TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tanesco wameweka nguzo mwezi wa 11 lakini cha ajabu mpaka leo hawana wire... umeme tunausikia tu
 
Huku kwetu mitaa ya FFU morombo, baadhi ya nyumba zilikua hazina umeme jana, leo nyumba hizo zina umeme ila nyumba yetu tu ndio haina, mna matatizo gani ninyi na kwa nn mnakua na viburi kiasi hicho? I miss JPM kwa kweli 😢
 
Leo umeme Darumekuwa unakatikatika. Kwa kauli ya Waziri Makamba yawezekana waya zilizo uchi, kituo chao cha Ubungo, zinagusana kwa sababu ya upepo. AIBU ya mwaka
 
Hiki kimekuwa kikundi cha wahuni joto lote hili mnakata umeme kila muda tena usiku
 
Siasa za miundombinu sijui haikuwa inafanyiwa nini wananchi haiwahusu.

Wananchi wanataka nishati ya umeme kwa shughuli za kujiletea maendeleo na kuishi.

Awamu ya 5 wananchi walipata umeme bila mizengwe.

Tunategemea awamu ya 6 tupate umeme bila kukatikakatika tena kwa bei nafuu zaidi.

Maendeleo hayana vyama!
 
Hii mijamaa imekata umeme Na ilipochoka ikaamua irudishe asubuhi hii Na kutufanya tulale Giza Hapa Dumila .

Halafu wanashindwa kuelewa kuwa ninaposema Dumila Hakuna umeme unakuta Na Magole hakuna Hadi Mvomero Hakuna sababu ili umeme uwepo Dumila inabidi kote huko kuwe Na umeme Ila ilivyo mipumbavu eti inakwambia Dumila Ni kubwa taja Eneo
Yaani wanaongea kama wamevimbiwa makande
Pole sana brother

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, pamoja na majibu mazuri ambayo naamini Watanzania wengi (wateja watarajiwa ) watanufaika nayo. Mimi nipo kwenye jibu la ANGALIZLO: MIMI nipo kijijini, Kati ya mwezi wa 7 na 8, 2019 nimefanyiwa taratibu zote za kupatiwa umeme hadi kuwepo kwenye komputa na kunitaka nikalipie: Tatizo linaanzia hapo, sipewi control no.; naambiwa nguzo za REA hamna kwa maana ya malipo hayo ya 27000/, aidha wananitaka niandike barua ya kulipia zaidi ya 600,000/- kwa nguzo 2 za TANESCO kama nina haraka, hivi kutoka 2019 hadi leo 2022 ni muda mdogo? Naombeni mwongozo wenu.
Mkuu TANESCO naomba/nasubili ufafanuzi wenu hoja hii, ni muda sasa
 
Back
Top Bottom