kimarabucha
JF-Expert Member
- Jul 29, 2017
- 791
- 621
Asante Mteja,Nachukua nafasi hii kuutaka uongozi Wa Tanesco Kigamboni ujaribu kuwa makini na utoaji Wa Huduma ya Umeme Kwa Wateja wake.Tanesco Kigamboni wamekuwa wanaongoza Kwa kukatakata umeme karibu mara 2 au 3 kila wiki na baya zaidi hata taarifa Kwa wateja wao hawatoi. Tunauomba uongozi Wa Tanesco Makao Makuu wauangalie uongozi Wa Tanesco Kigamboni nadhani kuna Shida kubwa.
kuna sehem ipo maneo ya kigambon mbele ya toangoma unaingilia mwembe mtemvu sehem inaitwa mkokozi au lugwadu mlisema mtaleta umeme mwezi wa tatu timeona kimya mkatumbia wa sita kimya tena na sasa mwez wa kumi vp tutegemee lini umeme utakuja maana asilimia kubwa ya wakaz wa huko wanasubir umeme tuAsante Mteja,
Kunamaboresho ya Miundombinu yanayoendelea maeneo ya Kigamboni.
Pia kunaujenzi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme.
Maboresho yakikamilika yataondoa tatizo la kukatika kwa umeme ama umeme kuwa mdogo
Lakini pia huwa tunajitahidi katika kutoa taarifa , mfano hii hapa tulitangaza
SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)
TAARIFA YA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA UMEMEMKOA WA TEMEKE
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Temeke kuwa kutakuwa na kazi ya maboresho ya miundombinu ya umeme kwa kufanya kazi ya kubadilisha nguzo zilizooza, kuimarisha viungio vya umeme na kukata miti inayogusa njia za kusambaza umeme, iliyolenga kuimarisha ubora na upatikanaji wa umeme Siku ya Jumanne, tarehe 24 Octoba,2017 kuanzia saa 03.00 Asubuhi hadi saa 12.00 jioni
Kutokana na matengenezo hayo baadhi ya maeneo yatakosa umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA
Kigamboni yote
Tafadhali usishike waya uliokatika toa taarifa kupitia simu zifuatazo:
Dawati la dharura Mkoa wa Temeke 0714485488, 0783360411, 0765654767 au
Kituo cha miito ya simu Makao Makuu 0222194400/0768 985 100.
Tovuti:www.tanesco.co.tz
Mitandao ya kijamii
www.facebook/twitter.com/tanescoyetu
Barua pepe:
customer.service@tanesco.co.tz
Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.
Imetolewa na:
Ofisi ya Uhusiano kwa wateja
TANESCO-TEMEKE
asante tumelipokea na tutalifanyia kazi
Mteja tumelichukua tutakupa mrejeshokuna sehem ipo maneo ya kigambon mbele ya toangoma unaingilia mwembe mtemvu sehem inaitwa mkokozi au lugwadu mlisema mtaleta umeme mwezi wa tatu timeona kimya mkatumbia wa sita kimya tena na sasa mwez wa kumi vp tutegemee lini umeme utakuja maana asilimia kubwa ya wakaz wa huko wanasubir umeme tu
Pole sana Mteja,Habari wanajamvi,
Naomba niwasilishe malalamiko yangu kwa Tanesco Mbezi ya Kimara. Kwa muda sasa wamekuwa na tabia ya kukata umeme angalau si chini ya mara 2 au 3 kwa siku.
Mfano kwa leo tu umeme ushakatwa mara 2 toka saa 9 alasiri!!! Je, kuna tatizo lolote linalosababisha kukatika kwa umeme frequently kiasi hiki?
Kero hii inatukumba sana wakazi wa Mbezi kuanzia Kwa Msuguli hadi Kibanda cha Mkaa!!! Tunaomba uongozi ushughulikie hili tatizo. Ni kero kwetu. Mfano kwa sasa umeme umekatika baada ya kurejea mida ya saa 1 usiku!!!
Haipendezi kwa kweli. Imani yangu wahusika watasoma hii post na kutafuta utatuzi wa jambo hili.
Mteja ipo kwa ajiri ya kujibu matatizo yote, utoaji na upokeaji wa taarifa maoni na ushauri pia.
Pengine swali halikuonekana samahani karibu uulize ili upate majibu
Eneo lipi na namba yako ya simu mpendwa mtejaNi kwa nini maeneo ya majohe gongo la mboto wilaya ya ilala huwa kuna matatizo ya umeme sana, hasa mvua zikinyesha, cha kushangaza hata inyeshe manyunyu tu ya robo saa umeme utakatika, hili tatizo nimeliona ni muda mrefu sana, sababu hasa ni nini?
Eneo lipi na namba yako ya simu mpendwa mteja
SHIRIKA LA UMEME TANZANIAMajohe kichangani, au plaza ukienda mpaka maeneo yote yanayozunguka ofisi za serikali ya mtaa. Tumia namba hii 0757617301