Habari TANESCO, nimepata tatizo luku iliisha nimeenda kununua narudi kujaza umeme namba za kuandikia kwenye mita hazifanyi kazi, nimewasiliana na nyie kwa namba hii 0748550000 nikapewa usaidizi na kweli mafundi wamefika mpaka nyumbani na wamesema mita inatakiwa kubadilishwa, lakini sijapewa maelekezo ya maana natakiwa kufanya nini niende wapi n.k kwani nashindwa kujaza umeme na token ninayo ni zile mita za ukutani, nilikuwa naomba naweza kuwapa mita namba na token mkaniwekea umeme kwani mpaka sasa ni giza na nashindwa cha kufanya, kwa wakati huu nasubiri huduma nipate umeme? na pia taratibu za kufuata napaswa nianzie wapi na kipi nifanye?