TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Nahitahi kufahamu , kwa sisi tuliopitiwa na line kubwa then tumekosa huduma ya kupata umeme wenu, nini kifanyike kupata huduma ya umeme.
Kibaya zaidi tumelipia na form zenu zile za online , then akatumwa surveyor..alitumwa ametuambia hakuna umeme tutapata.
Ni nini kifanyike hapo?
😀😀😀😀 Huyo survey kweli n hatari
Ameamua kuwapa makavi bila kupapasa
 
Nahitahi kufahamu , kwa sisi tuliopitiwa na line kubwa then tumekosa huduma ya kupata umeme wenu, nini kifanyike kupata huduma ya umeme.
Kibaya zaidi tumelipia na form zenu zile za online , then akatumwa surveyor..alitumwa ametuambia hakuna umeme tutapata.
Ni nini kifanyike hapo?
Ndugu Mteja

Tafadhali tupatie taarifa kamili kwa huduma bora

Jina

Simu

Eneo

Wilaya

Namba ya taarifa

Tatizo

Ahsante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja

SIMU 0748550000
 
Ifikie wakati ushindani uwepo Tanesco mmefeli. Nchi Ina miaka 61, lakini mgawo haukomi. Uchumi utakuaje kwa hali hii, viwanda vitafungwa, ajira zitashuka, mtaani walioishi kwa kutegemea ice cream ndio hivyo. Kwanini hamji na suluhisho, kwani bwawa la Nyerere limeishia wapi?

Au ndio msimu wa biashara ya majenereta ikue, mafuta yauzwe sheli, wanufaike wachache. Jua kali linalowaka nchi hii iliyopo karibu na mstari wa Ikweta, takribani mwaka mzima, hasa ukanda wa pwani, mnashindwa kuvuna jua, yaani Sola, hata angalau usiwe na megawati kubwa kuzalisha viwandani, basi hata mwanga wa taa upatikane, vipimo vifanye kazi hospitalini, miaka itafika 200 ya uhuru tupo hapa hapa.

Na haya mabadiliko ya tabianchi maji duniani ndio yatapungua kabisa, gesi yetu Iko wapi, au ya maonyesho?

Umeme ni huduma muhimu kama ilivyo huduma ya maji, chakula, hivi hamguswi hata kuwa na uzalendo wa ubunifu wa mpango wa muda mrefu na mfupi? Jiji la Dar lango la nchi Giza!

Jua liwakalo dar ingetosha kuwa na centre ya kuvuna jua, kwa kujaza Sola eneo fulani hata kwa ukubwa wa kilomita za mraba kadhaa.

Nchi zinazoendelea kuna wakati maisha duni tunayoishi inakuwa kama ndio utaratibu, kumbe mabadiliko yanawezekana tukiachana na mazoea. Dunia sasa ipo kiteknolojia, umeme ukatwe saa zaidi ya 10 katika Mkoa au mji mmoja madhara yake yamefanyiwa hesabu?

Hii slogan ya Tanesco mnayaangaza maisha, ibadilishwe!
 
TTCL walitesa watu, zamani simu ilikuwa mpaka uwapigie uombe kuongea na Mkoa Fulani, ilipokuja makampuni ya simu, nani anahangaika nao. Watu wapo tgo, voda, zantel, Airtel, lije shirika la kuuza umeme mbadala ndio dawa
 
Miaka 61 ya kujitawala umeme ni shida afadhali Ukraine pamoja na miundo mbinu yao inaharibiwa na Russia ila Mafundi wanarudisha faster ingekuwa kwetu umeme usingerudi miaka 6
 
TANESCO hamna mnachofanya
Angalau miaka 5 iliyopita kuliko mnavyofanya hivi sasa
Umeme wa mgao kila baada ya siku mbili

Shirika kubwa halina ubunifu, miaka 61 ya uhuru bado umeme wa mgao
Basi bora mtangaze leo tutakata watu tuchaji simu

Mpaka siku ya uhuru mnakata umeme bila aibu
 
tatizo kubwa ndani ya TANESCO kuna vidudu mtu wengi na hao ndio wanao hujumu Shirika.

wapo baadhi ya watendaji katika shirika wanahujumu kwa maksudi jitihada za Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika.

kuna miungu watu wachache ambao wanatakiwa wasafishwe kabisaaa, waziri aliyepo kajitahidi sana kusafisha lakini bado baadhi wapo.
kuna wahujumu wa mali za shirika, kuna wahibifu wa miradi yaani wapiga dili ndani ya shirika.

watumishi/watendaji wa TANESCO nchini tafadhali badilikeni, kuweni wazalendo kwa taifa lenu.
 
tatizo kubwa ndani ya TANESCO kuna vidudu mtu wengi na hao ndio wanao hujumu Shirika.

wapo baadhi ya watendaji katika shirika wanahujumu kwa maksudi jitihada za Serikali katika kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika.

kuna miungu watu wachache ambao wanatakiwa wasafishwe kabisaaa, waziri aliyepo kajitahidi sana kusafisha lakini bado baadhi wapo.
kuna wahujumu wa mali za shirika, kuna wahibifu wa miradi yaani wapiga dili ndani ya shirika.

watumishi/watendaji wa TANESCO nchini tafadhali badilikeni, kuweni wazalendo kwa taifa lenu.
Ndugu Mteja

Tafadhali tupatie taarifa kamili kwa huduma bora

Jina

Simu

Eneo

Wilaya

Namba ya taarifa

Tatizo

Ahsante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja

SIMU 0748550000
 
Nimejichanga kwa maumivu makali sana nikaunga umeme wa njia tatu ili niweze kuvuta maji toka duarani mimi ni mchimbaji nipo kahama eneo linaitwa mwime lakini cha ajab kabsa mgao ni mkali sana na ukija unakuja single yaan hauna msaada wowote zaid ya kuunguza pamp kila wakati hili shirika bora lifutwe tujue moja tuu
 
Umeme WA 5k ni unit 8 wazee alafu hata makato apo hayaelewek

Name:TANESCO
MeterNo:
Receipt:
Units: 8.4
Token: 9056 8882 3947
Amount:TSh 2459.02
Tax: VAT 18% TSH 442.62 EWURA 1% TSH 24.59 REA 3% TSH 73.77 Total Tsh 5000.
Ref: EC101599108039
2022-12-10 19:04:21
 
Tafadhali onesha namba ya mita kwa maelezo zaidi
 
Nipo mkoa wa kagera, bukoba mjini, kata kitendaguro, mtaa kagemu, kuna tatizo gani maana hapa nyumbani fridge guard haiwaki inaonyesha taa nyekundu tu.. ikiashiria power surge tafadhali toeni msaada maana bidhaa kwenye freezer zinaharibika,..
 
Jamaa waje kurekebisha fridge
 
Jamaa waje kurekebisha fridge
Mkuu fridge haina shida ni umeme wao ndo unasababisha fridge guard kujikata yaan kudisconnect fridge na mains... sijui kama umeelewa....au to make it clear kuna power surges ambazo likely zinaanzia power station...
 
Nipo DODOMA sehemu inaitwa KIBAIGWA Nimeomba kuunganishiwa umeme baada ya mradi wa REA kukamilika na kuwashwa katika eneo langu miezi 3 iliyopita nimejaza fomu NiKonect imepitishwa na mkandarasi surveyor akaja akasema natakiwa nguzo mbili nikamwambia nipo tayari kulipa izo gharama nipewe control number akasema sio leo wala kesho kupata control number mpaka mradi utakapokabidhiwa Tanesco nikamuuliza lini akasema hajui mkataba ukoje lkn inaweza kuchukua mwaka mzima NIMESIKITISHWA SANA NA HIZI TARATIBU ZA KIZAMANI. MTEJA NIPO TAYARI KULIPA GHARAMA YA NGUZO ZINIFATE NIUNGANISHIWE UMEME NAAMBIWA NIKAE MWAKA MZIMA KUSUBIRI.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom