Mteja halipii nguzo wala mita bali analipia kiasi halisi cha kufungiwa umeme hivyo wa vijijini wote ni Tsh 27000 na mijini gharama ni zile zile

Swali langu ni kuwa kuna baadhi ya wateja wa mijini kama ni service line tu wanalipia 321,000/= kuunganishwa ila kama inahitajika kuongeza nguzo moja mpaka kwenye nyumba basi unalipia 521,000/= sasa ndio maana nikauliza kama nguzo ni bure why kuwe na fedha tofauti? Hiyo laki 2 iliyoongezeka ni Gharama za nyaya zilizoongezeka kwa ajili ya kuongeza nguzo au kuilipia nguzo?
 
ndugu mteja,
TANESCO hatuuzi nguzo, gharama unayopewa ni kwa ajilii ya kuunganishiwa umeme kutokana na umbali uliopo na sehemu ya mwisho ambapo umeme umeisha
 
ndugu mteja,
TANESCO hatuuzi nguzo, gharama unayopewa ni kwa ajilii ya kuunganishiwa umeme kutokana na umbali uliopo na sehemu ya mwisho ambapo umeme umeisha
Hivi Tanesco kuna mgao unaendelea nchini au?
 
ndugu mteja,
TANESCO hatuuzi nguzo, gharama unayopewa ni kwa ajilii ya kuunganishiwa umeme kutokana na umbali uliopo na sehemu ya mwisho ambapo umeme umeisha
Huku Arusha ni mgao wa umeme au kitu gani? Tunaomba taarifa tujue. Kila siku mnakata umeme asubuhi mnarudisha usiku.
 
Huku Arusha ni mgao wa umeme au kitu gani? Tunaomba taarifa tujue. Kila siku mnakata umeme asubuhi mnarudisha usiku.
Subiri jibu lao rahisi tu la tunatengeneza mitambo yetu.

Tanesco inaangazia maisha yako.
 
Subiri jibu lao rahisi tu la tunatengeneza mitambo yetu.

Tanesco inaangazia maisha yako.
Basi tupewe taarifa jamani, mtu uamke ukijua leo hakutakuwa na umeme na pia tuelezwe inachukua muda gani.
Kazi za watu wengi zinategemea umeme. Tanesco mnaturudisha nyuma kimaendeleo..mnakata umeme mpendavyo, mnakera kupita maelezo.
TANESCO
 
ndugu mteja,
TANESCO hatuuzi nguzo, gharama unayopewa ni kwa ajilii ya kuunganishiwa umeme kutokana na umbali uliopo na sehemu ya mwisho ambapo umeme umeisha
Naomba mrudishe umeme hapa arusha angalau kwa dakika 10 nipasi chap nguo zangu then muendelee na mgao wenu.
 
Jamani Tannesco toeni basi ratiba ya mgao ,huku mbezi Beach ndio umerudi saaa moja .Tuambieni basi kesho mnakata maeneo gani ili tuamishe majeshi huko tufanye kazi
 
Jamani Tannesco toeni basi ratiba ya mgao ,huku mbezi Beach ndio umerudi saaa moja .Tuambieni basi kesho mnakata maeneo gani ili tuamishe majeshi huko tufanye kazi
Wakikujibu watakuambia tutumie namba yako ya simu.
 
Jamani Tannesco toeni basi ratiba ya mgao ,huku mbezi Beach ndio umerudi saaa moja .Tuambieni basi kesho mnakata maeneo gani ili tuamishe majeshi huko tufanye kazi
ndugu mteja, hakuna mgao ni matengenezo. pole sana kwa usumbufu unaopata
 
Temeke huku juzi kutwa nzima umeme umerudi saa nne usiku, jana pia kutwa nzima ukarudishwa sijui saa mbili usiku ila hiyo haitoshi kwenye saa saba usiku umekatika tena mpaka saa kumi alfajiri na hili joto la Dar aisee halafu bila hata taarifa sasa, TANESCO mnayaangaza maisha yapi?
 
Shirika la umeme Tanzania lipo kama halipo vile......
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

MACHI 01, 2021

TAARIFA YA MATENGENEZO KATIKA VITUO VYA KUZALISHA UMEME KWA GESI VYA SONGAS NA UBUNGO II

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake kuwa tunaendelea kufanya matengenezo ya miundombinu ya Umeme katika vituo vya kufua Umeme kwa Gesi Asilia vya Songas na Ubungo II.

Kutokana na matengenezo hayo, baadhi ya maeneo nchini yataathirika kwa kukosa huduma ya Umeme kwa nyakati tofauti.

Wataalamu wetu na mafundi wanaendelea na kazi kuhakikisha mitambo inatengemaa haraka.

Tutaendelea kutoa taarifa kadili kazi ya matengenezo inavyoendelea.

Tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza

Tafadhali usiguse wala kukanyaga waya uliokatika au kudondoka chini.

Toa taarifa Ofisi za TANESCO zilizo karibu nawe, au wasiliana nasi kupitia namba za simu zifuatazo: - Kitengo cha Miito ya Simu 0222194400 na 0768 985100

Mitandao ya Kijamii :
Website:

www.tanesco.co.tz

Instagram: tanesco_official_page

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz,

Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook: Tanesco Yetu

Imetolewa na;
OFISI YA UHUSIANO,
TANESCO MAKAO MAKUU.
 
Toeni ratiba ya mgao kutokana na hayo matengenezo mbona ni kitu rahisi tu.

Mfano kuanzia muda fulani umeme utakatika maeneo xyz. Tujipange.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…