Mi ni fundi umeme wa majumbani.
Nipo Karagwe Kayanga.
Nimekuwa nikifanya kazi zangu vijijini hata wilaya za jirani.
Lakini nimekutana na tatizo la wizi wa umeme/uhujumu.
Wananchi walifungiwa mita lakini hawajawahi kulipia chochote. Huu ni mwaka wa tatu hivi.
Wanahitaji kulipa lakini wamekosa pa kuanzia maana wakienda kulipoti wanaogopa faini. Hili hali walifunga kipindi cha REA.Labda niseme inawezekana kuna namna wizi ulipita kipindi hicho. Maana wengi vijijini hawana elimu sahihi juu ya ufingaji wa umeme.
Hawafahamu habari za wakandarasi wakiwaona wafanyakazi wa TANESCO wanawaomba wawafanyie mifumo yote matokeo unatokea uhujumu.
WIZI WA MITA
Pia kwa sasa kimekuwapo wizi wa mita hasa zinazo pachikwa kwenye nyumba.
Kuna matukio kama matano ambayo nimekwenda kufanya tasimini ya uharibifu. Na kwa tukio baya nimekuta mita zimen'golewa na watuhumiwa hawajulikani.
Wateja huwa nawaelekeza ofisini watoe taarifa .Lakini huwa hawahudumiwi kwa wakati maana kuna taratibu za kuitafuta uanza kufanyika. Labda hamjagundua jambo mi hawa wezi wengine hutumia akili na ndiyo maana huwa mafanikio ya kuwapata hawa wahujumu hayafanikiwi.
Naomba muwe na timu ya kufuatilia uhujumu nje ya mfumo wenu wa ofisi.
Fanyeni upelelezi hata wa kiteknolojia kama inawezekana mita zote ziwe na gps ili ziweze kufuatiliwa kwa ukaribu.
Pili watumie Wakandarasi waaminifu maana wanajuana na wafundi wengi waaminifu.
Hapa chini nitaambatanisha picha ya mita ambayo ilikuwa inakaribia kuibiwa na wahujumu huku amewapa jina la utani.(VISHOKA) Lakini majirani waliwakurupua hawakumaliza hadhira yao. Lakini inavyoonekana hawa wezi waliwahi kuwasiliana kwenye mfumo wenu ama wamo maana wanajua pamoja kuuza hizo mita waibazo.
Pia nawapongeza TANESCO wilaya ya Karagwe kwa utendaji wao wa kazi wakati huu.Kuanzia mapokezi, Mhasibu,Meneja na vijana ambao wanafanya kazi na meneja. Wanajitoa sana maana wateja wangu ambao huwa wanahitaji huduma wanazipa kwa wakati.
Emergency wanastahili kupewa nguvu zaidi maana wanafanya kazi katika mazingira hatari hasa nyakati za usiku. Maana wana maeneo makubwa mno.
Naomba pia kama mtaweza kuipatia nguvu kazi sehemu ya sarveh maana ana eneo kubwa mno na hana usafiri wa kumfikisha eneo la kazi yake kwa wakati.
Walau ofisi impatie usafiri wa pikipiki maana anatembea mwendo mrefu sana na huenda anatumia muda mwingi sana kutembea na miguu kuwasadia wateja wetu.Maana nakumbuka kuna kipindi niliwahi kumuomba amsaidie bibi yangu (SINA MAHUSIANO NAYE YA DAMU) ambaye alikuwa katika mazingira magumu kidogo na kampuni yetu huwa inatoa msaada hasa wa kiufundi na matengenezo ikiwemo na vifaa kwa wazee wazee kama eneo limepata mradi mpya wa umeme.
Lakini survey alitumia gharama zake mwenyewe kujisafisha tena wakati ambapo alikuwa amechoka na kazi ni kama ilikuwa imeisha muda wake anamsaidia bibi huyo.
KWA LEO NAISHIA HAPO ILA WAKATI UJAO NITAKUJA NA JAMBO LINGINE.(UPOTEVU WA MITA ZA WATEJA)
OFISI NINAZO FANYIA KAZI NI
JOSSEPH KOMBA(DANDU )