE: - KUPATIWA MAKADIRIO YA GHARAMA KIASI GANI ALIPE ILI AFUNGIWA UMEME

[emoji843]Mara baada ya kufanyiwa tathimini mteja anaweza kupatiwa makadirio ya gharama ya kiasi gani alipe ili kufungiwa umeme. Makadirio haya huweza kutumwa kwa njia ya nukushi, ujumbe mfupi wa meneno, barua pepe au mteja kufika ofisini na kuchukua barua. Viwango vya muda wa kutoa makadirio kama inavyoonekana hapo chini:

Muda wa kupimiwa ka kupewa makadirio

[emoji843]Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu) Ndani ya siku 7 za kazi

[emoji843]Ujenzi wa njia ya nyongeza unahitajika (mita 30- 100) Ndani ya siku 10 za kazi

[emoji843]Kama mfumo mpya wa usambazaji unahitajika kujegwa au mfumo wa umeme mkubwa unahitajika kuongezwa kwa ajili ya kiwanda au biashara kubwa (kama hakuna mfumo wa kumuunganishia mwombaji) (zaidi ya mita 100)
Ndani ya siku 14 za kazi

HATUA YA TANO: - KUFANYA MALIPO

Mteja atafika ofisi ya TANESCOA ili kupatiwa namba ya kumbukumbu (Control Number) itakayomuwezesha kufanya malipo bank, mteja atafanya malipo na atapatiwa stakabadhi ya malipo bank (risiti kwa njia ya ujumbe mfupi- sms).wateja wanahimizwa kufanya malipo yote bank na si kwa mtu mwingine yeyote. Malipo yote yatakayofanyika nje ya mfumo uliwekwa hayatambulika. Mteja akishafanya malipo bank husika hatatakiwa kurudi tena TANESCO bali TANESCO watakuwa na taarifa zake zote kupitia mifumo kuwasiliana na kinachofuata ni kumfungia umeme.

HATUA YA SITA:-KUUNGANISHIWA UMEME

Mara baada ya mteja kufanya malipo viwango vya muda wa kumfungia umeme vitakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye jedwali hapo chini.

[emoji843]Kama miundombinu iliyopo itatumika (ndani ya mita 30 kutoka kwenye nguzo iliyokaribu) mteja atafungiwa umeme ndani ya siku 30 za kazi

[emoji843]Kama ujenzi wa njia ya nyongeza utahitajika (mita 30- 100) mteja atafungiwa umeme ndani ya siku 60 za kazi

[emoji843]Kama mfumo mpya wa usambazaji utahitajika kujengwa au mfumo wa umeme mkubwa utahitajika kujengwa ( kama hakuna mfumo eneo husika) yaani zaidi ya mita 100 kutoka kwenye nguzo ya TANESCO mteja atafungiwa umeme ndani ya siku 90 za kazi

KWA MAULIZO WASILIANA HUDUMA KWA WATEJA

[emoji338]Kituo cha huduma kwa wateja Makao Makuu: - 0768985100/0222194400

[emoji843]Barua pepe: customer.Service@tanesco.Co.Tz

[emoji843]Facebook: www.Facebook.Com/tanesco yetu

[emoji843]Twitter: - www.Twitter.Com/tanesco yetu

[emoji843]Tovuti; www.Tanesco.Co.Tz
[emoji843]WhatsApp za huduma kwa wateja Nchi nzima

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA ZETU

TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO

Nguzo moja ni shilingi ngapi?
 
Ahsante kwa taarifa tafadhali onyesha namba ya simu kwa hatua zaidi
Ndugu mpendwa mteja wetu

Wataalamu wetj wamefatilia mpaka serikali ya mtaa hakuna taarifa hii tafadhali onyesha namba yako ya simu kwa hatua zaidi
 
TANESCO naomba mje hapa kitongoji cha lyalamu,kijiji cha Ilunda,kata ya mtwango,mkoa wa Njombe kwenye transformer yenu ya REA inaharibika kila wiki toka nifike hapa umeme unawaka siku 2 unakata siku 5 nadhani machine yenu inatatizo LA kujizima ghafla mafundi wakija wanatengeneza lakini tatizo linajirudia,na mwezi uliopita waliwachangisha wakazi wa hapa Tsh 3000 kila mmoja wawalipe mafundi wenu lakini still umeme bado unazingua ,nadhani tumeelewana msaada unahitajika sababu ni kero sana!

Ahsante kwa taarifa tafadhali onyesha namba ya simu kwa hatua zaidi

Ndugu mpendwa mteja wetu

Wataalamu wetj wamefatilia mpaka serikali ya mtaa hakuna taarifa hii tafadhali onyesha namba yako ya simu kwa hatua zaidi
 
NAKATAA kwa herufi kubwa hamjafika kitongoji cha lyalamu,kijiji cha Ilunda,Kata ya mtwango,mkoa wa Njombe kufanya marekebisho mbaka muda huu kupo Giza kwa siku 4 hamjafika kutengeneza halafu mnanambia mmefika hamjaona tatizo kwa kudai niweke namba ya simu
Hebu acheni urongo kuuhadaa umma kwamba mmekuja na hakuna tatizo hivi mnapata faida gani kudanganya ?

Mtanifanya niandike shit mods wanipe ban hapa kwa ajili yenu
Hebu fikeni hilo eneo mtatue tatizo
Naishia hivi!
 
