HIVI TANESCO KIGOMA KUNA TATIZO GANI
Kwakweli ni jambo la kusikitisha vile nishati ya umeme ni kitendawili katika mkoa huu wa kigoma. Yaani tanesco kama hawajui wanafanya nini. Umeme unawaka nusu nusu mara siku nzima ni giza yaani tabu tupu. Leo tangu asubuhi hakuna umeme na mpaka sasa haujarudi. Huu mkoa upo nyuma sana yaani.
 
TANESCO HABARI Nmefuta bahati mbaya luku token Sijaiingiza naomba msaada namna ya kuirudisha
 
Huo mkoa Kwa ufupi upo nyuma
Kama mfuko wa jins Kwa taasisi
Zote huo mkoa hakuna taasisi
Inayofanya maendeleo

Zaid Tu policcm kuzid kuumiza wananchi
 
Mimi ninaomba msaada,
Hivi ukishalipia control number inachukua muda gani mpaka kufungiwa umeme nyumbani?

Maana nimelipia control number tangu tarehe 2/6/2021 lakini mpaka Leo sijafungiwa umeme.
Nimefuatilia Mara kadhaa lakini majibu yamekuwa hayaniridhishi naambiwa eti mita hazipo., nishafuatilia sana mpaka nimechoka nimeamua nisubir mpaka watakapoamua wao.


Nipo Turiani-Morogoro.
 
Nimehamia mkoa wa Kigoma mwezi wa pili mwaka huu. Mwanzoni umeme ulikuwa haukatiki hovyo hovyo (nadhani sababu ya ukali na utendaji wa Dr. John Pombe Magufuli. R.I.P).

Toka mwanzoni mwa mwezi huu wa nane UMEME UNAKATIKA hakuna mfano.

Tanesco hakuna taarifa yoyote wanayoitoa kwa uma wala hawajali. Umeme unaweza katika siku mbili bila taarifa yoyote. Mfano Jana tarehe 17/8/2021 umeme wamekata saa mbili asubuhi maeneo mengi ya mji na mpaka leo hii tarehe 18/8/2021 baadhi ya maeneo hatujarudishiwa umeme.

Linalotushangaza zaidi hawa TANESCO kutwa kuchwa wanazurura na Landcruiser la emergency mitaani hata hujui ubize huo ni wa nini na umeme hakuna.

Kweli mkoa huu umesahaulika sana sana kwani ukiachilia kwamba umeme ni tatizo kiasi hiki (maana bado kigoma haipo katika gridi ya taifa) hata barabara kuja kigoma bado si lami[emoji848][emoji848].

Tunao tumia umeme kwenye shuhuli zetu za kila siku tunapata hasara sana.

Tanesco kigoma amkeni kidogo, mbona kipindi cha JPM mambo yalikuwa yanaenda? Amkeni mnatuangusha kwakweli.
 
Hili shirika limekuwa la hovyo sana yaani wanatutia hasara mno
 
Hongera Tanesco kwa kuwawekea umeme wote walioomba kuwekewa huku Kisasa-Dodoma.
 
Naitwa Anna George teophili nipo mkoa wa songwe wilaya ya mbozi ni mwezi sasa tokea niombe kufungiwa umeme lkn bado sijapewa control number ili nilipie japo taratibu zote nilizifuata.

Sasa basi inachukua Siku ngapi ili nipate control number nilipie na kufungiwa umeme?
 
Nimebadilishiwa matumizi kutoka matumizi madogo ya uniti chini ya uniti 75 kwenda matumizi ya viwanda vidogo bila kujua sababu wakati matumizi yangu ni ya taa tu.

Nauliza najibiwa kuwa mfumo utajirekebisha wenyewe wakati mwanzo wamenibadilishia kwa kunipa key change.
 
Inakaribia mwezi sasa umeme umekuwa unakatika kila siku, outage time ni ndefu kuliko muda wa uwepo wa umeme, hakuna taarifa kwa wateja, je hii tumerudi kwenye promotion ya majenereta?
 
Kuna transformer imepata shida huko, waziri husika ameshawaagizia nyingine toka Dodoma.
 
Morogoro mwezi huu mwanzoni palitokea ajali ya moto katika substation ya Msamvu.
Hivyo mpaka sasa mnapata umeme kutoka substation ya Chalinze na mafuni wapo kazini kujenga HT kuunga feeder za Kidatu na Kilosa ili Moro mjini mpate umeme wa uhakika.

Mafundi wapo site porini Mikumi huko week ya pili sasa.

Taarifa ninazo toka chanzo chakuaminika.
 
Mbona Waziri aliwapa siku 4 na wakaahidi kurudisha hali ya umeme kuwa sawa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…