TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Tanesco mnakera sana jana usiku tumelala bila umeme na leo tunalala bila umeme
 
Mimi naulizia LUKU jioni hii ni vp? Najaribu kununua umeme naona naambiwa "muamala wangu haujakamilika, nijaribu baadae" Hiyo baadae sijui ni saa ngapi na umeme unaisha??!
 
Nauliza Mita Imetoa Kikatuni Upande Wa Kulia Na Umeme Ume Ganda Unit 2 Hauishi Wala Auingii Nn Tatzo?Ila Umeme Upo...
 
Mimi naulizia LUKU jioni hii ni vp? Najaribu kununua umeme naona naambiwa "muamala wangu haujakamilika, nijaribu baadae" Hiyo baadae sijui ni saa ngapi na umeme unaisha??!
Tunaomba mita namba yako mteja
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUTOKEA KWA HITILAFU KATIKA GRIDI YA TAIFA

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu Wateja wake waliounganishwa katika Mikoa iliyo katika Gridi ya Taifa kuwa leo Alhamisi Oktoba 26, 2017 majira ya Saa 12:03 Asubuhi imetokea hitilafu kwenye Gridi ya Taifa na kusabisha Mikoa hiyo kukosa umeme.

Mafundi wanafanya jitihada usiku na mchana ili kuhakikisha hali hii haijirudii na umeme unarejea katika hali ya kawaida kwa haraka

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi

TANESCO inaomba radhi kwa usumbufu unaojitokeza.

Tafadhali usishike wala kukanyaga waya uliokatika au kuanguka.

Toa taarifa kupitia namba za simu zifuatazo

Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400 na 0768 985100

Tovuti: www.tanesco.co.tz

Mitandao ya Kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu

Imetolewa na:-
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu

26/10/2017
 
Nauliza Mita Imetoa Kikatuni Upande Wa Kulia Na Umeme Ume Ganda Unit 2 Hauishi Wala Auingii Nn Tatzo?Ila Umeme Upo...
Asante kwa taarifa Mteja

Tunaomba utu DM namba yako ya simu
 
Mimi nina tatizo katika rimoti ambayo mita yake ni no. 24217849173 tuna miezi 6 tu toka umeme uingie na sasa aiwaki taa ya kijani na ina leta meseji ERR- 77 ili ni tatizo gani? Tukiingiza yuniti za umeme hazi ingii, siku tatu sasa. Naomba kujuzwa
 
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)

TAARIFA YA KUTOKEA HITILAFU MKOA WA KINONDONI KUSINI

Shirika la Umeme Tanzania Mkoa wa Kinondoni Kusini linawataarifu Wateja wake kuwa imetokea hitilafu kwenye kituo cha kupoza na kusambaza umeme Magomeni na kusababisha baadhi ya maeneo kukosa umeme kuanzia Jana Oktoba 26, 2017 hadi leo Oktoba 27, 2017

SABABU YA TATIZO
Hitilafu katika Breaket katika kituo cha Magomeni.

Mafundi wanaendelea na Jitihada zakurudisha Umeme.

*MAENEO YANAYOATHIRIKA*
Magomeni Mikumi, Magomeni kwa Shekh Yahaya, Mwembe chai, Kagera, Manzese, Argentina, Highway, na Manzese Midizini.

Imetolewa na
Ofisi ya Uhusiano
TANESCO Makao Makuu
27/10/2017
 
Mimi nina tatizo katika rimoti ambayo mita yake ni no. 24217849173 tuna miezi 6 tu toka umeme uingie na sasa aiwaki taa ya kijani na ina leta meseji ERR- 77 ili ni tatizo gani? Tukiingiza yuniti za umeme hazi ingii, siku tatu sasa. Naomba kujuzwa
Tumepokea mteja
 
Bonyeza 0nambaya mita0namba ya mita ok kisha itaandika good kisha ingiza umeme wako
 
Huku mbezi ya kimara umeme umekatika SAA kumi na moja kamili jioni hii....Tanesco mnatuharibia siku
 
Ni heri serikali itangaze rasmi kama kuna mgao wa umeme ili wananchi wachukue tahadhari mapema.
 
Back
Top Bottom