TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Utaratibu wa vijijin mtu unanuua umeme 5,000 unapata units sawa na mtu wa mjini....
Hili limekaaje?
 
Tangu asubuhi huku maeneo ya ngaramtoni Arusha hakuna umeme mpaka muda huu saa tatu kasoro, kwanini mnatutesa hivyo? Kazi zetu zinategemea umeme, mnataka tuishi vipi? 😳 TANESCO
 
Mimi naomba kutoa pongezi kwa Tanesco hapa Dodoma mjini. Ni Mara kadhaa zaidi ya Mara 5 kwa nyakati tofauti nilipiga simu customer service kwa ajili ya huduma za emergency. Kweli kabisa nilipata huduma ndani ya dakika 45- 120 Tanesco emergency walikuwa wameshafika eneo la tukio physically na kunipatia msaada. Kongole Sana Tanesco Dodoma Mjini TANESCO
 
Ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi, tunashukuru kwa pongezi. Tanesco tunaangaza maisha
 
Tangu asubuhi huku maeneo ya ngaramtoni Arusha hakuna umeme mpaka muda huu saa tatu kasoro, kwanini mnatutesa hivyo? Kazi zetu zinategemea umeme, mnataka tuishi vipi? 😳 TANESCO
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto, tumepokea taarifa za hitilafu ya miundombinu maeneo hayo, tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, wataalamu wetu wanafanya jitihada katika zoezi hilo matengenezo yatakapokamilika huduma itarejea.^EB
 
Hapa Shinyanga umeme umezimwa tangu asubuhi ya saa mbili ..nini kima endelea ?
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana na TANESCO huduma kwa wateja na pole kwa changamoto, tumepokea taarifa za hitilafu ya miundombinu maeneo hayo, tunaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza, wataalamu wetu wanafanya jitihada katika zoezi hilo matengenezo yatakapokamilika huduma itarejea.^EB
Hiyo hitilafu inaisha lini? 😳
 
Ushauri wa kizalendo shirika la tanesco lingizwe ktk ushindani wa biashara libaki na Kuza umeme na kukusanya mapato kodi serikali tu idara zingine kuzivunja ziende ktk sekta binafsi wakandalasi wasambaze umeme na matengenezo na kuza vifaa vya ujenzi wa line na meter kuzwa madukan na kusajir kama line sm ilo litaongeza wigo wa wateja na mapato kwa masilai ya umma na nchi yenyewe pia
 
@TANESCO naombeni msaada WA hiyo
Habari ya wakati huu ndugu mteja, maombi yako no 240823-2058 na 230723-1152, bado hayaja kamilisha hatua za awali, za kuamabatanisha mchoro wa wiring, hivyo mpatie mkandarasi wako ajaze taarifa muhimu pamoja na kuambatanisha mchoro wa nyumba yako kwenye mfumo ^EB
 
Naona limekuwa ni suala au jambo sugu la kukatika Umeme kila siku mikoani tena bila taarifa ,Wanajamvi tuhamasishane lini na mkoa upi Umeme utakatwa kwa hapa Mbeya saizi wameshakata Umeme ilihali hakuna taarifa na mkate wa siku unategemea Umeme uwepo
 
Huu umeme mliokata Leo hapa Iringa mtasema ni hitilafu gani imetokea??

Kwani nani anawakataza kusema kuwa kuna Mgao wa umeme nchini?

Kila mkikata umeme mnadai ni hitilafu mara eti mnafanya matayarisho ya kupokea umeme toka bwawa la Nyerere.

Kuweni wawazi na wakweli.
 
Back
Top Bottom