TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
TANESCO Huduma kwa wateja, Makao Makuu, tarehe 27Nov 2022 alasiri, wateja wa Lumo, barabara ya Forkland,tumepata kadhia ya kuwa na umeme hafifu-Low voltage na baadhi ya nyumba umeme ume katika kabisa kwa mfano mita 37220069415.Tulitoa taarifa jana saa 1.30 usiku na kuahidiwa kuletewa mafundi, kurekebisha, lakini mpaka hivi sasa mafundi hawajafika eneo la tukio.Au shirika linasubiri mpaka patokee maafa ndiyo Mkurugenzi Mkuu na Waziri mwenye dhamana ya umeme ndiyo muunde tume kuchunguza ajali, miaka 60 ya Uhuru watendaji hawawajibiki,mnataka hata suala hili Rais aingilie Kati.Wahusika wajitafakari.Achane umangimeza

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
 
Arusha it's too much...hebu mtuonee huruma...umeme unakatika mno jamani
 
Salama
Kumekuwa na tatizo sugu la upatikanaji wa umeme huku Arumeru ,Arusha.
Kwa muda mrefu umeme umekuwa ukikatwa kwa masaa mengi sana .Wakati mwingine umeme huja kwa masaa 4 na kukatika tena.Sio usiku sio mchana hakuna umeme huku Arumeru,Arusha.
Tunahitaji kufahamu masaa ya mgao wa umeme,manake kwetu sisi wananchi wa Arumeru ni zaidi ya mgao, ili tuweze kujipanga kwa shughuli zetu.Shughuli zetu za uzdlishaji zinategemea umeme.
Natumaini hili tatizo la ukatikaji umeme kiholela huku Arumeru,Arusha litatafutiwa ufumbuzi.
 
Tanesco mnaharibu uchumi wa nchi kwa sasa
angalia mahotel tote mtaa wa lindi wapo Gizani na wageni wao
si muwaonee watu huruma?
 
Wakuu hivi ukifungiwa umeme

Kwa mara ya1 ukitaka kununua inapaswa ununue wa shingapi
 
Nahitahi kufahamu , kwa sisi tuliopitiwa na line kubwa then tumekosa huduma ya kupata umeme wenu, nini kifanyike kupata huduma ya umeme.
Kibaya zaidi tumelipia na form zenu zile za online , then akatumwa surveyor..alitumwa ametuambia hakuna umeme tutapata.
Ni nini kifanyike hapo?
 
Nipo Ilala Kata ya Pugu, Mita imenigomea kutambua nimebakishwa na units ngapi, lkn nashindwa kuingiza umeme pia. Nikiwasha KISOMA MITA kunakuja maadishi CONNECT FAIL. Nilifika Tanesco Chanika wamenipa namba tarakimu sita niigize zikifatiwa na namba za Mita (nikiwa karibu sana na mita) nimefanya hivyo mara kadhaa bila mafanikio.
Naelekea kulala gizani sasa!
Napaswa kufanyaje?
 
Ndugu tanesco
Je, Ni kweli gharama za kufungiwa umeme zimenipanda?!
Kutoka 321000(bila nguzo)
Mpaka 500000(bila nguzo (?!
 
Ndugu tanesco
Je, Ni kweli gharama za kufungiwa umeme zimenipanda?!
Kutoka 321000(bila nguzo)
Mpaka 500000(bila nguzo (?!
Ndugu Mteja

Tafadhali zingatia kula gharama hizi hazijabadilika toka mwaka 2016

Ahsante sana
 
Nipo Ilala Kata ya Pugu, Mita imenigomea kutambua nimebakishwa na units ngapi, lkn nashindwa kuingiza umeme pia. Nikiwasha KISOMA MITA kunakuja maadishi CONNECT FAIL. Nilifika Tanesco Chanika wamenipa namba tarakimu sita niigize zikifatiwa na namba za Mita (nikiwa karibu sana na mita) nimefanya hivyo mara kadhaa bila mafanikio.
Naelekea kulala gizani sasa!
Napaswa kufanyaje?
Tarakimu nane na siyo sita kama nilivyoeleza mwanzo
 
Back
Top Bottom