Kuna Mtaalam wa kukata Umeme na kuna yule Engineer Gwiji wa Disco lights anapiga zima washa zima washa kama ishirini hivi ndani ya nusu saa, akihakikisha kuna TV, Fridge na vifaa kadhaa vya wapiga kura vimeungua hapo anapumzika na kuendelea na report za kuonesha maeneo yatayoathirika na katizo la Umeme kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wao na anamalizia kwa kuomba radhi kwny tangazo huku akicheeeeka

halafu anam cc tangazo Brother Rugemalila

Sent from my SM-G9500 using JamiiForums mobile app
 
Hivi Tanesco ni lini mtaona Raha mkifanya kazi kwa weledi? Ratiba ya mgao hamtoi mnakata umeme mnavyojisikia nyie. Kwa nini hamuwi wazalenda kwa kuitumikia nchi yenu ipasavyo? Kutoa tu taarifa ya ratiba ni issue,Kitengo cha taarifa kinafanya nini? Mfano wiki hii maeneo mengi ya Dar mmekata umeme bila taarifa, hili shirika mnakera sana.
 
Mjomba angu ameshalipia nguzo ipo ila kwenye kumuunganishia imekua shida, Wakati Kuna jirani yake kalipia Mbele yake baada ya siku moja kaunganishiwa fasta kuweni Fair.
Mwenyewe kajiongeza[emoji23][emoji23]
 
TANESCO sina umeme leo siku ya tatu nyumba ipo Kihonda Azimio no#910 mtaa wa msimamo. Morogoro TB 4993703 nililipoti kwa namba 0652612531. Fundi anasema rilei imefunga au kufinguka
 
Nimesoma malalamiko mbalimbali ya wateja wa UMEME! mm pia nikapata mstuko na kujaribu kufuatilia! Lkn pia nikasikia majibu yenu juu ya KILICHOITWA - unit za umeme kuisha kwa HARAKA -

Hii hali imetokea hivi karibuni, majibu yenu yalikuwa " hali hiyo inatokea kipindi hiki kwa kuwa wananchi wengi msimu huu wapo MAJUMBANI.

NILINUNUA umeme tarehe 19/12/2023 kwa tsh 20,000/= nikapata unit 51.9 KWH .matumizi ya hapa nyumbani ni
1 - rice cooker
2- pasi ( mara mojamoja jumapili)
3- feni vyumba 2 usiku kucha na mchana .
4- fridge
5- taa za kwenye ukuta ( fensi)
6- Tv
Umeme huu ulidumu siku 8.

Tarehe 27/12/2023 saa 20:32nilinunua tena umeme kwa tsh 20,000/= nikapata unit 42.1KWH

Matumizi yangu yamezidi kidogo kwani nimeongeza FENI jingine hivyo feni ziko 3 zinazokesha.

Fridge nilikuwa nalizima wakati wa mchana sababu ya joto kali lkn hivi sasa linafanya kazi muda WOTE.

Matumizi mengine yamebaki kama kawaida. Leo ni siku ya 10 umeme bado upo.

Tarehe hiyo hiyo 27/12/2023 saa 19:58 nilinunua umeme kwa tsh 20,000/= nikapata unit 56.1 KWH ( huu niliponunua sikuuona nilidhani umeshindikana nimeuona leo kwenye simu)

Kwanini 20 , 000/= unit 51.9 KWH
Kwanini 20 ,000/= unit 56.1 KWH

Iweje 51.9 unit Zitumike siku 8
Halafu 42.1 unit zitumike zaidi ya siku 10

NAWASILISHA
 
Habari za muda huu wana Jamii,

Kuna baadhi ya vitu sivielewi kuhusu hawa TANESCO

1) Mtu unapohitaji huduma ya umeme unatakiwa kununua nguzo?

kwa sababu nikiangalia katika kijiji changu cha NAIBILI (Kilimanjaro wilaya ya Siha) mwananchi anatozwa shilingi 200000(laki mbili ) kununua nguzo , nje ya hapo kuna gharama nyinginezo kama 27000 kwa ajili ya mita bado kuna 30000 kwa ajili ya mkaguzi anayekuja kukagua nyumba yako kama inafaa kuvutiwa umeme.
kwa mantiki hiyo mwananchi anatakiwa alipie zaidi ya Tshs 250000.

Naomba mnieleweshe kama ni halali kwa mwananchi kununua nguzo ili nisije nikajichanganya.

Asanteni.

Naomba kuwasilisha.
 
Mnachukua mda gani mpaka mje kufunga Umeme kwa MTEJA haiwezekani hela ya mteja ikae week mbili kwenu huduma hajapata
Hiyo hela angefanya Jambo lingnevsi angepata faida hata sent 100
Week 2 unalalamika na uko seriously kabisa?? Na waliokaa mwaka j
e??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…