ndugu mteja, asante sna kwa pongezi
tusaidie taarifa zako sahihi kwa ajili ya ufuatiliaji
1. jina kamili
2. namba ya simu
3. eneo lako
 
Ndugu Mteja

Tunashukuru kwa taarifa, Tumezipokea kwa ufatiliaji na hatua zaidi.

TANESCO Huduma kwa Wateja

Makao Makuu

0748550000
MREJESHO

Nashukuru ombi langu limefanyiwa kazi.

Jana, Jumatano, 03/08/2022 mafundi wa Tanesco walifika na kuniunganishia umeme.

Asante sana TANESCO, asante sana Jamii Forums.
 
Watu tumelipia Mita tayari lakin umeme wamefungiwa watu wawili tu eneo zima mwezi wa pili sasa, mkipigiwa simu mnatupiana mpira tu shida nn nyie😡
 
HABARI za kazi ndugu watendakazi wa Tanesco specifically wa Dodoma na Kongwa nina haja ya kujulishwa hili.

Nimefanya application ya kuwekewa umeme pale kwetu kijiji cha Mlali Iyegu na ombi langu kupewa namb 2907220636 , nikiambiwa kuwa Mkandarasi aliyesajiliwa atafika aweke taarifa za wirering na kuwasilisha TANESCO.

Mkandarasi alikamilisha taarifa na kuziwasi
 
Panga hoja yako vizuri hasa mwishoni.
 
Shida yako inafanana na yangu.
Mimi nimefanya application ya kuwekewa umeme kupitia Namba ya kumbukumbu ya malipo 991033634676
Na nimeshalipia ile hela yao.

Wiring na chuma cha kupokelea umeme vipo tayari ila huyo fundi wa kuja kuweka mita hajafika hii wiki sasa.
Nyumba ipo kwamtoro ,wilaya ya chemba.

TANESCO dodoma wana shida.
Ukipiga simu hii 0789844078 ya TANESCO CHEMBA wanakupiga sound hatari.

Sasa sijajua wanataka wapewe hela ndo waje kufunga mita. Hili shirika zuri ila lina watendaji wa ajabu sana huku chini.
 
Tumepokea taarifa kwa hatua zaidi tafadhali
 
Huku kwa Kijiji Cha kisholo tarafa ya vikindu wilayani mkuranga hakuna nguzo hata moja
 
Habari zenu Tanesco,mie mkazi wa Dar ilala,eneo ni mchikichini karibu na soko la Sambusa,tangu jana tarehe 6/7/2022 saa nane mchana hatuna umeme takribani nyumba zaidi ya elfu mbili, namba ya taarifa ni 256648,
Tanesco laiti mngelipata ushindani nyie kama yalivyo makampuni ya simu hakuna mtu ambae angebaki nanyie, mnatulazimisha tu kuwa na nyie, kiukweli yaani ni kero sana kutokuwa na umeme eneo ambalo ni mita chache tupo karibu na Ikulu ya rais, kama sie tulio Dar tunakalishwa ivyo je mtu aliye uko Mtwara inakuwaje.

Mkurugenzi Tanesco Bwana Maharage chande meseji hii ikufikia kero ya umeme imezidi watumishi wa chini yako ni mizigo.
 
Nikonekt Sasa unaweza kupata huduma za TANESCO kupitia Nikonekt APP, Nikonek.tanesco.co.tz au USSD kwa kubofya *152*00# , Nikonekt kilichobora zaidi kutoka TANESCO. Kwa maelezo zaidi tupigie 0748550000

TANESCO Tunayaangaza maisha yako
Hamuangazi maisha ya watu bali mnawaingiza watu gizani.......nimetoa taarifa kwenu tangu tarehe 6/7/2022 namba ya taarifa ni hii 256648,halafu uje hapa uniambie hayo maisha mnayoangaza ni maisha ya watu wa wapi,
 
Ndugu Mteja

Tunashukuru kwa taarifa, Tumezipokea kwa ufatiliaji na hatua zaidi.

TANESCO Huduma kwa Wateja

Makao Makuu

0748550000
 
Ndugu Mteja

Tunashukuru kwa taarifa, Tumezipokea kwa ufatiliaji na hatua zaidi.

