Kwa kweli
TANESCO kigamboni sijui kuna tatizo gani! Nyumba inakatika umeme tangu mwaka jana mwishoni, ukiita emergency wanakuja (baada ya siku moja au mbili) wanawapa temper number umeme unarudi, unadumu wiki unakata, unawaita routine ni ile ile, mteja unabaki kujiuliza hivi huu mchezo ni mpaka lini? Now ninapoandika hapa, nyumba haina umeme siku ya SABA leo kwa maana tangu ulipokatika last week tukapata temper number jumamosi saa 7 mchana, ukakatika masaa mawili baadae ndo mpaka leo!! Dar es salaam hii kukaa gizani siku 7, nyumba yenye frem za biashara zinazotegemea umeme, wapangaji (wengi wao wanafunzi) wanalala giza siku 7 mfululizo kweli Tanesco mko serious??? Naandika kwa uchungu sana cz ni tatizo la muda mrefu mnooo, kwa nini halipatiwi ufumbuzi? Less than a kilometre from tanesco kigamboni, lkn tupo gizani kama wachawi!!! Hii hali inakatisha tamaa sana, natamani niite kishoka aniungie umeme maisha yaendelee, mkiamua kuja hata baada ya mwaka sitaumia kamwe lakini kwa sasa hivi kila sekunde inayopita inapita na maumivu sana!!