Asante Mteja,
Kunamaboresho ya Miundombinu yanayoendelea maeneo ya Kigamboni.
Pia kunaujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme.
Maboresho yakikamilika yataondoa tatizo la kukatika kwa umeme ama umeme kuwa mdogo
Lakini pia huwa tunajitahidi katika kutoa taarifa , mfano hii hapa tulitangaza
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA UMEMEMKOA WA TEMEKE
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Temeke kuwa kutakuwa na kazi ya maboresho ya miundombinu ya umeme kwa kufanya kazi ya kubadilisha nguzo zilizooza, kuimarisha viungio vya umeme na kukata miti inayogusa njia za kusambaza umeme, iliyolenga kuimarisha ubora na upatikanaji wa umeme Siku ya Jumanne, tarehe 24 Octoba,2017 kuanzia saa 03.00 Asubuhi hadi saa 12.00 jioni
Kutokana na matengenezo hayo baadhi ya maeneo yatakosa umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA
Kigamboni yote
Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:
Dawati la dharura Mkoa wa Temeke 0714485488, 0783360411, 0765654767 au
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400/0768 985 100.
Tovuti:
www.tanesco.co.tz
Mitandao ya kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu
Barua pepe:
customer.service@tanesco.co.tz
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano kwa wateja
TANESCO-TEMEKE