Tunafanyia kazi tafadhali
TANESCO LINI MTANDAO UTAREJEA? NINA SIKU YA TATU SASA SINA UMEME ,MITA IMETEMPLE NIMETUMIWA NO ZA KU CLEAR KILA NIKIWEKA NAAMBIWA REJECTED(SIKU YA TATUU HII). MAFUNDI WA TANESCO WAMEKUJA WANATOA MAJIBU SIMPLE "SYSTEM IPO CHINI IKIKAA SAWA TUTAKUTUMIA NO ZINGINE UWEKE"[emoji3166]HIYO SYSTEM INARUDISHWA LINI?
 
Hata namba za simu mnazotuwekea hazipokelewi mnaweka za nn sasa
 
Wasi wasi wangu kuna jambo Tanesco wanafanya. Na watakapo rudisha huduma INAWEZEKANA WAKARUDI NA BEI TOFAUTI YA UMEME PER UNIT.

Lazima umeme utapanda bei.
 
Hivi kwanini TANESCO msingetoa taarifa ya kutokuwepo kwa huduma ya luku watu wanunue umeme wa kutosha kuliko kufanya ujinga huu mlioufanya!!?

Au mnamtia hujuma Mama Samia maana hii kitu haijawah kutokea ikachukua muda mrefu namna hii.

Mnachokitafuta mtakipata.😈😈😈
 
Tafadhali tuwekeeni option ya kupunguziana Units. Siku ya tatu Leo sina umeme..samaki wote wabiashara wamechina zaidi ya tani moja.
 
Tunaomba mtueleze tatizo ni nini katika mfumo wa kununua umeme kwa njia ya mtandao naona tatizo hili ni kwa nchi nzima.
Muda huu natoka TANESCO makao makuu ya Mkoa wa MWanza, kompyuta wapo wanachezea game la karata maana mfumo wa kuuza umeme hakuna, asante sana kwa kuihujumu nchi!
 
Ngoja nivute pumzi kwanza ili nipoze hasira....nimepata sehemu ya kuhifadhi vyakula vyangu visioze kwenye friji...(kwa jirani)

Jamani Mama Samia Rais wetu mpendwa, unawategemea watendaji wako ndio wakupe taarifa kuhusu nchi yako eti? Kwa taarifa yako mtangulizi wako alikuwa na informers wengi nje ya system ya kawaida....
 
Kwa hiyo ina maana ni nchi nzima umeme haununuliki waziri mwenye dhamana na shirika amelala usingizi mpaka rais tumekwisha.
 
Kwa hiyo ina maana ni nchi nzima umeme haununuliki waziri mwenye dhamana na shirika amelala usingizi mpaka rais tumekwisha.
Ni nchi nzima mkuu, kama una akiba ya unit kwenye meter yako jitahidi uzime vifaa na taa za ziada maana hakuna anayejua hili tatizo litatatuliwa lini, labda wadukuzi waliodukua bomba la mafuta la huko USA wameelekeza mashambulizi yao Tanzania!
 
Je unaongelea kijiji gani? TAFADHALI tambua huduma ya usambazaji wa umeme maeneo ambayo haujafika inaenda kwa awamu hivyo vijiji ambavyo havijapata vitafikiwa mwa awamu zijazo.Jm
Oya nimeunganisha umeme Direct kwangu

Kama fidia kwa uzembe wenu mkinikamata nitajua naenda vp kujitetea mahakaman

Heko TANESCO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…