Ni shirika pekee la kutoa huduma ya nishati ya umeme kisheria ndani ya JMT.Shirika hili kiasi fulani kwa upande wangu naoma linajitahidi sana kwa kutoa huduma japo malalamiko kamwe hayawezi kuisha kwani sehemu ya yoyote ile ya kutoa huduma,TANESCO ina changamoto zake, kwa hiyo tuzivumilie tu japo hazitaisha lakini zitapungua sana tu. Ni kweli serikali yetu chini ya jemedari wetu mkuu mheshimiwa SSH inapambana sana kuisadia TANESCO na mashirika mengine ya serikali ili yaweze kutoa huduma kwa watanzania wote.
Changamoto zilizopo kwenye mashirika na idara nyinginezo za serikali ni nyingi sana japo serikali inajitahidi sana tena sana kuzitatua lakini hii ya TANESCO inaonekana ni kubwa sana kwani matokeo yake yanaonekana hata kwa mtoto mdogo.Tatizo kubwa kwa TANESCO yetu ni uchakavu mkubwa wa miundo mbinu ambao husabisha upotevu mkubwa wa umeme pindi unapo zalishwa,kusafirishwa hadi kumfikia mlaji wa mwisho ambaye ni mtumiaji yaani mimi na wewe pamoja na uhujumu mkubwa wa miundo mbinu kama vile wizi wa umeme unaofanywa na baadhi yetu sisi watanzani.
Kwa hiyo tuwe wavumilivu sana tu naamini ipo siku TANESCO YETU ITASIMAMA VIZURI,KWANI SERIKALI YETU SIKIVU INALIFANYIA KAZI JAPO ITACHUKUA MUDA KWANI KAPU KUU LINAJITAHIDI SANA KUHUDUMIA SHUGHULI NYINGI SANA ZA SERIKALI IKIWEMO TANESCO YETU NA KUMBUKA PIA SERIKALI YOYOTE ILE DUNIANI INAENDESHWA NA KODI.EWE MTANZANIA LIPA KODI KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU