Ifikie wakati ushindani uwepo Tanesco mmefeli. Nchi Ina miaka 61, lakini mgawo haukomi. Uchumi utakuaje kwa hali hii, viwanda vitafungwa, ajira zitashuka, mtaani walioishi kwa kutegemea ice cream ndio hivyo. Kwanini hamji na suluhisho, kwani bwawa la Nyerere limeishia wapi?
Au ndio msimu wa biashara ya majenereta ikue, mafuta yauzwe sheli, wanufaike wachache. Jua kali linalowaka nchi hii iliyopo karibu na mstari wa Ikweta, takribani mwaka mzima, hasa ukanda wa pwani, mnashindwa kuvuna jua, yaani Sola, hata angalau usiwe na megawati kubwa kuzalisha viwandani, basi hata mwanga wa taa upatikane, vipimo vifanye kazi hospitalini, miaka itafika 200 ya uhuru tupo hapa hapa.
Na haya mabadiliko ya tabianchi maji duniani ndio yatapungua kabisa, gesi yetu Iko wapi, au ya maonyesho?
Umeme ni huduma muhimu kama ilivyo huduma ya maji, chakula, hivi hamguswi hata kuwa na uzalendo wa ubunifu wa mpango wa muda mrefu na mfupi? Jiji la Dar lango la nchi Giza!
Jua liwakalo dar ingetosha kuwa na centre ya kuvuna jua, kwa kujaza Sola eneo fulani hata kwa ukubwa wa kilomita za mraba kadhaa.
Nchi zinazoendelea kuna wakati maisha duni tunayoishi inakuwa kama ndio utaratibu, kumbe mabadiliko yanawezekana tukiachana na mazoea. Dunia sasa ipo kiteknolojia, umeme ukatwe saa zaidi ya 10 katika Mkoa au mji mmoja madhara yake yamefanyiwa hesabu?
Hii slogan ya Tanesco mnayaangaza maisha, ibadilishwe!