Kibaga serikali ya mtaa,Nyumba namba 90 ,Kinyerezi,Wilaya ya Ilala,Dar es salaam,tulitoa taarifa ya tatizo la mita ,hatuwezi kuingiza umeme.TANESCO Tafadhali naomba mfike kutuondolea hili tatizo.Mita no.24319752218 imefungiwa.
 
Tanesco imebadili jina na kuitwa Watafuta Miradi ya Kujitathimini maisha
 
Kibaga serikali ya mtaa,Nyumba namba 90 ,Kinyerezi,Wilaya ya Ilala,Dar es salaam,tulitoa taarifa ya tatizo la mita ,hatuwezi kuingiza umeme.TANESCO Tafadhali naomba mfike kutuondolea hili tatizo.Mita no.24319752218 imefungiwa.
Habari Jackal, asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto, tafadhali tupatie namba ya taarifa kwa msaada zaidi. ^GK
 
Baada ya GK kuimba nitakufaje zamu yetu kuimba Watakufaje😂😂😂
 
Kuna tatizo la umeme kukatika katika Shinyanga lakini hakuna taarifa yoyote ni kwa nini!
Inakera sana kuona tatizo lipo muda mrefu lakini linajirudia rudia na halitatuliwi

Meneja unaendesha shirika kizamani sana.Kuna njia nyingi za bure kutoa taarifa lakini hazitumiki. Je ni kiburi kwa vile huna mbadala au ni nini?
 
Habari Cashman, asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto, tafadhali tufahamishe kama bado mnakosa huduma ya umeme kwa msaada zaidi. ^GK
 
Habari Cashman, asante kwa kuwasiliana nasi na pole kwa changamoto, tafadhali tufahamishe kama bado mnakosa huduma ya umeme kwa msaada zaidi. ^GK
Bado hadi sasa hakuna umeme.
Nadhani sio muhimu sana kwa meneja kwa vile tunaopata changamoto hii ni baadhi ya nyumba.Leo siku ya 3 bado hakuna suluhisho
 
 
Application ya Nikonnekt haifanyi kazi kwa Simu za ios tangu jumamosi. Jaribuni kuchunguza hilo.
 
Asante kwa taarifa nzuri sana,mimi shida yangu ni matumizi ya umeme,maana natumia uniti kati ya 9 au 10 kwa siku wakati ni matumizi ya nyumbani tu na sina biashara yoyote nayofanya,je yawezekana kuna tatizo?
 
Ila TANESCO mna dharau sana na wateja wenu, yaani leo ni siku ya inne nimetoa ripoti ya dharura na haijafanyiwa wala haifanyiwi kazi?
Hivi kweli mnajiatambua?
 
Sasa ya nini kudanganya wanainchi na namba za dharura? Yaani mnaboa sana, ni bora sasa tuungane kuwatoa madarakani hamna namna nyingine
#Kwapamojatutaweza
 
Leo tarehe 18/12/2024 mlikata umeme ucku wa manane then mmekuja kukata saa 3 asubuhi lkn Hadi muda huu wa saa 6 mchana umeme haujarudi tatizo nn?
 
Leo ni siku ya tano natoa ripoti ya dharura na TANESCO hawajaja na kila nikipiga simu naambiwa wapo njiani

Bora magufuli aje upya tu
 
Hili shirika toka kifo cha hayati Magufuli na kuondolewa Mh. Kalemani wiazara ya nishati, limekuwa ni shirika la hovyo sana na watumishi wake wananuka rushwa. Yaani nakumbuka tulimuunganishia bibi umeme kwa 27k ndani ya muda wa mwezi mradi wa nguzo 10 kutoka ulipoishia umeme mwaka 2019.

Ila sasa mwaka 2024 mteja upo maeneo ya Morogoro Manispaa kabisa, mtu unaomba kuungiwa umeme umbali wa nguzo tatu (3) tena hapo moja ni ya kwenye kona. Surveyor amekuja toka mwezi wa kumi mwishoni ila mpaka muda huu control number haitumwi. Ukifuatilia ofisini wanakupa majibu rahisi tu, kuwa kuna shida ya mtandao, mpaka wiki ijayo utakuwa umetumiwa control number ila tarehe 23 ya mwezi December ntakuwa nauanza mwezi wa 3 toka surveyor aje site.

Ila ukitoka nje ya ofisi unakutana na vishoka wanakushauri ati umuone surveyor kwa chochote ili mambo yaende. Sasa kama kuna shida ya mtandao namuona surveyor ili iweje? Siko tayari kutoa rushwa wala fedha ya aina yeyote nje ya malipo halali maana umeme siungiwi kwa hisani, nalipia kila kitu kuanzia nguzo, nyaya nk. Tunakoelekea kuna mtu atapewa pesa ya moto ili iwe ubaya ubwela.
 
Naomba muachane na sheria za kikoloni ama ujima.
Mfano umeme kufika kwangu nguzo tano zinahitajika,uwezo wa kulipia nguzo tano ninao ila naambiwa hairuhusiwi kulipia nguzo tano zote ball mbili,halafu hizi tatu tutaandikia mradi.
Ni mwaka sasa umekata nimechoka kufatilia.
Nifanyeje?.
Au mliambiwa umeme ni kwa watu wachache?.
Mambo mengine mnazingua
 
Niwape maua yenu tu, ukipiga simu huduma Kwa wateja unahudumiwa vzr sana,
Big up
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…