Naombeni msaada wa mawazo
Nyumbani kwangu umeme unakata kwa muda lakini kwa majirani upo
Yaani inatokea hivyo mara nyingi na Luku huwa nakua nayo
 
kweli hata kwetu shida hiyo ipo utakuta hapa upo jirani hakuna ni kweli kuna laini ya zamani na mpya halafu hakuna taarifa tupeni taarifa tusipate hasara.
 
Shirika la kisenge kabisa. Hakuna shwaini zaidi ya nyie nchi. hii. Wahuni wstupu.
 
Naombeni msaada wa mawazo
Nyumbani kwangu umeme unakata kwa muda lakini kwa majirani upo
Yaani inatokea hivyo mara nyingi na Luku huwa nakua nayo
Mkuu kama unatumia mita ya vibox vile vya kuwekea umeme wa remote ya ndani ujue ilo tatizo sio kwako bali ni nchi nzima zile mita zinasumbua sana yani tanesco nao wameshindwa kabisa kulitolea ufafanuzi.
 
Mkuu kama unatumia mita ya vibox vile vya kuwekea umeme wa remote ya ndani ujue ilo tatizo sio kwako bali ni nchi nzima zile mita zinasumbua sana yani tanesco nao wameshindwa kabisa kulitolea ufafanuzi.
Ndiyo ninayo itumia kiongozi, mita ndefu yenye kutumia remote, inanipa changamoto sana

Sent from my ANE-LX2 using JamiiForums mobile app
 
Toeni ratiba ya mgao Dodoma sio tunaenda Kibubu tu Mama nchi imeshamshinda
 
Tanesco mna shida gani? Umeme unakatwa kupita kiasi hata kama ni mgao ni hatari, Mfano, Kilimanjaro mmekata umeme asb na mapema, mkarudisha saa 1 Usk , baada ya dk 10 mmekata Tena mpk sasahivi tupo gizani, simu zenu hazipatikani . Je wananchi tufanyeje?

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
TANESCO makao makuu nawaamini sana. Mna nia njema na Maendeleo ya Nchi Hii. Lakini siku zote juhudi zenu zinakwamishwa na watendaji wenu ngazi ya Wilaya.

Ni vyema mkaunda monitoring and Evaluation Team kutoka makao makuu ili kuwawajibisha hao watendaji wenu wa halmashauri.

Nilikaa miaka miwili bila kuwashiwa umeme, waliolipia kabla yangu walipata huduma baada ya kuchanga rushwa. Nilipowasilisha malalamiko makao makuu niliwashiwa umeme ndani ya siku tatu!
 
Salaam. Nimenunua umeme online nikapewa token. Nilipojaribu kuingiza kwenye meta ukawa inaniandikia error77. Hivyo nimeshindwa kuingiza umeme kabisa na mpaka Sasa nipo gizani. Je tatizo ni Nini na nalitatua vipi?
 
Tunaomba Mamlaka husika, TANESCO Yombo kufika Lumo barabara ya Forkland kurekebisha tatizo la umeme kutetema,au kuwaka na kuzima,au low voltage eneo la Lumo mwanzo,kitongoji Cha Forkland ukipata daraja la kwa Mmasai, wilaya ya Tenesco Yombo.Usiku wa leo nyumba nyingi tumelala gizani, wakati haikuwa siku yetu ya mgao na taarifa tulitoa CC 0748550000 na kuahidiwa kuletwa mafundi,Ni matumaini yetu mafundi watafika leo kurekebisha tatizo hili kwa maana usipoziba UFA utajenga ukuta.

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…