Nichukue nafasi hii kumpongeza waziri wa Nishati kwa kazi kubwa anayoifanya. Pia ni ipongeze wizara nzima na watendaji wake wote kwa ujumla.
Niende moja kea moja kwenye mada. Wakati wa ujuo wa Mh rais wa JMT, Dkt Magufuli kipindi cha kampeni, alikutana na kero ya watu wengi kutofungiwa umeme mjini Babati. Na katika kipindi hicho alitoa mwezi mmoja wa watu kufungiwa umeme. Tunashukuru agizo hilo lilifanyika na wengi kufungiwa umeme.
Tatizo lililojitokeza baada ya watu kufungiwa umeme, ni pale unapoenda Tanesco ili kupata control number kwa ajili ya malipo umeme wako unapokuwa umeisha ili uendelee kutumia mita yako, baadhi ya watumishi wa TANESCO wamekuwa na majibu yasiyo ya kupendeza. Kwanza wamekuwa wakisema ninyi ndio mlifungiwa umeme wa Magufuli, hivyo wanakusumbua kuwa Surveyor anahitajika kuja kwanza kwenye nyumba kuikagua, sasa mtu unajiuliza, umeme tayari ulifungiwa na ukatumia kwa kipindi fulani zile unit zilizopo za mwanzo, iweje sasa unapokatika uzungushwe kama haujawahi kuunganishiwa umeme. Pili basi hao Surveyors ambao ni muhimu, mbona hawafiki kwa wakati katika kuzikagua hizo nyumba na kuhakikisha kuwa watu hawalali na giza?. Je hakuna dalili za rushwa hapo watu wanajitengenezea. Tunaomba meneja wa TANESCO Mkoa ushughulikie kero hii. Kwa pamoja tunaweza.
Imetolewa na muhanga wa kuunganishiwa umeme baada ya tamko la Mh Rais, Mkoani Manyara.
 
Tunakuomba radhi sana mpendwa mteja wetu, Tafadhali tusaidie namba yako ya simu tufatilie na kufanyia kazi swala lako

Huduma kwa Wateja
TANESCO MAKAO MAKUU
 
Mshatukatia umeme sasa hivi Morogoro Manispaa na sio mara moja hivi ni mgao hama ni nini embu tupeni info ?
 
Siku hizi mnakata umeme mara kwa mara,, kwa siku umeme unakatika na kurudi zaidi ya mara kumi! kuna shida gani?
 
Pale Tandale nyumba nyingi zimevunjwa ikiwemo yangu,sasa wamekuja watu wakijidai kutoka Tanesco na kung'oa mita yangu wakishirikiana na s/mitaa
Nimefuatilia Magomeni wanadai hawafamu jambo hilo
Nifanyeje
1) Nipate ile au nyingine
2) Kuzuia hao wezi/vishoka kumuuzia mtu mwingine
TANESCO
 
Chukua polisi loss report kwanza andikia barua kwenda TANESCO ifikishe pale Magomeni Usalama tutaifanyia kazi
 
Asante
 
Naomba kujua ili kubadirishwa tarrif ni taratibu gani zinafatwa
Muhimu sana kuzingatia haya;
1. Uwe mteja mdogo haswa kijijini
2. Kusiwe na biashara yoyote ( hata kupangisha nyumba)
3. Anaomba awe mmiliki wa nyumba na sio mwakilishi
4. Matumizi yawe chini ya unit 75 kwa wastani wa miezi 3 hadi 6
5. Isiwe imewahi kubadilishwa tarrif toka ifungwe
 
Kwahyo mita inapobadirishwa daraja mteja anapea taarifa au inakuwaje.mfano ukibadirishwa kutoka kwa watumiaji wadogo kwenda wakati.
 
Hili bado halijafanyiwa kazi
 
Tanesco (w)Ilala shida ipo wapi kila uchao umeme kukatika kulikoni kama kuna maboresho au marekebisho mbona hatuonani matangazo ili watu wajipange namna ya kuhifadhi bidhaa zilizo kwenye mafriji ili hasara isiwepo?
Natanguliza shukrani kama nitapata majibu mema
 
Kariakoo kila uchao giza leo mtaa wa lindi kesho mtaa mwingine kama kuna mgao semeni watu wanapata hasara pia kama ni matengenezo (maboresho) pia tuambiwe kumbukeni Ilala ndo jiji na linatakiwa kuwa mfano bora kwa miundombinu haswa Umeme
 
Msaada wa haraka, natumaini nitasaidika nyumba yetu imezima umeme yenyewe mita ni ya kwenye nguzo units zipo ni kwamba umeme hautoki kwenye mita. Kupata token za kufungulia ni hadi jumatatu ofisi za tanesco zikiwa wazi, kwa kuwa matumizi ya umeme ni muhimu haswa weekend tunaomba mtusaidie namba ya mita ni 24212097125 TANESCO
 
Namba hizi hazitumwi mpaka wataalamu wetu wafike kwako tafadhali onyesha

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Namba ya taarifa
 
Nanunua umeme inakataa inarudisha ujumbe kuwakilisha there are pending key change needed to be printed, nini tatizo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…