TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri
Nimetaka kujua muda ambao mteja akishalipa inabidi apewe huduma ndiyo swali langu
Ndio maana tumekuuliza maswali hayo kwa kuwa mteja hufungiwa umeme kutokana na umbali aliopo kutoka kwenye nguzo ya TANESCO au kama ni mradi taratibu zipo,tupatie hizo taarifa tukujibu kutokana na huduma unayohitaji
 
OK,nimelipa tarehe 10/11/2017 kwa jina la samwel mgasa hamisi hapa Mkoani Rukwa wilaya ya Nkasi nimelipa 177000,namba Yangu ni 0766211028
 
OK,nimelipa tarehe 10/11/2017 kwa jina la samwel mgasa hamisi hapa Mkoani Rukwa wilaya ya Nkasi nimelipa 177000,namba Yangu ni 0766211028
Wewe utafungiwa ndani ya siku 30 za kazi kuanzia siku umefanya malipo yako
 
TANESCO nyumbani kwangu nikinunua wa 2000 napata units 5.7 ila jirani yangu akanunua wa 2000 anatapa units 16 na mimi nina matumizi ya kawaida tu, kwanini kuna tofauti kubwa namna hiyo?
 
Asante kwa majibu yenu,nitarudi hapa ikipita siku 30 kama ulivyoandika

Yeye yupo tarif 4 wewe tarif 1 tafafhali tupatir namba yako ya mita na namba ya simu tukuangalizie
TANESCO nyumbani kwangu nikinunua wa 2000 napata units 5.7 ila jirani yangu akanunua wa 2000 anatapa units 16 na mimi nina matumizi ya kawaida tu, kwanini kuna tofauti kubwa namna hiyo?
 
Naomba kujua tariff plan zenu,kwani hamna consistence kabisa kati ya ninacholipia na matumizi yangu,nahisi nakua overcharged.

Pia Tangia Jana usiku huku Gezaulole Mwera-Kigamboni mshakata umeme Mara tatu sasa bila taarifa kuna tatizo gani na kwa nini hamtoi taarifa kabla?
 
Naomba kujua tariff plan zenu,kwani hamna consistence kabisa kati ya ninacholipia na matumizi yangu,nahisi nakua overcharged. Pia Tangia Jana usiku huku Gezaulole Mwera-Kigamboni mshakata umeme Mara tatu sasa bila taarifa kuna tatizo gani na kwa nini hamtoi taarifa kabla?
Tunaomba namba yako ya mita na simu
 
Habari ndugu? Mita ikiwa haionyeshi kioo vzr inaweza kubadilishwa na vipi utaratibu wake wakubadilisha hiyo meter ? Kuna gharama yyt? Na inachukua muda gani mpaka kubadilishiwa?
 
Habari ndugu? Mita ikiwa haionyeshi kioo vzr inaweza kubadilishwa na vipi utaratibu wake wakubadilisha hiyo meter ? Kuna gharama yyt? Na inachukua muda gani mpaka kubadilishiwa?
Hii iliwahi kutokea nikaenda ofsi za tanesco na kutoa taarifa, najua huduma hii ni bure jombaa
 
Tafadhali chukua fomu ya maombi ya umeme kisha tutapima na kukupa gharama ya makadirio kwa kuwa ni lazima gharama zote stahiki zibainishwe mara baada ya kufamya survey
Survey kasha pita shida analazimisha tulipie na extension ya laini kutoka waya mbili kuwa 4 kwa madai kwamba ya low voltage na nguzo ni nyingi mno za extension ni km 10 ukijumlisha na zetu 5 ni 15 na hii yote baada ya kugoma kump a chochote kitu na cha kushangaza zaidi kuna mwenzetu kaenda kulipia na kaungiwa na yy ni nguzo 2 na hakuambiwa hizo habari na distance za nguzo zimepitiliza si 50meter na kazi ili fanyika wikiend na ndo tabia yao huku kigamboni kufanya kazi za nguzo na kufungia watu luku wikiend na kila unaemuuliza alie fungiwa luku kwa design hiyo anakuambia yy kajiongeza je huu ni utaratibu au mnataka tuharibiane hizo ishu zinafanyika wilaya ya kigamboni naomba mkafanye uchunguzi wenyewe wale vijana wenu wa kusurvey hawafanyi kazi wanaendekeza rushwa na hayo mambo yamenishangaza sana huku kigamboni.

Hemu tumeni watu waje wafanye uchunguzi haraka kabla haija tokea aibu iliyo tokea mbagara hivi karibuni majuzi!!!!
 
Mradi wa umeme kwekitui kumalizia waya kwenye nguzo zilizosimama miaka mitatu bila kufungwa waya. mliahidi kuwa week ijayo mtatekeleza lakini hadi leo week tatu zimeisha na kesho inaaanza ya nne hakuna utekelezaji.
Nini tatizo?
 
Morogoro mjini tunakwenda kulipa umeme dirishani kuna mama/kibibi kikali kama pilipili na chenchi 50/100/200 anazuia.Dai Uone moto wake
 
Naomba kujua tariff plan zenu,kwani hamna consistence kabisa kati ya ninacholipia na matumizi yangu,nahisi nakua overcharged. Pia Tangia Jana usiku huku Gezaulole Mwera-Kigamboni mshakata umeme Mara tatu sasa bila taarifa kuna tatizo gani na kwa nini hamtoi taarifa kabla?
Tunaomba namba yako ya mita na simu

Mkoa gani... wilaya...eneo... namba yako ya simu tafadhali
Mradi wa umeme kwekitui kumalizia waya kwenye nguzo zilizosimama miaka mitatu bila kufungwa waya. mliahidi kuwa week ijayo mtatekeleza lakini hadi leo week tatu zimeisha na kesho inaaanza ya nne hakuna utekelezaji.
Nini tatizo?
 
Morogoro mjini tunakwenda kulipa umeme dirishani kuna mama/kibibi kikali kama pilipili na chenchi 50/100/200 anazuia.Dai Uone moto wake
Tunaomba namba yako ya simu tafadhali tukusikilize
 
Wilaya ya misungwi,tarafa ya usagara,kata ya Kanyelele,kijiji cha Mwaholo kwa nini zaidi ya nyumba 20 zinazohitaji umeme hamtski kuwawekea? Mmewekea watu wachache tens kwa ubaguzi.Ni lini mtaweka umeme?
 
Back
Top Bottom