Tanesco acheni kuzingua.

Tatizo gani leo tena??
 
uko wapi wewe.
mbona wengine umeme kukatika ni luku kuisha au miundombinu kupata shida na ukipita unawakuta jamaa wako wanashughulikia.
Jieleze vzr, tatizo la kijiji sio lazima liwe la kitaifa.

weka hoja zako vyema, thread inapwaya
 
Wakuu naomba kuuliza na kuwaomba tanesco .maeneo ya kimara Mimi Niko kibo hatuna Umeme tangu Jana je ndio mgao?wa Umeme au kuna tatizo mbona mnatutesa ?tunaingia Siku ya tatu biashara zimesimama vitu vinaharibika usalama unazidi kuwa mdogo hasa kutokana na matukio ya watu wasiojulikana mi naamini kukiwa na mwanga nitawajua...tafadhali turudishieni Umeme....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUTOKEA HITILAFU KATIKA TRANSFORMER LA SIA GARAGE MKOA WA KINONDONI KUSINI

Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) linawataarifa Wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kusini kuwa imetokea hitilafu katika transformer letu la kwa Sia Garage.

Kutokana na hitilafu hiyo baadhi ya maeneo ya kimara kibo na Msewe yanakosa umeme.

HATUA ZILIZOCHUKULIWA
Mafundi wa wanaendelea na kazi ya kutatua tatizo ili kuhakikisha umeme unarejea mapema iwezekanavyo

Kwa mawasiliano: Dawati la dharura Kinondoni Kusini 0784/0715 271461au kituo cha miito ya simu Makao makuu 2194400 au 0768 985100

Mitandao ya Kijamii
Tanesco Yetu,
Tanescoyetu (@tanescoyetu) | Twitter

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

TANESCO Makao Makuu

Huduma kwa Wateja

Simu: 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz

Tovuti:www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii
www.facebook.com/tanescoyetu

www.twitter.com/tanescoyetu

TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO
 
JAMANI NAHUKURU SANA INGAWA MAJIBU YAMENIPA NUSU MATUM,AINI .. ILA NIMEJISIKIA FAHARI KWA RESPONCE YENU THAT'S HOW USASA ULIVYO .. ASANTENI SANA ...sana kwa kutujali wateja wenu tusaidieni basi liishe tatizo usiku mwema ila kwetu bado giza japo tunajua tarizo sasa ngoja tujipange na wasiojulikana kwa uck huu
 
Shukrani sana mpendwa mteja shirika lipo pamoja nawewe

TANESCO Makao Makuu

Huduma kwa Wateja

Simu: 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz

Tovuti:www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii
www.facebook.com/tanescoyetu

www.twitter.com/tanescoyetu

TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO
 
Kwangu mm sina lolote nakumbuka kuna siku umeme ulikatika hom tuliviwpigia walikuja sa 12 asubuhi sikutegemea asee hongeleni sana
 
Ni matumaini yangu humu jukwaani tu wazima na shukrani za pekee zimuendee yeye atupae uzima huu pasipo kulipia chchote...bila kusahau dua sala na maombi yetu kwa TL Mungu amjalie aweze kupona haraka arudi kwenye majukumu yake.

Nijielekeze moja kwa moja kwenye mada kuhusu hii katakata ya umeme bagamoyo mjini bila hata taarifa kwetu sisi walaji.

Kama mnapitaga humu tafadhalini sana hii kitu shughulikieni vinginevyo mnataka kututia hasara ya vyombo vyetu vinavyotumia umeme.

Ni kama wiki ya pili hii nashuhudia hii kitu japo hakitokei kila siku lakini si vyema kukalia kimya. Huwa nakereka ila ya Leo ni too much, hivi ndani ya dakika kumi na tano umeme unakatwa na kurudi Mara tano kweli au kunasoketi huko makao makuu zinajizesha off and on automatically, maana haingii akilini kabisa kama lengo ni kukata mkate hata siku nzima tujue moja ila siyo huo mchezo mnaofanya.

kunamtu humu jukwaaani alishawahi kusema yawezekana kunamtu huwa anaenda na mtoto kazini afu anamuacha anachezea main switch ndo anatupa shida mjini sikuwa najua jamaa aliawaza nini ila kwa mwendo huu unaweza kujikuta unayaamini haya maneno hakyanani, kuweni sirias basi ebooo!!
 
Aaisee huku kwetu Majohe umeme hatuna toka ulipokatika usiku wa jumanne na hatuna taarifa yoyote ile
cc Tanesco kisarawe

mjinga hajijui
 
Bagamoyo eneo gani haswa na namba yako ya simu mpendwa mteja

TANESCO Makao Makuu

Huduma kwa Wateja

Simu: 0768985100/0222194400

Barua pepe: customer.service@tanesco.co.tz

Tovuti:www.tanesco.co.tz

Mitandao ya kijamii
www.facebook.com/tanescoyetu

www.twitter.com/tanescoyetu

TANESCO TUNAYAANGAZA MAISHA YAKO
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…