Naishi kimaraTanesco tanesco nimeshindwa kuwaelewa,,,au mnataka pesa?ni week ya pili sasa tangu waisimike nguzo kwaajili ya kunivutia umeme lkn hawajaniunganishia mini tatizo au niwape pesa?
Heri wewe mwezi sisi mwaka sasa.Tanesco tanesco nimeshindwa kuwaelewa,,,au mnataka pesa?ni week ya pili sasa tangu waisimike nguzo kwaajili ya kunivutia umeme lkn hawajaniunganishia mini tatizo au niwape pesa?
Mkuu tunaomba radhi kwa hili, tatizo lako linashughulikiwa mara mojaTANESCO mnasikitisha katika kutoa kipa umbele kwenye matatizo yanaporipotiwa. Nimekuwa mhanga wa kutoshughulikiwa tatizo langu mbali ya kutoa kwangu taarifa zaidi ya mwaka na nusu sasa.
Katika chuma ya juu ya paa langu la nyumba linalopokea umeme kuingiza ndani kuna loose connection. Hii inapelekea kila pakitisika kidogo na upepo umeme hukatika ama cheche kutoka. Zaidi ya mwaka na nusu nimetoa taarifa katika ofisi za wilaya ya Ilala pasi kupata msaada wowote.
Mimi sio fundi lakini nina hakika si jambo kubwa kurekebisha ila limekuwa na uzito tu katika kutekeleza. Kuna mpaka mmoja wa vijana wa TANESCO alidiriki kunambia nitoe kitu kidogo ili tatizo langu lishughulikiwe. Sasa nashangaa kidogo hicho nikitoe vipi katika jambo ambalo kila siku mnaimba kuwa ni bure.
Mita namba yangu ni 22132264494.
Mtaa Kilosa No. 6, Ilala Dar es Salaam.
0715 286 322.
Tunaomba mita namba na namba yako ya simu tafadhaliNipo Tabata dampo mkoa wa Dar es salaam wilaya ya ilala
matumizi yangu ya umeme wastan kwa siku moja ni unity 1
Kwa mwezi ni unity 30
Sijawahi kufikisha hata unity 35 kwa mwezi tokea nimeanza kutumia umeme wa mita ya Luku huu sasa ni mwaka wa 2
TANESCO mnasema ukiwa huko chini ya unity 75 nenda ofisi ukaandike barua ya kubadilishiwa Tarif kutoka Tarif 1 kwenda tarif 4 kama ukikidhi vigezo utabadilishiwa
mimi nilikwenda ofisi za TANESCO Tabata Liwiti nikaandika barua ,mara ya kwanza meneja aligoma kupokea barua yangu alisema barua za maombi zipo nyingi sana
Nilitumia akili ya ziada nikaingia ofisi nikawasilisha maombi yangu
Yule mdada pale ofisini sijui alinizuga ,nimeona kabisa kawasha computer akaniambia swala lako tunalifanyia kazi
Tangu siku ile ni kimya kabisa mbaka nimekata tamaa
Kifupi swala la kubadilisha tarif kwa wale tunaotumia umeme chini ya unity 75 ni kizungu Mkuti ukisoma humu maneno yao watu wa TANESCO ni ya kukupa matumaini ila usithubutu kwenda ofisini kwao kulalamikia hili utapigwa sound tu,
Utekelezaji wake ni mgumu sana kwa sababu wao wanafanya biashara ya kutudhulumu sisi wananchi
Ukiwa tarif 4 sh elfu 10 ni unity 70 wakati ukiwa tarif 1 sh elfu 10 ni unity 28 unafikiri TANESCO watakubari kubadilisha tarif ili wapate hasara
Nawasilisha.
Inaruhusiwa bila tatizo, unafika ofisi ya tegeta na kupewa maelezo pamoja na fomu.TANESCO habari, Mimi ni mkazi wa wazo ninatumia umeme wa Tanesco nilikua nahitaji kufunga mita ya pili kwenye nyumba yangu, je narusiwa kufanya ivo? naomba utaratibu kama inawezekana.
Mku hicho kifaa kabala sijahamia kwangu kilikuwa shida maana wapangaji waliokimbia umande hawaelewi kitu wao wanaona umechezea. Na lazima pia uchangie. Mikataba ya wenye nyumba pia ni kero. Inasema huduma za umeme na maji zitachangiwa.kunakifaa cha kuonesha wewe unatumia umeme wa kiasi gani ili ulipe kutokana na unavyotumia waulize tanesco vizuri