TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
TANESCO hebu tufanyieni msaada watu wa Kimara mwisho na hili tatizo la kukatikakatika umeme jamani.
Mbona sehemu nyingine tunakwenda tunakaa wiki hadi mwezi umeme haukatiki na mvua zinanyesha nyingi tu?
Kwanini hamzingatii malalamiko ya wateja mrekebishe vitu tusikae tunalalama muda mrefu hivi?
Tatizo la kukatika umeme Kimara mwisho ni sugu mno jamani embu lifikisheni mwisho hili tatizo.
Hapa naandika tangu juzi mvua ikianza tu mnazima umeme.
Leo hata mvua hakuna mmezima umeme.
Miezi mingine isiyo na mvua nayo bado unakatika.
Kimara tumewakosea nini Tanesco?
 
Nina shughuli zangu maili moja kibaha.Mvua zinanyesha ila ni mwezi sasa sijashuhudia umeme ukikatika.
Kimara mwisho hazipiti siku mbili bila umeme kukatwa.Wakati wa mvua kama huu ndio inakuwa kama kisingizio.
Hivi hawa tanesco wenzenu wa maeneo mengine wamewezaje kudumisha huduma bora na Kimara wanashindwa miaka nenda miaka rudi?
Mimi naomba uongozi wa Tanesco ufanye uchunguzi nini kinachosababisha tatizo la kukatika umeme Kimara mwisho na maeneo mengi ya Dar halipatiwi ufumbuzi?
Nina uzoefu wa kuwepo Kimara tangu 2006 sijawahi kuona umeme umetulia walau kwa mwezi tu,haijawahi tokea.
Lazima kuna uzembe kwa timu inayohusika na Kimara.
Ili iweje?ili kila siku muwe site mlipwe overtime?why hamuondoi tatizo moja kwa moja?nyinyi mnaona sifa kupita mitaani na magari yenu mkienda kurekebisha matatizo hayo hayo kila siku?si hujuma hiyo?!
Badilisheni hivyo vinavyosumbua.Kuendelea kusumbua kila vikitengenezwa maana yake vimechoka havifai na vitaendelea kusababisha huduma isiyo na uhakika,iwe ni mtambo wenu huko ubungo,iwe ni matransfoma,waya na nguzo huku mitaani
Fanyeni operesheni ya hata mwezi,badilisheni mfumo wote uliooza wa kimara.tuko radhi kukaa giza hata wiki mbili ilimradi mtutangazie mnafanya jambo litakalokuwa solution ya kudumu,baada ya hapo tusione huu upuuzi ukiendelea.
 
Tanesco app, naomba masaada wenu kila nikiingiza meter number inasema not found
 
Mkitaka Tanesco wa respond, wafuateni kule Twitter. SSH hua anatembelea kule, akiona uvundo umezidi atatenda.
 
Waziri wa Tanesco inabidi ajitafakari kabla hajaambiwa na Mheshimiwa Rais Samia,

Hali ya kukatwa kwa umeme inatisha,

Watu wako gizani almost kila siku, imagine.
 
Kalemani muamgalie mwenzio Waziri wa Maji Jumaa Aweso, amestuliwa na Mama na wewe vipi?

Sauti za wananchi unazisikia ?

Je unatusoma?

Je huna watu wako wakukwambia huku kunafukuta?

Unataka watu wafanye nini ili usikie kilio chao?
 
Almost kila siku lazima umeme ukatwe.

Yani ni mgao kama ndivyo tangazeni tujue, kama ni tatizo la kiufundi kwanini halitatuliwi likaisha?
 
Waziri Kalemani Fanya jambo, fumua fumua uongozi wa watendaji wako Mpaka wale wa vituo vidogo,

Wavuruge kwanza , waache kufanya kazi kwa mazoea.

Waziri wa Tanesco popote ulipo tafadhali.

Wananchi kuwa gizani ni tatizo kubwa sana.

Ni zaidi ya kero.
 
Wameurudisha!

Mnaudhi sana nyie!

Utazani mnatupatia bure wakati mnatuuzia kwa bei ghali. [emoji18][emoji57][emoji57]
 
Nilishangaa kuona miundumbinu ya umeme ikisambazwa vijijini, nikaona ni jambo zuri.

Lakini nikajiuliza Hawa jamaa wamejipangaje kisawasawa kuhakikisha uhakika wa huduma ya Umeme kuwepo throughout the year?

Every year reliably?

Ikiwa hapo awali tu % ya population ilipokuwa ikifikiwa na huduma ya umeme ilikuwa ni waachache nanga zilikuwa zinapaa umeme wa uhakika hakuna inavyoonekana ni mashaka matupu sembuse kuongeza wigo wa usambazaji wa hiyo huduma kwa nchi nzima?!

Sasa ona kinachotokea!
 
Kwa kweli TANESCO kigamboni sijui kuna tatizo gani! Nyumba inakatika umeme tangu mwaka jana mwishoni, ukiita emergency wanakuja (baada ya siku moja au mbili) wanawapa temper number umeme unarudi, unadumu wiki unakata, unawaita routine ni ile ile, mteja unabaki kujiuliza hivi huu mchezo ni mpaka lini? Now ninapoandika hapa, nyumba haina umeme siku ya SABA leo kwa maana tangu ulipokatika last week tukapata temper number jumamosi saa 7 mchana, ukakatika masaa mawili baadae ndo mpaka leo!! Dar es salaam hii kukaa gizani siku 7, nyumba yenye frem za biashara zinazotegemea umeme, wapangaji (wengi wao wanafunzi) wanalala giza siku 7 mfululizo kweli Tanesco mko serious??? Naandika kwa uchungu sana cz ni tatizo la muda mrefu mnooo, kwa nini halipatiwi ufumbuzi? Less than a kilometre from tanesco kigamboni, lkn tupo gizani kama wachawi!!! Hii hali inakatisha tamaa sana, natamani niite kishoka aniungie umeme maisha yaendelee, mkiamua kuja hata baada ya mwaka sitaumia kamwe lakini kwa sasa hivi kila sekunde inayopita inapita na maumivu sana!!
 
Pole sana mpendwa mteja wetu je ni eneo gani haswa na namba yako ya simu kwa hatua zaidi.Jm
 
Ninataka kuulizia Kama kuna mabadiliko ya bei za umeme, Mana nimenunua umeme wa 3000 nikapata 8.5 units, wkt huwa nipo ile tariff ya sh 100/unit.
 
Samahani Tanesco naomba kufahamishwa kama kuna mabadiliko ya bei ya umeme.
 
Kuna afisa wa tanesco aliniambia watu wote wanaotumia umeme ambayo sio wa REA wanaanza kuwekwa kwny tariff za bei ya juu, baada ya kumhoji umeme kwangu umekuwa ghali gafla wkt kea mwezi simalizi hata units 30
 
Back
Top Bottom