TANESCO Huduma kwa Wateja

Makao Makuu

0748550000
Hello!! Umeme kwangu umekata tangu asubuhi lakini kwa majirani upo unawaka. Kwenye remote inanionesha ki emoji che hasira na alama za switch ziko parallel.

Nimepiga simu nimeambiwa mafundi watakuja lakini hofu yangu ni kukosa pesa leo.
 
Hello!! Umeme kwangu umekata tangu asubuhi lakini kwa majirani upo unawaka. Kwenye remote inanionesha ki emoji che hasira na alama za switch ziko parallel. Nimepiga simu nimeambiwa mafundi watakuja lakini hofu yangu ni kukosa pesa leo.
Ndugu mteja,
Tusaidie namba ya taarifa uliopewa baada ya kuripoti kwenyw namba yetu ya kituo cha miito ya simu 0748550000
 
TANESCO mimi ni mkazi wa mwanza wilaya ya nyamagana mtaa wa mwananchi nahudumiwa na kituo chenu cha nyakato.

Tangu tarehe 5 June nimetoa taarifa ya emergency ya nguzo iliyooza na imedondoka, bahati nzuri ipo karibu na mti kwahiyo imeegemea mti ndio maana haijafika chini, namba ya taarifa ni 0707.

Mafundi walikuja tarehe 8 June wakaiangalia angalia then wakaniambia wataibalisha, ila ikipita wiki kama itakua bado hawajaibadilisha niwakumbushe kwa kutoa tena taarifa.

Bahati mbaya kweli wiki ilipita na nguzo haikubadilishwa nikatoa tena taarifa tarehe 18 June, simu alipokea mdada akaniambia taarifa imefika na itafanyiwa kazi.
Tangu siku hiyo sijaona fundi yeyote wa tanesco na nguzo bado inaning'inia.

Tarehe 6 August nikatoa tena taarifa kwenye banda la tanesco nanenane, nikiwa hopo bandani wahudumu walipiga simu kwenye kituo chenu na kuulizia taarifa yangu. Taarifa yangu ilikuepo na taarifa ya mafundi waliokuja kuiangalia nguzo pia ilikuepo, nikaahidiwa tena kwa mara ya tatu kua tatizo litashughulikiwa leoleo.

Hadi nimeamua kupost hapa kwenye thread yenu ni kwamba tatizo halijashughulikiwa na mbaya zaidi nguzo inazidi kuinama. Maybe hadi patokee janga ndio mtaibadilisha.

Ni kitu cha ajabu sana mtu unatoa taarifa ya emergency mara zaidi ya tatu halafu inapita miezi almost miwili bila tatizo kutatuliwa.

Tafadhali TANESCO kuweni wawajibikaji shughulikieni hili swala.
 
Shida yangu ni swala la umeme KUKATIKA na kuwaka kila dakika Moja hasa hasa kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 4 usiku, cha ajabu kwa majirani zangu umeme unawaka mda wote tena ambao wamefungiwa umeme mbele yangu, kama ni shida ya hizi MITA mpya iweje mteja ambae amefungiwa umeme miezi sita baada yangu kwake umeme usikatike na kwangu ukaitke wakati nategemea mita zetu zitakuwa sawa?

Kweli maaeneo yetu inasemekan kuna kuwa na Low voltage kwa mida hiyo lakini kwani kwangu tu? Nawezaje kubadilishiwa aina hii ya MITA? Nawasilisha kwenu TANESCO
 
Umeme KUKATIKA kuanzia saa 12 jioni mpaka saa 4 usiku, kama ni swala la aina ya MITA mbona kwa majirani zangu umeme kwao unawaka Mida hiyo?

Nilijaribu kufatilia TANESCO wakaniambia kuna tatizo la Low voltage maeneo yangu, na aina ya miter yangu inakata umeme pindi umeme unapokua mdogo,sawa mbona kwangu tu na wengingine upo? Na tumipishana within 2 month kuwekewa umeme?

Je kama ni kubadilishiwa aina ya MITA naomba msaada, kwani tatizo hili tangia nimeliripotia ni zaidi ya 6 month hakua mrejeaho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…