TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Nimefanya taratibu zote ikiwa pamoja na Kulipia gharama za kufungiwa Umeme lakini mwezi sasa umepita hakuna anayekuja kunifungia Umeme, Nyumba yangu ipo Kinyerezi Kanga, Mtaa wa Kariakoo
 
Nimetoa tarifa hapa zaidi ya wiki tatu kuhusu waya zilizopita kwa ndani ya madrasa huku zikiwa zimeminywa na bati mpaka leo haluna kilichofanyika au mnataka watoto wafe ndiyo mtakwenda?
 
Ndugu mpendwa Mteja wetu

Tunafurahia kukuhudumia kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii, tafadhali onesha taarifa kamili kwa huduma bora.

Jina

Eneo

Wilaya

Namba ya simu

Tatizo

Toka lini

Namba ya taarifa

Ahsante sana

TANESCO Huduma kwa Wateja

SIMU : 0748550000
Inbox
 
Tanesco mkoa wa Kilimanjaro ,Kijiji Cha Shari wilaya ya Hai .kweli wamewakosea Nini haiwezi kuisha week bila umeme kukatika sio masika sio kiangazi .hata saa hii wamekata umeme toka saa 2 asubuhi kurudi Ni majaaliwa .

Hii nimesema kwa kijiji nilichopo ila naamini maeneo mengi ya huku Hali ipo hivyo hivyo
 
Tanesco mkoa wa Kilimanjaro ,Kijiji Cha Shari wilaya ya Hai .kweli wamewakosea Nini haiwezi kuisha week bila umeme kukatika sio masika sio kiangazi .hata saa hii wamekata umeme toka saa 2 asubuhi kurudi Ni majaaliwa .

Hii nimesema kwa kijiji nilichopo ila naamini maeneo mengi ya huku Hali ipo hivyo hivyo
Tunashukuru kwa taarifa tafadhali onesha namba ya simu kwa hatua zaidi
 
Mimi naitwa VALENCE CASSIAN KUNDY
NIPO MOSHI
NILIOMBA KUUNGANISHIWA UMEME TOKA MWEZI WA 8 MWAKA JANA NIKAFANYA SURVEY ILA HADI LEO SIJAPATA CONTROL NUMBER NA KIKA NIKIFIKA OFISINI WANASEMA MTANDAO UPI CHINI SIJUI MTANISAIDIAJE?
0755705925
Lini nitapata control number nikekaa muda mrefu sana bila kupata
 
Tulifika eneo lako mwezi wa Tisa na kugundua kuwa upo umbali wa zaidi ya mita 120 hivyo mpaka tusogese miundombinu ya umeme ndio unaweza kupata huduma, tumepokea taarifa kwa hatua zaidi
 
Namba ya simu uliyoandika kwenye form tako ya maombi ya umeme itatusaidia kuona taarifa zako kwa urahisi
Mwanza kuna Shida Gani toka umeme unakatika asubui unarudi jioni, kama kuna shida si mtutangazie tupange ratiba zetu na kutupiga mgao wa kimya kimya
 
Back
Top Bottom