Ndugu Mteja!

Zifuatazo ni gharama halisi za kuunganishiwa umeme kuanzia tarehe 5/01/2022

[emoji3578]Gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia moja kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 320,960/=,

[emoji3578] Mteja wa njia moja ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 515,618/=,

[emoji3578]Umbali wa njia moja ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 696,670/=

[emoji3578]Aidha, gharama za kuunganisha umeme mjini ndani ya mita 30 kwa mteja wa njia tatu kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 912,014/=,

[emoji3578] Mteja wa njia tatu ndani ya mita 70 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,249,385/=,

[emoji3578]umbali wa njia tatu ndani ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu ya umeme shilingi 1,639,156/=.

Zingatia

Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/= kama ilivyoelekezwa na EWURA.

NB: Gharama zote zimejumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
 
Wajibu Wenu mnautambua..
 
Mambo yanaendelea kurahisishwa.Bei elekezi ya kuunganishwa umeme vijijini ni shilingi 27,000/= tu.

TANESCO tunaendelea kuangaza maisha yako wewe mtanzania popote pale ulipo, wasiliana nasi sasa tuweze kukuhudumia kwa haraka na kwa bei nafuu ndani ya muda mfupi.

#TupoKazini
 
Uamuzi wa uwekezaji mradi wa Julius Nyerere ni UTHUBUTU makini uliofanywa na taifa. Kongole kwa mafundi wetu na wakandarasi wanaofanya kazi usiku na mchana kuhakikisha malengo yaliyokusudiwa yanakamilika kwa wakati.

#TupoKazini
 
Mlituaminisha baada ya zile siku kumi za maboresho umeme utaimarika ila bora ya ata ilivokuwa

Chang'ombe temeke kila siku umeme unakatwa , leo tokea mchana mpaka mda huu hakuna umeme , mara unarudi ukiwa mdogo
 
Utekelezaji wa mradi wa JNHPP unaendelea kwa Kasi na kukamilika kwake kutaiwezesha nchi kupata umeme wa uhakika, unaotabirika na wa gharama nafuu.

#TupoKazini
 
Ndugu Mteja!



Zingatia

Gharama ya kuunganisha umeme vijijini kwa wateja wa njia moja ni shilingi 27,000/= kama ilivyoelekezwa na EWURA.

NB: Gharama zote zimejumuisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Mkuu, pamoja na majibu mazuri ambayo naamini Watanzania wengi (wateja watarajiwa ) watanufaika nayo. Mimi nipo kwenye jibu la ANGALIZLO: MIMI nipo kijijini, Kati ya mwezi wa 7 na 8, 2019 nimefanyiwa taratibu zote za kupatiwa umeme hadi kuwepo kwenye komputa na kunitaka nikalipie:

Tatizo linaanzia hapo, sipewi control no.; naambiwa nguzo za REA hamna kwa maana ya malipo hayo ya 27000/, aidha wananitaka niandike barua ya kulipia zaidi ya 600,000/- kwa nguzo 2 za TANESCO kama nina haraka, hivi kutoka 2019 hadi leo 2022 ni muda mdogo?

Naombeni mwongozo wenu.
 
Nilichokiona ni kuwa
Marekebieho ya mfumo wa umeme kwa zile siku 10 na ile siku 1 mliyoiongeza ni mabadiliko ya kuboresha ukatikaji wa umeme haswa hapa Dumila
TANESCO turudishieni umeme Dumila
Kweli wameboresha ukataji wa umeme

Aisee hii nchi tuna safari ndefu sana yaani umeme umekua hovyo sana sahivi

Ila dumila ndio kumezidi kwa hovyo kabisa umeme umekua ni nadra sana..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu Ndio mtindo mameneja wa Tanesco wilaya nchi nzima wamekuja nao.

Ulichokiandia hapa ni ukweli kwa AsiliMia 100.
Tanesco inaiweka ccm kwenye eneo gumu sana sana mwaka 2025
 
Huu Ndio mtindo mameneja wa Tanesco wilaya nchi nzima wamekuja nao.
Ulichokiandia hapa ni ukweli kwa AsiliMia 100.
Tanesco inaiweka ccm kwenye eneo gumu sana sana mwaka 2025
Mkuu, kumbe ndivyo ilivyo!!! Mimi nangojea maelekezo ya hawa TANESCO maana hawa naona watanipatia mwongozo sahihi ambao hauna mawaa.
 
Habari? Nimenunua Luku kwenye namba hii 43000423798 ila nikiweka meter haipokei ni nini tatizo,nimepiga simu kwenye sijapokelewa

Mnaweza kuwasiliana na mimi 0625547181
 
Habari? Nimenunua Luku kwenye namba hii 43000423798 ila nikiweka meter haipokei ni nini tatizo,nimepiga simu kwenye sijapokelewa

Mnaweza kuwasiliana na mimi 0625547181
Je ukiweka unapata ujumbe gani ukiweka umeme? Je umepiga simu namba ngapi tafadhali na upo wilaya gani?
 
Tafadhali, kama ambazo tulitoa taarifa hapo awali namba yetu ya huduma kwa wateja kwa sasa ni 0748550000 kwa Mikoa yote ya Dar es Salaam.
Basi tatizo limeisha kuna mtu katupa wazo la kununua kwenye mashine na tumeweka umekubali.

Je kuna limit ya kununua umeme kwenye simu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…