Kule kwenye SGR umeme ulipokosekana ama hitilafu ilipotokea na treni ikasimama for 2hrs Tanesco mlihusika ama lilikuwa ni suala la ndani la TRC?
 
Nina tatizo la kuingiza units kwenye meter 430128541712
 
Habari,
Nimenunua umeme lakini kila niingiza sipati umeme sijajua shida nini?
 
TANESCO mje mumsaidie mteja wenu huku.

Lakini mkae mkjiua huu ujinga wenu wa kuturudisha analogia kwa kutuletea tokens tatu kuingiza kwenye mita moja kwa wakati mmoja wengi hatuupendi.
 
Habari,
Nimenunua umeme lakini kila niingiza sipati umeme sijajua shida nini?
Ongeza hela unayoweka hiyo haitoshi yaani hapo una madeni sirikali ya mama kizimkazi inataka kupita nayo.
 
TANESCO kila nikijaribu kupiga simu kwa msaada zaidi haipokelewi.
Mkuu hizo token em jaribu kuziingiza kwa mfuatano kuanzia ya kwanza mpaka ya tatu,ingiza ya kwanza bofya kidude cha kukubali ↩️ ya pili hivyo hivyo mpaka ya tatu uone matokeo yake.

Hawa watu ni wa hovyo nchi hii huwezi kupiga simu shirika la umma kutaka msaada ikapokelewa.
 
Shukrani mkuu, kuna namba nimepata nimepiga nimepata maelezo na nimefanikiwa kuiingiza.

Ahsante sana kwa kujali.
 
Tanesco chanika ilala
Mbona hamjanitumia control number mpaka Leo na nimefanya wirering na surveyor amekuja sasa ni mwezi shida nini?
0766786620
 
OMBI LA MSAADA WA TATIZO SUGU LA UMEME NYUMBANI KWANGU

Umeme umeshapungua nguvu na umesababisha matatizo yafuatayo

1.0 KUHUSIANA NA TV

TV imepoteza video signal moja kwa moja, ikabakiza sauti tu


Hapo kabla, video signal ilikuwa inapotea na kurudi tena mara kwa mara ila kwa sasa imepotea kimoja

2.0 KUHUSIANA NA REDIO KUBWA

Signal ya radio kubwa ilikuwa ina-flucutate, mara sauti inakuwa chini sana na wakati mwingine inakuwa juu sana na KWA VOLUME ILE ILE, yaani pasipo kubadilisha volume

Kwa sasa umeme umepungua kiasi kwamba umeme huo hauwezi tena kui-power radio kubwa na hivyo haiwezi kuwaka kabisa; huku wakati huo huo umeme huo unawasha jiko la umeme japo si kwa nguvu ile ya awali

3.0 KUHUSIANA NA ICHARGING YA PAD SMATRPHONES

Wakati mwingine, IPAD Smartphone inaweza kuchaji usiku mzima pasipo kujaa, ila kwa umeme wa mwingine kama vile wa ofisini inachaji muda mfupi tu na kujaa

Kwa umeme wa nyumbani, wakati mwingine inaweza ikafukia hatua hadi ukalazimika kuitumia IPAD ikiwa iko kwenye charger, lakini baadaye IPADA iliyo kwenye chaji itaisha chaji na kuzima kabisa, kitu ambacho si cha kawaida

Kwa umeme wa ofisini, IPAD iko kawaida

4.0 KUHUSIANA NAPLATES ZA JIKO LA KUBWA LA UMEME

Plates za jiko hili huwa zinaongezeka umeme na kupungua na kwa sasa, karibia zote zimepungua nguvu na zinatumia muda mrefeu mno kuivisha chakula

Mara ya mwisho mojawapo ya plates hizi iliongezeka umeme baada ya kuwa ulipungua, ilikuwa ni kwenye kipindi cha Julai- Septemba 2022, mwaka juzi

Kabla ya kipindi hicho, plate hii ilikuwa imepungua nguvu na nguvu hiyo ilikuja kurudi kawaida tena kwenye kipindi hicho tajwa, na baada ya hapo plate hiyo iliupungua tena nguvu hadi leo

Kabla ya plates hizi kupungua nguvu, kuna irreugularity iliyokuwa inatokea kwenye plates nne za jiko hilo kwamba plate hii leo inaweza kuwa ina nguvu ya kawaida na nyingine ikawa ina nguvu pungufu

5.0 KUHUSIANA NA MICROWAVE OVEN

Kwa experience aliyonayo mhusika, chakula alichokuwa anaweza kukichemsha kwa kutumia dakika 3 kabla umeme haujapungua nguvu, kwa sasa anaweza kukichemsha kwa kutumia angalau dakika 15

MATATIZO AMBAYO MARA YA MWISHO TANESCO WALIWAHI KUFIKA NYUMBANI PHYSIVCALLY NA KUYATATUTA

Miaka kadhaa iliyopita, TANESCO waliwahi kuja hadi nyumbani kwangu wakarekebisha kwenye transforma iliyo jirani kpembezoni mwa barabara

Kwa wakati huo, jiko lilikuwa na nguvu ya kawaida na lilikuwa linafanya kazi kawaida, wakati MICROWAVE OVEN ilikuwa haipati umeme ilhali ilikuwa ni nzima

Pasi pia pamoja na machine ya kunyolea ndevu navyo pia vilikuwa havipati umeme wa kutosha na walivirekebisha

Kwa hiyo evidence zote za nyuma zinaonyesha umeme ndiyo umekuwa ukipungua nguvu, huku vifaa vikliwa ni vizima

Mbali na hayo, mteja wa taarifa hizi amesoma pia Physics hadi kwenye level ya degree ya kwanza na hivyo angalau anaelewa BASICS zote za umeme na hivyo ana uhakika kabisa kuwa vifaa vyake ni vizima ila tatizo liko kwenye umeme unaoingia kwenye nyumba yake

Natanguliza shukrani zangu

Contact details zipo kwenye PM message ya akaunti hii ya TANESCO
 

Hii Kila sehemu imekuwa ni changamoto Sana ishu ya upungufu wa umeme kwa kawaida standard voltage ya umeme wa majumbani ni 220V Hadi 240V lakini saiz Kuna muda remote ukiiuliza umeme unaoingia ndani inasoma mpaka 170V kitu umeme ambao hauwezi kuorerate vifaa vya umeme kiufasaha
 
Hapana. Kwenye ghorofa moja tumekuwa tukiishi familia 6 na wengine wote hawajawahi kupata tatizo hili hata mara moja isipokuwa mimi. Vifaa vyao vimekuwa viki-operate kama kawaida siku zote, isipokuwa mimi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…