Dungu mteja token zako ni: 38102842227586130917

Tunaomba namba zako mpendwa mteja wetu

Mimi ni mkaazi wa UBUNGO RIVERSIDE tangu asubuhi hatuna umeme kwa baadhi ya nyumba, tumepiga cm tanesco lakini hawapokei cm zetu kulikoni?
Tunaomba namba yako ya simu

tarehe 07/11/17
muda : 15:10 alasiri
kiasi : 10000
namba : 0687237985
mita : 22124473921

namba token sijapokea
3810 2842 2275 8613 0917

Toka juzi usiku umeme kwangu umekatika na inaonekana tatizo lipo kwenye nguzo au waya za kuja kwenye Luku nipo Morogoro ,Changalawe jirani na Mzumbe University na nimeripoti juzi usiku nikapewa namba 0389 mpaka leo siku ya pili imeisha Tanesco hamjaja kila nikiulizia naambiwa wanakuja sasa sijui hiyo ni Emergency au ni after emergency mnakera sanaaaaa.....bora tuwe hata na Mashirika binafsi lbd tutaheshimiana....... Tooo much sijui

Tumeipokea mpendwa mteja kwa hatua zaidi

Nimeomba kuvutiwa umeme kwenye nyumba yangu mpya kigamboni lakini mpaka leo nazungushwa.

Nimejaza form mara mbili na mata mbili zote wamenilipisha pesa za watu kwenda ku ona site na nina amini hizo pesa ni rushwa na mpaka leo sijavutiwa umeme wakati hata jirani yangu ana umeme ninasikitika sana. Imefikia mahala naona bora niweke umeme wa solar.

Nafikiri kuna sababu nyingi za kuwaangalia vizuri hawa wanaopokea simu kutoka kwa wateja na wale wanaokutana na wateja moja kwa moja either kwa kuwaongezea mafunzo ya huduma kwa wateja au kuwakumbusha wajibu wao mara kwa mara maana na wao ni binadamu coz inafika wakati wanaiona kama tanesco ni mali yao binafsi.

Jitahidini sana mimi nilimepata shida sana week iliyopita nimelala giza siku tano bila sababu ya msingi na kila nikipiga huduma kwa wateja mbezi dah aisee ilinibidi nionyeshe rangi yangu halisi ndipo nilipata huduma haraka sasa najiuliza je kwa wenzangu na mimi sijui inakuaje.

Alafu niliuliza swali sikujibiwa ila kwa kuwa nilikua bize sikutaka kufuatilia, sikuwahi kupeleka malalamiko ya kuhusu mita ya luku niliyonayo na haikuwahi haribika lakini walikuja kuitoa na kufunga mita nyingine kisa ile mita ilikua na units nyingi alikua anakaa staff sasa najiuliza huo ndio utaratibu?

Na je hiyo mita inaenda fungwa wapi? Maana yake inaenda fungwa illegal au inabadirishiwa location na kulikua na sababu gani za kuitoa mita yote badala ya kufuta units tu? Mna utaratibu mpya siku hizi au?

Tunaomba taarufa kamilia ya unacholalamikia
Mkoa
Wilaya
Eneo
Mita namba
Tatizo
Namba ya simu

Ulivyolipa ulipewa stakabadhi yaani receipt? Ulimpa nani namba yako ya simu na jina uliloombea

Nguzo zikiwa 5 njia moja bei yake ni sh ngapi?
Tafadhali chukua fomu ya maombi ya umeme kisha tutapima na kukupa gharama ya makadirio kwa kuwa ni lazima gharama zote stahiki zibainishwe mara baada ya kufamya survey

Ndugu mteja Nguzo tano ni mradi, kwa maelezo zaidi tunaomba ufike Ofisi ya TANESCO iliyo karibu.

Hata tukiwatumia hamna msaada malizeni kwanza shida zenu na mkiwa teari kushirikiana na wana nchi ndo muombe mviombavyo ila kwa sasa huu ni upuuzi mtupu

Mbona ardhi ya wananchi wa same mjini mliochukua hamtulipi? Kilimo na ujnzi vyote vimesimama.

Mbona ardhi ya wananchi wa same mjini mliochukua hamtulipi? Kilimo na ujnzi vyote vimesimama.
Ndugu mpendwa mteja
Kwa swala lako tafadhali fika ofisi ya Wilaya ya Same kwa maelezo zaidi au tupayie taarifa za jina, eneo, namba ya simu, unachodai kisha tutawasiliana na wewe

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…