Tunaomba kutatatuliwa Tatizo la umeme kukosa nguvu maeneo ya mtwara DC katika kata ya Libobe
Wananchi tumewasiliana na Tanesco mtwara huduma ya dharula lkn wameendelea kutupa matumaini Kila siku. Tatizo hili leo ni siku ya nne tuna umeme wa Taa tu hata TV hauwashi na Baadhi ya nyumba hauwaki kabisa

Tunaomba Sana,biashara zinazohitaji umeme zimesimama
 
Asante, tunaweza kupata namba yako ya simu ndugu mteja
 
NAKATAA kwa herufi kubwa hamjafika kitongoji cha lyalamu,kijiji cha Ilunda,Kata ya mtwango,mkoa wa Njombe kufanya marekebisho mbaka muda huu kupo Giza kwa siku 4 hamjafika kutengeneza halafu mnanambia mmefika hamjaona tatizo kwa kudai niweke namba ya simu
Hebu acheni urongo kuuhadaa umma kwamba mmekuja na hakuna tatizo hivi mnapata faida gani kudanganya ?

Mtanifanya niandike shit mods wanipe ban hapa kwa ajili yenu
Hebu fikeni hilo eneo mtatue tatizo
Naishia hivi!
Rumepokea kwa hatua za haraka zaidi
 
asante tumelipokea na tutalifanyia kazi
Habari za kazi na poleni kwa majukumu. Nipo turiani morogoro nyumba yangu ilipo umepita umeme wa REA na nyumba za jirani wameasha washiwa mimi sikuwa na nguzo baada ya kufwatilia nilipewa nguzo na kuvutiwa waya lakini nguzo haina waya wa stay unaoshika nguzo nimefwatilia mpka kwa meneja naambiwa subiri watu wa REA wakitoka kilosa watafunga umepita mwaka sasa na bado sijapata huduma hadi nimekata tamaa naomba ushauri labda kuna namna nyingine naweza kufanya niwashiwe umeme maana hata kulipia tu nimekatazwa mpka niwekewe stay. Asante
Namba yangu ya simu ni 0621066798
 
Ahsante kwa taarifa tumepokea kwa hatua zaidi
 
Tunaomba kutatatuliwa Tatizo la umeme kukosa nguvu maeneo ya mtwara DC katika kata ya Libobe
Wananchi tumewasiliana na Tanesco mtwara huduma ya dharula lkn wameendelea kutupa matumaini Kila siku. Tatizo hili leo ni siku ya nne tuna umeme wa Taa tu hata TV hauwashi na Baadhi ya nyumba hauwaki kabisa

Tunaomba Sana,biashara zinazohitaji umeme zimesimama
Tafadhali onyesha namba ya simu kwa hatua zaidi
 
NAKATAA kwa herufi kubwa hamjafika kitongoji cha lyalamu,kijiji cha Ilunda,Kata ya mtwango,mkoa wa Njombe kufanya marekebisho mbaka muda huu kupo Giza kwa siku 4 hamjafika kutengeneza halafu mnanambia mmefika hamjaona tatizo kwa kudai niweke namba ya simu
Hebu acheni urongo kuuhadaa umma kwamba mmekuja na hakuna tatizo hivi mnapata faida gani kudanganya ?

Mtanifanya niandike shit mods wanipe ban hapa kwa ajili yenu
Hebu fikeni hilo eneo mtatue tatizo
Naishia hivi!
Tunashukuru kwa taarifa

Tafadhali weka namba ya simu hata inbox tuweze kukuhudumia kwa kuwa lengo la kutoa taarifa ni kuhudumiwa na imekuwa vigumu kukupata bila mawasiliano
 
Maimuna Ahmadi
Kivule kwa ticha
Ilala
Dar es salaam
0715 737 203/0768 333 953
Tatizo letu ni nguzo kuwa ndani ya eneo letu (kiwanja chetu)

Huu ni mwaka was nne sasa, tunaenda Tanesco Gongolamboto, tunaandika barua, tunakutana na viongozi. Wanatuambia eti magari yote mabovu hawana magari. Kila tunaenda kuwaomba waje tuisogeza tu hawataki.

Nguzo zimekaa vibaya, siwezi endeleza eneo langu. Maana nyaya zinapita kati kati. Hata ukuta nashimdwa kujenga.

Tunaomba huko Tanesco makao makuu mtusaidie. Sidhani kama hili ni jambo gumu sana.
 
Ila TANESCO mnajitahidi mno kujibu humu ndani na pia mno moyo, taasisi nyingi zimekimbia ila nyie mmebakia, hongereni......

Hivi kwanini nyinyi mnasubiria wateja wawafate ili kuunganishiwa huduma, kwanini msitafute wateja nyinyi afu gharama mtakatana mbele kwa mbele?
 
Tunawatafute wateja wetu

Tumepunguza bei vijijini sasa ni 27000 tu sawa na jogoo wawili tu hivyo maombi ya wateja ya umeme ni mengi tunaendelea kuwafungia kwa ari kubwa zaidi
 
Maimuna Ahmadi
Kivule kwa ticha
Ilala
Dar es salaam
0715 737 203/0768 333 953
Tatizo letu ni nguzo kuwa ndani ya eneo letu (kiwanja chetu)

Huu ni mwaka was nne sasa, tunaenda Tanesco Gongolamboto, tunaandika barua, tunakutana na viongozi. Wanatuambia eti magari yote mabovu hawana magari. Kila tunaenda kuwaomba waje tuisogeza tu hawataki.

Nguzo zimekaa vibaya, siwezi endeleza eneo langu. Maana nyaya zinapita kati kati. Hata ukuta nashimdwa kujenga.

Tunaomba huko Tanesco makao makuu mtusaidie. Sidhani kama hili ni jambo gumu sana.
Ahsante kwa taarifa

Je unaweza kutuma naka hata kwa picha ya barua hizo kwenye namba 0714219508
 
Back
Top Bottom