Namba zetu unachukua lakini hupigi wala hata hubip..unazingua sana.
Tanesco mnatuletea umaskini tu
 
Namba zetu unachukua lakini hupigi wala hata hubip..unazingua sana.
Tanesco mnatuletea umaskini tu
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tafadhali tusaidia taarifa kamili ili tuweze kufanyia kazi taarifa zako

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja, JM
 
Tunashukuru kwa ushauri na taarifa mpendwa mteja wetu.Tafadhali tupatie namba yako inbox tuongee na kuweza kufanyia kazi changamoto za eneo husika
 
Nimepita twitter nimekuta maelezo hayo..kipengele 'd' kipo poa sana...we kila siku unaomba taarifa zetu tu hufanyii kazi
 
Ni kama umeweka ka ' automated sms'..jina..namba..eneo etc
 
TANESCO hebu naomba tusaidieni wakazi wa Kimara mwisho.Kuna laini hii inayotoka Ubungo kupitia upande wa Dawasco hadi machinjioni.
Inasumbua sana kukatika umeme.Ninavyoandika hapa umekatwa.Ni kila wiki lazima nije hapa kulalamika nadhani utanizoea maana nina muda mrefu naandika humu lakini tatizo hili haliishi line hii ya dawasco.
Hii ni too much line hii.
Kimara pana line mbili kubwa za umeme.moja inakwenda mpaka Mbezi inapitia upande wa kushoto wa Moro road kama unakwenda Mbezi(upande wenye zile nguzo zenu kubwa za high tension toka kidatu).Nyingine ni line fupi inatokea Ubungo,inapitia kulia kwa moro road inalisha maeneo ya ebonite college,kam college,Mavurunza,Matangini,dawasco,tra,kimara sokoni,mpaka machinjioni inaishia pale.Hii ya pili ndio ina shida ya kukatika umeme sana.Wewe nifuatilie utaona post zangu kila wiki humu miaka na miaka.
Tusidieni jamani wengine tumewekeza huku mnatutia hasara.Tatizo gani hili lisiloosha miaka na miaka au walau kupungua?kiila wiki ni hivi.
 
Ahsante kwa taarifa tunaifanyia kazi.Jm
 
Tanesco mnazingua sana tangu jana hakyuna huduma ya LUKU , ukinunua kwa simu zote inakataa , mara nyingine ikikubali mnaleta Token feki , yaani mmefeli sana , na ule utaratibu wenu wa kusema na kutoa taarifa kama kuna shida kutumia vyombo vya habari hamsemi tena yani mmeboa sana watu wamelala gizani ,usumbufu mkubwa sana mmesababisha. Sidhani kama Kitengo chenu cha Mawasiliano kwa sasa kina fanya kazi zake ipasavyo Tunamkumbuka sana Leila Muhaji, sasahivi tungemsikia kwenye maredio huko anataoa ufafanuzi
 
Changamoto ya kulipia umeme ( LUKU)
Tokea jana mchana nimejaribu weka luku imekataa.. mtandao unaonesha nimeshalipa ila haileti token. Nomejaribu na tigo pia. But nikiweka inakataa. Malalamiko Arusha, Moshono
 
mkuu vp umefanikisha hata mimi inanzingua tu
 
Tangu jana mnaonekana mna shida kwenye kununua luku. Baada ya ucheleweshaji nimepata token. Ila napoingiza umeme hauingii. Je hii itakuwa ni shida gani?

TANESCO
 
Nimepeleka form ya maombi ya kuunganishiwa umeme tangu mwezi wa 8 mwaka 2019 mpaka leo sijapata huduma
 
Tanesco kama kuna shida kwenye mfumo si mseme mbona hatuwezi kununua umeme kwenye mitandao ya simu?
 
Tanesco kama kuna shida kwenye mfumo si mseme mbona hatuwezi kununua umeme kwenye mitandao ya simu?
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUKOSEKANA KWA HUDUMA YA MANUNUZI YA LUKU KWA BAADHI YA WATEJA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawaomba radhi wateja wake kutokana na hitilafu iliyotokea kwenye mfumo wa manunuzi ya umeme wa LUKU siku ya Jumatatu, Mei 17, 2021 na kusababisha baadhi ya wateja kushindwa kununua umeme.

Tunaomba uvumilivu wakati wataalamu wetu wanafanya kazi kuhakikisha tatizo hilo linatatuliwa haraka.

Tutaendelea kutoa taarifa kadri huduma itakavyo kuwa ikirejea.

Tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza

Kituo cha miito ya simu makao makuu +255 222 194 400 na +255 768 985 100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii

Twitter: www.twitter.com/tanescoyetu

Facebook Tanesco Yetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
Mei 18, 2021.
 
Jitahidini mrekebishe haraka , maana mnatukwamisha wateja wenu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…