Mimi ni mteja mpya.

Nimepimiwa ( Surveyor mwezi wa 10 mwaka jana nimesubiri simu yenu kimya mbaka nimeamua kuja mwenyewe TANESCO mwezi wa 1
Nimekutana na msamiati mpya andika barua ya kuomba kulipia service line ya nguzo 1.

Nimeandika barua na kisha kikapewa gharama za malipo nimelipa service line ya nguzo toka mwezi wa 1
Nimekaa miezi 7 ndio nimeletewa nguzo

hivi sasa ninavyo ongea hapa nina miezi 2 nguzo imelala chini sioni huduma yeyote ya kuunganishiwa umeme

hapa hisia zangu ninashawishika nitumie vishoka kitu ambacho sikitaki
ebu nambieni TANESCO lini mtanifungia umeme

Nipo Bunju A kanda ya kaskazini
Mkoa wa Dar es salaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaomba jina ulilolipia na namba yako ya simu mpendwa mteja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kwanini swala la Mtwara hamtaki kujibu kila siku mnakata umeme tena ovyo ovyo zaidi ya mara 7 sasa huu mwezi wa nne tunaelekea mkiulizwa mtoe jibu mnaomba namba ya simu ya nini sasa badala mseme tatizo ni nini? na zaidi ikifika tu saa mbili usiku mnakata wakati tunasubiria kuangalia taarifa ya habari mnaboa sana tena sana.
 
Mpendwa mteja
Mtwara ni mkoa mkubwa wenye wilaya nyingi hivyo tunapokuamba taarifa ya eneo lako na mawasiliana yako inatupatia nafasi kulifanyia kazi .ushirikiano wako ni muhimu zaidi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naombeni ufafanuzi wenu iv ni kweli cc wenye matumizi madogo yaan taarif 4 pindi zinapokuwa zinabaki kila mwezi na kufikia zaidi ya unit 150 huwa mnazichukua na kubakiza kidogo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Magomeni karibu na mangowela
TUPATIE TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA.

NDUGU WAPENDWA WATEJA WETU MNAOTOA TAARIFA KUPITIA MITANDAO YETU YA KIJAMII TUNAWAOMBA MZINGATIE YAFUATAYO ILI KURAHISISHA UFAFANUZI NA UFUMBUZI WA TATIZO AU TAARIFA HUSIKA

1.ENEO HUSIKA

(Mnaweza kuwa eneo moja lakini mnahudumiwa na transfoma au njia ya kusambaza umeme (feeder) tofauti)

2.NAMBA YA SIMU

(Wakati mwingine umeme upo kote isipokuwa kwako hivyo na rahisi kuwasiliana na wewe)

3.KARIBU NA NINI

(Kuna alama vitu au watu mashuhuri karibu na eneo lako mfano ofisi ya Serikali ya Mtaa, Mahakama, Kituo cha Polisi nk)

4.JINSI YA KUFIKA MAKAZI YAKO

(Toa ufafanuzi wa jinsi ya kufika makazi yako,chukulia unamuelekeza mtu ambaya hajawahi kufika kabisa)

5.MKOA,WILAYA NA KITONGOJI/KIJIJI

(Taarifa hii ni muhimu sana kusaidia kubaini eneo husika lipo wapi kwani yapo maeneo yanayofanana kwa majina lakini yapo Mikoa tofauti mfano Magomeni ipo Dar es Salaam na Mkoa wa Mtwara pia.)

6.KAMA NI TATIZO LA MITA NINI KINATOKEA UKIWEKA UMEME

(Kila mita ina ujumbe wake unaoashiria kitu fulani hivyo kubainisha ujumbe kunamsaidia mpokea taarifa kukupatia maelezo sahihi mfano mita namba 24339173921 inaonyesha error 77)

7.KAMA NI KUSHINDWA KUNUNUNUA UMEME UNAPATA UJUMBE GANI NA UNANUNUA KWA NJIA GANI

(Ujumbe huu ni muhimu sana kuweza kubaini chanzo cha tatizo pamoja na njia iliyotumika kununulia umeme mfamo Mpesa, Tigopesa, Maxcom nk)


TUNAENDELEA KUWASIHII WATEJA WETU KUZINGATIA UTOAJI WA TAARIFA SAHIHI NA FASAHA KWA HUDUMA BORA ZAIDI KUTOKA TANESCO.

ENDELEA KUFURAHIA HUDUMA BORA KUTOKA TANESCO

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilichogundua hapa sio kabisa hivi kama nyie Tanesco mnashindwa kuwauliza wenzio kweli sisi tutapataje taarifa sahihi.umeme uwezi kukatika kwangu pekee nisigundue acha uongo kwangu si kisiwa, na pia miezi 4 sasa hili tatizo lipo alafu mnaleta ngonjera humu khaa ......
 
Pongezi kwangu tanesco

Baada ya juzi kuja na malalamiko yangu humu ndani nikiwa nimenuna kweli kweli leo natoa pongezi zangu za dhati kwa kupewa stahiki yangu ya huduma ya umeme

Ninapoandika uzi huu dk 15 nyuma nimetoka kuwekewa umeme

Mungu awabariki na nawatakia majukumu mema

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuhh, asante kwa shuhuda mkuu! Kuna watu wanalalamika lakini wakishasikilizwa hawarudi tena hapa ku-acknowledge!

Big up sana TANESCO
 
Juzi nimekasirika sana baada ya kwenda tanesco na kuchukua savea mita kama 30 kutoka kwangu umeme upo.

Jamaa hata kushuka kwenye gari hajataka kaniambia hatupimi nguzo huku subiri mradi ukija, sa nawauliza tanesco mnatusaidia au ni biashara mnafanya, sawa nakubali Kuwa mradi utakuja ila Kwa Muda huu mkituunganishia umeme uliopo kabla ya huo mradi hamwoni Kuwa iko faida mngepata?

Au kuendesha shirika Kwa mazoea na siasa?
 
TANESCO wakati wa kampeni DAR mpya iliyofanywa na RC Makonda mlitoa ahadi kuwa mtaleta umeme huko mtaa wa Zavala kata ya Buyuni by Mei 2017.

Leo Agost 2017 hakuna dalili isipokuws kwa watu wenye uwezo wa kujinunulia nguzo na kutoa cha juu. Je mlimuongopea RC Makonda siku ile ya mkutano
 
Reactions: ADK
Mkuu na wewe habari za Bashite humu za nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…