TANESCO makao makuu mnafanya kazi moja nzuri sana humu,
Mimi baada ya kufanikisha mambo yangu kupitia ukurasa huu
Nimewaleta humu jamaa zangu wengi sana
Na ninayo furaha kusema na wao wamesikilizwa na kero zao zimeanza kufanyiwa kazi
Ushauri wangu kwenu,
TANESCO hivi sasa anzeni kuwaondosha wafanyakazi wanaofanya kazi kwa mazoea hawa ndio wanaotufanya sisi au wateja wenu kwa ujumla tukimbilie humu kuja kutoa kero zetu
Ila nyuma yetu wapo watanzania wengi sana wana kero zao nyingi sana na awana pa kukimbilia
Awana smartphone awajui namna ya kujiunga JF
Ombi langu
Nendeni mkapeleke huduma kama hii facebook au Twitter
Angalau muwe mnatatua kero kupitia hizo kurasa za FB na twitter kwa wiki mara 2
Binafsi kiongozi aliyebuni ukurasa huu wa kero nampa hongera sana kwa ubunifu huu
Shirika la TANESCO hivi sasa linapata heshima kubwa kupitia uzi huu.
Aksanteni sana.