TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Nashangaa umeme wa nyumbani kwa Wazee wanapata unit chache kuliko mimi wa mnjini naomba msaada wenu nifanyaje
 
Habari Tabesco Team

Tunaomba mrudishe huduma kwenye Tanesco mobile App... haifanyi kazi takribani wiki sasa
 
Tanesco wilaya ya Moshi, kitengo cha EMERGENCY, mwananchi unaporipoti tatizo la kukatika kwa umeme kwenye mtaa wako, mara nyingi zinafika hadi saa 24 bila ya umeme kurejea. Unaporipoti tatizo unaelezwa mafundi watakuja kufanya matengenezo baada ya muda mfupi lakini mara nyingi zinafika hadi saa 24 bila ya mafundi kufika. Hii hali huwa inatuathiri sana kwasababu huwa tunakaa muda mrefu bila ya kuwa na umeme. Kuna udhaifu mkubwa kwenye kitengo cha emergency Tanesco wilaya ya Moshi hadi inasikitisha.
 
Suluhisho ilikuwa Tanesco mobile App tu
 
Ni masherti yapi mteja aliye ingiziwa umeme kwa mara ya kwanza anatakiwa kuyafuata ili aweze kubadilishiwa tariff kwenda D4. Maana huku niliko maelezo ni mengi hadi nashindwa kuelewa.
 
Tanesco wilaya ya Moshi, kitengo cha EMERGENCY, mwananchi unaporipoti tatizo la kukatika kwa umeme kwenye mtaa wako, mara nyingi zinafika hadi saa 24 bila ya umeme kurejea. Unaporipoti tatizo unaelezwa mafundi watakuja kufanya matengenezo baada ya muda mfupi lakini mara nyingi zinafika hadi saa 24 bila ya mafundi kufika. Hii hali huwa inatuathiri sana kwasababu huwa tunakaa muda mrefu bila ya kuwa na umeme. Kuna udhaifu mkubwa kwenye kitengo cha emergency Tanesco wilaya ya Moshi hadi inasikitisha.
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Nadhani hata meneja wao hajui, lakini wafanyakazi hapo wanadai rushwa sana. Mtu akiomba umeme anazungushwa sana, kwanza saveya haji mpaka utoe rushwa. Akija saveya umeme hupewi hadi utoe rushwa na ikiwa nguzo hakuna basi utaambiwa utoe chai. Pamoja na onyo kali alilotoa Kalemani, watu hawasikii kabisa.

Sasa kalemani fuatilia
 
Kalemani na Biteko ni masalia ya mwendazake

Muda wa kukabidhi ofisi umefika

Walizoea kufanya kazi kwa kiki lakini toka mwendazake aondoke,wamepigwa na butwaa hata kuonekana kwenye vyombo vya habari imekuwa shida.
 
Jana naongea na sista ananiambia umeme wenu wa huko unakapua balaa. Poleni sana, ila ngoja aje.
 
Nadhani hata meneja wao hajui, lakini wafanyakazi hapo wanadai rushwa sana. Mtu akiomba umeme anazungushwa sana, kwanza saveya haji mpaka utoe rushwa. Akija saveya umeme hupewi hadi utoe rushwa na ikiwa nguzo hakuna basi utaambiwa utoe chai. Pamoja na onyo kali alilotoa Kalemani, watu hawasikii kabisa.

Sasa kalemani fuatilia
Huyu waziri mwenyewe ni mzigo bado unamtwisha mzigo
 
Habari TANESCO katika harakati za kununua umeme, kwa wenge la usiku nimekosea meter number, umeme umekuja naweka naona rejected, kufikicha macho natizama vizuri naona nimekosea, napiga airtel naambiwa niwacheki nyinyi mabosi wa nishati tanzania.

Mnanisaidiaje katika hili? Km kuna kauwezekano mnirejeshee tu kafweza kangu ninunue kibando cha wiki.

Shukrani
 
Tafadhali fika na umeme huo ofisi za eneo lako kuna form maalumu utajaza kwa hatua zaidi
 
Niko namalizia kujenga nyumba yangu ila nyumba yangu iko mbali m300 toka nguzo ya mwisho ya REA na mita 100 toka nguzo ya tanesco je nikijitosa kununia nguzo zitakaa ngap na shi ngap
 
TANESCO mnatuangusha sana...nimejenga nyumba ya kupangisha nimemaliza nasubiri umeme wapangaji waingie lakini TANESCO KIGAMBONI hawaeleweki nimelipia kila kitu...nikiiangalia nyumba naumia sana ...
 
Back
Top Bottom